Makombora ya Urussi kuipiga Ukraine Makombora ya Urussi kuipiga Ukraine 

Papa Francisko:vita hivi ni aibu kwa wanadamu wote!

Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Matangazo ya Radio kwa Kiitaliano C.B,katika Ukumbi wa Paulo VI.Akiwahimiza shughuli ya kujitolea katika ulinzi wa raia na mshikamano na watu walio hatarini zaidi,hasa wakimbizi kutoka Ukraine, ametoa mwaliko wa kuwasaidia sio mara moja tu,lakini kufikiria siku zijazo ambapo kutakuwa na mahitaji zaidi ya sasa.Amerudia kupongeza tena juhudi za watu wa kujitolea nchini Italia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Shirikisho la matangazo la Italia” na kumshukuru Mwenyekiti kwa maneno yake ya utamngulizi ambayo yemekumbusha historia ya chama cha Italia cha kujitolea kwa njia ya Radio na jitihada kuu za kujitolea. Shirikisho hilo limetawanyika kwa mapatano na harakati nyingi za watu wa kujitolea Italia ambao Papa amesema haishi kamwe kupongeza na ambao wanastahili kutiwa moyo na kusaidiwa. Shirikisho lao kwa namna ya pekee mwaka jana wamehitimisha miaka 50  hivyo amewapongeza. Wanaweka shauku yao kama mastaa wa radio katika huduma ya jamii. Wamefanya kuwa chombo muafaka wa ajili ya huduma ya ulinzi wa raia na mshikamano wa watu wenye kuhitaji zaidi, wadhaifu na makundi ya kijamii yenye matatizo. Hiyo ni nzuri sana, upendo mkuu kibinafsi ambayo imegeuka kuwa huduma ya kijamii. Ni msingi wa zawadi, wa talanta ambazo wameweza kuzifanya zizae kwa wema wa pamoja. Tabia yao ya utendaji ni ile ya haraka katika kuingilia kati, shukrani kwa radio ambayo inavuka mipaka, lakini hata shukrani kwa masafa yao. Kwa hakika sio tando la kibinafsi, nguvu yao hasa iko katika uwepo wa masafa ya taifa na katika uwezekanao wa kufanya taarifa na habari zizunguke kwa haraka na kila sehemu. Na mantiki nyingine ni ule ya uhuru, ya kujitegemea. “Tunafikiri jinsi hii inaweza kuwa ya uamuzi ambapo serikali au kituo kingine cha mamlaka kinataka kudhibiti mawasiliano. Ni muhimu kudumisha uhuru, ili kuwa kweli katika huduma ya watu, ya manufaa ya wote”.

Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea
Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea

Pongezi kwa Ulaya kujikita kusaidia dharura ya wakimbizi

Papa ameeleza alivyosika kwamba wanajikita kutoka hata mchango wa shughuli za ndugu kaka na dadfa wengi waliokimbika kutoka Ukraine kwa sababu ya vita. Amewashukutu kwa hili. Ni matarajioa na kusali ili vita hivi viishie haraka, havikubaliki, ni ya aibu kwa wote na kwa ubinadamu wote, kila siku wanaongezeka vifo vingine na uharibifu. Watu wengu wameweza kuamkana na kusaidia wakimbizi. Watu wa kawaida, hasa katika Nchi zinazopakana, hata Italia, mahali ambapo wamefika na wanaendelea kufika maelfu ya waukraine. Mchango wao ni wenye thamani, kwa namna ya dhati, kiufundi kwa ujenzi wa amani. Papa Francisko ameunga mkono aliyosema Mwenyekiti wao akizungumza juu ya Ulinzi wa Rais Ulaya “Ulaya kwa kutoa jibu la vita hii zaidi ya mipango ya Taasisi nyingine, hata juu ya mpango wa jamii ya kiraia, ya vyama vya kujitolea kama yao. Huo ndio mtundo wa kuanza kwa upya, msingi na unaweza kufanya kuuunganisha kiini cha kibinadamu, na kijamii, kwa uwepo wa jereha kubwa hili kama linavyosababishwa na vita. Na kuwasaidia wakimbizi wa Ukraine si tu kwa wakati wa sasa lakini baadaye mbele zaidi, wakati vita vitakuwa kumbu kumbu kwa sababu wakati huo watakuwa na matatio makubwa zaidi ya sasa, kwa sababu sasa hivi tuko pamoja na badaye… Ni lazima kufikiria wakati ujao. Na sio rahisi” Papa amebainisha. Papa amehitimisha kwa kuwashuru tena na kuwakia mema katika shughuli zao, Daima waendelea ule uhuru na mshikamano. Watazamie mema ya pamoja na siyo mafao ya upande. Kuwa na upendeleo wa kitu kimoja “maskini, wasio na mlinizi, na walioachwa. Amewabariki.

Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea
Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea

Kuhusiana shirikisho la matangazo Italia

Shirikisho la matangazo la Italia “Federazione italiana ricetrasmissioni - Citizen's Band”, linajulikana kwa FIR CB au FIR CB - SER au FIR – SER ni shirikisho la kitaifa lililoundwa awali na vilabu vya radio vya CB vilivyozaliwa kwa hiari, hata kabla ya kuhalalishwa kwa CB, katika eneo la kitaifa la Italia, na baadaye na vyama vya hiari vinavyofanya kazi hasa katika sekta ya radio. Shirikisho hilo ni sehemu ya Shirikisho la CB la Ulaya (ECBF) na Umoja wa Bendi ya Wananchi Duniani (WCBU). Shirikisho hilo lilizaliwa mnamo Februari 1971, wakati masafa transceivers katika bendi ya wazalendo walikuwa bado hawajahalalishwa nchini Italia. Utambuzi rasmi wa CB ulifanyika kwa kuanzishwa kwa gombo jipya la posta kupitia D.P.R. 156/73 mnamo Machi 1973. Baada ya tetemeko la ardhi la Friuli la 1976, ambapo waendeshaji wa CB pia walitoa usaidizi wao katika kazi ya uokoaji, wazo lilizaliwa kuunda, ndani ya shirikisho, muundo wa kujitolea kwa dharura, kutoa maisha kwa ajili ya Huduma ya Dharura ya Radio.

Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea
Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea

Huduma ya dharura ya radio

Huduma ya Dharura ya Radio, kwa kifupi SER, ni tamko la moja kwa moja la CB FIR na hutoa huduma ya ulinzi wa raia wa shirikisho lenyewe. Huduma hii mara nyingi hutambuliwa kwa kifupi FIR - SER. Kazi ya SER ni kuhakikisha viunganishi vya radio katika ngazi zote, kuanzia ile ya mtaa (manispaa, kati ya manispaa na mkoa) hadi ile ya kimkakati (ya kikanda na kitaifa). Marudio yanayotumika kwa kawaida ni chaneli za kawaida za CB, lakini masafa mengine yanayotolewa kwa utendakazi wa Idara ya Ulinzi wa Raia (bendi ya 160 MHz na 43 MHz) au masafa ya VHF au UHF yaliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano kwa miundo pia yanaweza kutumika kwa vyama vya SER. Kwa miaka mingi, FIR CB imeshiriki katika dharura na matukio makubwa ambayo yamefanyika katika eneo la kitaifa, ikiwa ni pamoja na: Tetemeko la ardhi la Friuli (Mei-Septemba 1976); Sarno (Mei 1998); Utume wa Upinde wa mvua (1999); Kuvamia kwa barafu ya Belvedere ya Mlima wa  Rosa (Juni 2002);  matukio ya milipuko na matukio ya mitetemo yaliyounganishwa na shughuli ya volkeno ya Etna (Oktoba 2002); matukio ya tetemeko katika jimbo la Campobasso (Oktoba 2002);  matukio ya angahewa Liguria, Lombardia, Piedmont, Veneto, Friuli, Emilia-Romagna (Novemba 2002);  mazishi ya Baba Mtakatifu Yohane Paulo II (Aprili 2005); uchaguzi wa Papa Benedict XVI (Aprili 2005); Tetemeko la ardhi la Abruzzo (Aprili-Desemba 2009).

Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea
Papa Francisko akutana na Shirikisho la Italia la Matangazo na huduma ya kujitolea
HOTUBA TA PAPA YA SHIRIKISHO LA MATANGAZO ITALIA
28 March 2022, 10:07