Tafuta

Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na kuanguka kwa ndege nchini China Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na kuanguka kwa ndege nchini China 

Papa atuma salamu za rambi rambi kufuatia na ajali ya ndege,China

Katika telegeramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,ambayo imetumwa kwa Rais Xi Jinping, wa China, Papa Francisko anawakikishia sala zake kwa wote waliopoteza maisha katika ajali ya ndege na kwa ajili ya faraja wote wanaoomboleza kuondokewa na wapendwa wao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni habari ya kusikitisha sana kuhusu ajali ya ndege iliyoanguka huko China katika Wilaya ya Guangxi, na maisha mengi kupotea katika janga hilo. Kwa maana hiyo Papa Francisko ametuma salamu za rambo rambi kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Bwana  Xi Jinping.  Katika Telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Papa Francisko anawakikishia sala zake marehemu wote waliokufa na wakati huo huo kuwatia moyo na faraja wote wanaoomboleza kwa ajili ya wapendwa wao na kuwatakia baraka ya Mungu kwa kila mmoja wao.

Kuhusu taarifa za Ndege ya Boeing 737, ya ‘China Eastern Airlines’ yaani ya ‘ Kampuni ya Ndege ya Mashariki China”, inasemekena iliangukoa mara baada ya kupaa kwa kilomita elfu nane tu. Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na watu 132, miongoni mwao  abiria ni 123 na wafanyakazi 9. Ndege hiyo ilikuwa imeondaka baada ya saa saba mchana mahali hapo kutoka katika mji wa Kunming na ilikuwa inaelekea huko Canton,  karibu umbali wa 1,300 km.

23 March 2022, 16:09