Papa:tamaa ya madaraka inafanya kuwa watumwa.Usikubali kamwe!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tamaa na umaarufu, kuwa na uwezo, mali na mafanikio, yote ni sumu inayofanya kuwa utumwa na ambayo hufanya maisha kudanganywa. Kwa maana hiyo lazima kuwa macho. Amesema hayo Papa Francisko kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana katika Dominika ya kwanza ya Kwaresima, kwa waamini na mahujaji waliofika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 6 Machi 2022, akitafakari kuhusu Injili inayosimulia siku arobaini za Yesu akiwa jangwani, huku akijaribiwa mara tatu na shetani. Ibilisi yule yule ambaye pia anajionesha kwetu kwa macho matamu, kwa uso wa malaika na ambaye, Papa anmethibitisha katika tafakari yake kuwa hata anajua kujificha kwa sababu takatifu, zinazoonekana kuwa za kidini! Ni lazima tuwe macho, amesisitiza, ili tusijadiliane na vishawishi ambavyo mara nyingi hujidhihirisha katika hali ya dhahiri ya wema na, zaidi ya yote, kutokubaliana na uovu.
Majaribu ya Yesu ni sawa na majaribu yetu
Katika pambano hilo tuchukue mfano kutoka kwa Kristo, Papa Fransisko amesisitiza kwa waamini karibu elfu 25 waliokuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro, akikumbuka uzoefu wa Yesu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani, ambalo ni kielelezo cha mapambano dhidi ya ushawishi wa maovu ili kujifunza kuchagua uhuru wa kweli. Ni kupitia pambano hilo la kiroho ndipo anathibitisha kwa uhakika ni Masiha wa namna gani na a aneyekusudia kuwa nani. Yeye sio Masiha wa namna hiyo, bali Masiha wa namna hii. Papa ameongoze kusema: “Nitasema kwamba hii ndiyo hasa tamko la utambulisho wa kimasiha wa Yesu, wa njia ya kimasiha wa Yesu: 'Mimi ni Masiha, lakini katika njia hii'. Na ametazama kwa karibu majaribu ambayo Yesu anapambana nayo na ndio sawa sawa na yale ambayo yanatusindikiza hata sisi katika safari ya maisha.
Pendekezo la udanganyifu linakupeleka katika utumwa
Mara mbili shetani anamgeukia Yesu akisema: “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu...". Yaani anapendekeza kwake kutumia nafasi yake, ambayo kwanza kabisa ili kukidhi mahitaji ya kimwili anayohisi; kisha kuongeza nguvu zake; hatimaye kuwa na ishara ya ajabu kutoka kwa Mungu. Ni majaribu matatu, amefafanua, Papa. Ni kana kwamba anasema: “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, tumia fursa hiyo! Hiyo ni fikiria juu ya faida yako”. Ni pendekezo la kudanganya, lakini linaongoza katika utumwa wa moyo: inatufanya tuwe na tamaa ya kuwa na, inapunguzia kila kitu katika milki ya vitu, ya nguvu, ya umaarufu. Hiki ndicho kiini cha majaribu:nguvu ya mambo, ya umaarufu ... Ni sumu ya tamaa ambayo uovu umekita mizizi. Kristo anapingwa kwa njia ya kushinda kwa vivutio vya uovu.
Majaribu ndani mwetu yana mtindo mbali mbali
Yesu anafanya hivyo kwa kujibu majaribu kwa njia ya Neno la Mungu, ambalo linasema tusijifaidishe, tusimtumie Mungu, wengine na vitu kwa ajili yetu binafsi, sio kutumia nafasi ya mtu kujipatia mapendeleo. Furaha ya kweli na uhuru hautegemei kuwa na kitu, bali katika kushiriki; si kwa kuwadhulumu wengine, bali kuwapenda; si kwa kutamani sana mamlaka, bali katika furaha ya kuhudumia. “tutazame ndani yetu na tutaona kwamba majaribu yetu daima yana mtindo huu, njia hii ya kutenda, Papa anasema hayo mbali na kusoma tafakari yake kwamba “Ibilisi, ambaye ni mjanja, daima hutumia udanganyifu kwani alitaka kumfanya Yesu aamini kwamba mapendekezo yake yalikuwa ya manufaa kuthibitisha kwamba yeye alikuwa Mwana wa Mungu kweli. Lakini Yesu hazungumzi na shetani, Papa Francisko amesisitiza, “Yesu hakuzungumza na shetani kamwe.
Kamwe usiingie mazungumzo na shetani
Kamwe usiingie kwenye mazungumzo na shetani, yeye ni mwerevu sana kuliko sisi. Kamwe! amesisitza Papa. Inabidi kushikamana na Neno la Mungu kama Yesu na kujibu kila wakati kwa njia ya neno la Mungu. Na katika njia hii hatutakosea. Na hivyo ni lazima pia kufanya hivyo hata sisi. Na tukikubali kujipendekeza kwake, tunaishia kuhalalisha uwongo wetu, tukificha kuwa nia njema kwa kusema ‘Nilifanya biashara ya ajabu, lakini nilisaidia maskini’; 'Nilichukua fursa ya nafasi yangu, kama vile mwanasiasa, kama mtawala, kama kasisi, askofu, lakini pia kwa madhumuni mazuri'; 'Nilikubali silika yangu, lakini kimsingi sikumdhuru mtu yeyote', na kadhalika”. Papa ameongeza kuonya “Tafadhali katika uovu, hakuna maelewano! Pamoja na shetani, hakuna mazungumzo”.
Tuige Yesu haisiye tafuta makao wala mapatano na uovu
Hatupaswi kujadiliana na majaribu, hatupaswi kuangukia katika usingizi huo wa dhamiri unaotufanya tuseme: 'kimsingi sio mbaya, kila mtu anafanya hivi'! “, Papa ameonya. Ni jambo zito, yaani, kufikiri kwamba si jambo la maana sana: “Hebu tumtazame Yesu ambaye hatafuti makao, hafanyi mapatano na uovu. Kwa shetani yeye hupinga Neno la Mungu na hivyo hushinda majaribu”, Papa amehimiza. Kwa njia hiyo Papa ametoa mwaliko kuwa wakati huu wa Kwaresima uwe pia wakati wa jangwa kwetu, ambamo kuchukua nafasi za ukimya na sala. Kile kidogo kitatufanyia mema, katika nafasi hizi tuache; tuangalie kile tunachochochea mioyoni mwetu kile kinachosisimua mioyoni mwetu, ukweli wetu wa ndani, kile tunachojua hakiwezi kuhesabiwa haki ”.Tufanye uwazi wa mambo ya ndani, tukijiweke wenyewe mbele ya Neno la Mungu katika sala, ili mapambano ya manufaa dhidi ya uovu unaotutia utumwani, mapambano ya uhuru, yafanyike ndani yetu”.