Tafuta

2022.03.24  Papa Francisko amekutana na wanachama wa Kituo cha Wanawake Italia. 2022.03.24 Papa Francisko amekutana na wanachama wa Kituo cha Wanawake Italia. 

Papa Francisko:Mabadiliko yanahitajika na si ununuzi wa silaha

Papa Francisko akizungumza na wanachama wa Kituo cha Wanawake Italia amesema wanawake wanaweza kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko ikiwa hawajaunganishwa na mfumo wa sasa wa madaraka.Nia ya kutawala haijibiwi kwa vurugu na uchokozi zaidi,lakini kwa njia tofauti ya kuelewa uhusiano wa kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 24 Machi 2022 amekutana na wajumbe wa Kituo cha Italia cha wanawake. Katika hotuba yake amemshukuru Mwenyekiti wa chama hicho kwa Renata Natili Micheli, kwa maneno yake ambayo amefafanua mkutano huo. Amemsifu alivyo jasiri kijana huyo na kwamba wamefika Roma kufanya Mkutano wa uchaguzi ambao umeongoza na mada pana yenye “Utambulisho wa uumbaji wa mwanaume na mwanamke katika ushirikishano wa utume”. Amewatakia kazi njema na kuwashiriki kwa mchango wao wanaotoa katika mazungumza kuhusu mada hiyo ya utambulisho. Ni sauala la sasa, na si tu kuhusiana na maana ya kinadharia, lakini kwa maana ya kuishi, katika maisha ya watu, hasa kwa watoto wa kike na kiume ambapo katika makuzi, wanahitaji sehemu ya kuiga mfano, watu wazima ambao wanaweza kukabiliana, kwa maana hiyo wanaume na wanawake. Papa amependa kuwashukuru hasa kwa uwepo wao kwa sababu nchini Italia wako mbele zaidi kwa chama cha wanawake ambacho kinahishwa na Injili na wanataka kuzungumza na wote kwa ajili ya wema wa jamii. Hiyo haiwezi kutozingatiwa!

Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia
Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia

Kituo cha Italia cha wanawake kilizaliwa katika muktdha wa kutetea hadhi na haki ya mwanamke, katika kipindi kilichokuwa cha utajiri, wenye matunda kwa Italia yaliyopatikana mara baada ya vita ya II ya Dunia. Katika muktadha huo wa nguvu ulikuwa na ncha ya kiitikadi na ndiyo Kituo cha wanawake (CIF) Italia kilianzishwa kama chaguzi na uwajibikaji wa kulinda ubinadamu. Ilikuwa ni uchaguzi ambao leo hii unaitwa utamaduni wa kutunza, mbadala wa utamaduni wa kunyonya na wa kumiliki. Historia ya miaka sabini iliyopita inathibitisha hili: vita vya kikanda havijawahi kukosekana, na  ndiyo maana Papa alikwisha sema kuwa tulikuwa katika vita vya tatu vya dunia  vilivyo gawanyika vipande vipande. Kila mahali kidogo, hadi leo hii, ambayo ina mwelekeo mkubwa na inatishia dunia nzima. Lakini tatizo msingi ni lile lile: tunaendelea kutawala dunia kama “chessboard” yaani “mchezo wa Dana”, ambapo wenye nguvu hutafiti namna ya kuchuukua hatua ya kupanua utawala kwa madhara ya wengine au kuongeza utawala kwa madhara ya wengine, Papa amesisitiza. Jibu la kweli kwa hiyo si silaha nyingine,au  vikwazo vingine; Papa ameongeza: “ lakini,nilipata aibu niliposoma kwamba sijui, kundi la Nchi limejitolea kutumia asilimia mbili, nafikiri, au mbili kwa kila elfu la Pato la Taifa kwa ajili ya ununuzi wa silaha, kama jibu kwa kile kinachotokea sasa ... wazimu, huh? Jibu la kweli, kama nilivyosema, si silaha nyingine, au vikwazo vingine, miungano mingine ya kisiasa na kijeshi, bali ni mbinu nyingine,  yaani njia tofauti ya kuitawala dunia, bila kutoonesha meno, kama wafanyavyo sasa, hapana? na kuanzisha mahusiano ya mazungumzo kimataifa. Mtindo matibabu tayari umewekwa, asante Mungu, lakini kwa bahati mbaya bado iko chini ya ile ya nguvu za kiuchumi-kiteknolojia-kijeshi”.

Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia
Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia

Papa Francisko ameeleza pia ni kwa nini ameamua kufanya tafakari hii kwamba wao ni chama cha wanawake na wanawake mi wahusika wakuu  wa mabadiliko hayo Isipokuwa hazijaidhinishwa na mfumo wa nguvu uliopo. Ilimradi wahifadhi utambulisho wao kama wanawake. Katika suala hili, Baba Mtakatifu amegependa kurejea kifungu kutoka katika Ujumbe wa Mtakatifu Paulo VI kwa wanawake, mwishoni mwa Mtaguso wa II wa Vatican. Anasema: “Saa imefika, saa imefika, ambayo wito wa wanawake umekamilika, saa ambayo mwanamke anapata mvuto, mwanga, uwezo ambao haujawahi kupatikana katika jamii. Ni kwa sababu hiyo, katika wakati huu ambapo ubinadamu unapitia mabadiliko hayo makubwa, kwamba wanawake waliojazwa na roho ya Injili wanaweza kufanya mengi ili kusaidia wanadamu wasioze” (nn. 3-4), amemaliza kunukuu. Kwa kuendelea amesema “ Nguvu ya kinabii ya usemi huu ni ya kuvutia. Hakika, kwa kupata nguvu katika jamii, wanawake wanaweza kubadilisha mfumo na wanaweza kabisa ikiwa watasimamia, kubadilisha nguvu ya kutoka katika mantiki ya kutawala kufika ile ya  huduma, na ya utunzaji”.

Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia
Papa amekutana na wanachama cha wanawake Italia

Papa alitaka kuzungumza juu ya hili na wao ili kujikumbusha mwenyewe na kila mtu, kuanzia na sisi Wakristo, kwamba mabadiliko haya ya mawazo yanahusu kila mtu na inategemea kila mmoja. Ni shule ya Yesu iliyotufundisha jinsi Ufalme wa Mungu hukua kutoka kwa mbegu ndogo sikuzote. Ni shule ya Gandhi, ambayo iliongoza watu kwenye uhuru kwenye njia ya kutokuwa na vurugu. Ni shule ya watakatifu wa nyakati zote, wanaofanya ubinadamu ukue kwa ushuhuda wa maisha yaliyotumika katika huduma ya Mungu na jirani. Lakini pia Papa amesisitiza juu ya shule ya wanawake wengi ambao wamekuza na kulinda maisha; ya wanawake ambao wameponya udhaifu, ambao wameponya majeraha, ambao wameponya majeraha ya kibinadamu na kijamii; ya wanawake ambao wamejitolea akili na mioyo yao kwa elimu ya vizazi vipya. Nguvu ya mwanamke ni kubwa! Papa aemeendelea kusema “Kuna msemo mmoja zaidi ya msemo ni tafakari: ikiwa mwanume ambaye bado ni kijana  anabaki mgane ni vigumu kwake kujisimamia. Mwanaume hawezi kuvumilia upweke mkubwa namna hiyo. Lakini ikiwa mwanamke anakuwa mjane, anajiweza, anavumilia: yeye hubeba familia, hubeba kila kitu. Je mnaweza kuelezea utofauti hii.  Ni igwiji wa kike.  Huo ndiyo ugwiji wa kike. Mfano huu unaangazia ukweli huu vya kutosha”. Papa Francisko amesisitiza

Utamaduni wa utunzaji, ukarimu, utamaduni wa kuwa karibu, Papa amesisitiza kuwa wao wanaiishi kwa kuchota katika Injili. Wamefunza katika Kanisa mama na mwalimu na kwa kujifanya wao wenyewe kusitawisha maisha ya kiroho kwanza kabisa ndani yao  wenyewe, kutunzana, katika urafiki, kwa kujaliana, hasa nyakati za shida, kwa kusali kwa Mungu na kwa ajili ya kila mmoja, si kusemana  juu ya mmoja,  hapana, hiyo si sawa”. Kwa kuhitimisha Papa amesema kwa haya yote anawashukuru na amewahimiza waendelee mbele. Kama vyama vingine vya kihistoria vya Kikatoliki, pia la kwao limebadilika kutokana na mabadiliko katika jamii ya Italia. Kwa sababu hiyo, ni vizuri piakupunguza" kutokana na miundo ambayo imekuwa isiyoweza kudumu, kujitolea bora kwa elimu na uhuishaji wa kitamaduni na kijamii. Bikira Maria daima awasindikize, ambaye katika tutatafakari ya katika Siku Kuu ya Kupasha habari kwa Bikira Maria 25 Machi 2022 amewabariki  wanachama waliokuwapo na wale walio dhaifu zaidi.

HOTUBA YA PAPA LWA WANACHAMA WANAWAKE WA ITALIA
24 March 2022, 17:51