Papa Francisko:tuache tuguswe kwa kina na mateso ya ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Kanisa mama la Jumuiya ya Shirika la Yesu (Wajesuit) Roma Papa Francisko ameshiriki katika Misa Takatifu katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 400 tangu kutangazwa kuwa watakatifu: Mjesuit Ignazio wa Loyola na Francis wa Xaveri,Mkalimeli Teresa wa Avila, Filippo Neri na mlei, Isidori mkulima. Aliyeongoza ibada Misa Takatifu hiyo alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Yesu, Padre Arturo Sosa, Jumamosi jioni tarehe 12 Machi 2022. Wakati mahubiri yalitolewa na Baba Mtakatifu Francisko ambapo kwa kuongozwa na Injili ya 'Kugeuka Sura kwa Yesu' imempatia fursa ya tafakari kuhusu matendo manne yaliyofanywa na Yesu, ambayo kwayo inawezekana kabisa kupata habari muhimu kwa kuchukulia wito wetu binafsi na historia ya jumuiya yetu kila siku; kupaa kuelekea kwenye mipaka iliyooneshwa na Mungu, kwa kutoka nje ya nafsi zetu; kuona ili kugeuza ulimwengu ambamo tumezamishwa; na kubaki, sehemu ambayo ni kuwa makini ili kulinda mambo muhimu ya maisha ambayo hayapiti, Papa amebainisha.
Kwa maana hiyo Papa amekumbusha kwamba hatua ya kuwa wanafunzi daima huanza na Yesu, ambaye anapenda, kuchagua na wito. Hivyo ameangazia kile kilicho kwenye chimbuko la fumbo la taaluma: neema, uchaguzi, ambao unatarajia maamuzi yetu yoyote. Ni yeye aliyetuita, bila sifa zetu. Kabla ya kuwa wale waliofanya maisha kuwa zawadi, sisi ndio tulipokea zawadi ya bure amesisitiza, Papa. Mungu anatuongoza akiwa ametushika mkono hadi marudio ya njia ya Kikristo ambayo ni mlima wake mtakatifu, ambapo tayari sasa anatuona milele pamoja naye, tukigeuzwa sura na upendo wake. Neema inatuongoza huko. Kwa hiyo, tunapohisi uchungu na kukatishwa tamaa, tunapohisi kudharauliwa au kutoeleweka, tusipotee katika majuto na kukata tamaa. Ni majaribu ambayo yanapooza njia, njia zisizoongoza mahali popote amesema Papa.
Badala yake, Papa amesisitiza kuwa tuchukue maisha yetu mkononi kwa kuanzia na neema. Na tunakaribisha zawadi ya kuishi kila siku kama njia ya kufikia lengo. Papa amesisitiza juu ya uzuri wa mwelekeo wa jumuiya ambamo wito umekita mizizi yake, katika mwanga wa ukweli kwamba Yesu huchukua wanafunzi pamoja. Kwa hiyo amesisitizia ndugu zake Wajesuit kwamba wanahitaji kufufua neema ya kuchukuliwa ndani ya Kanisa, Mama yetu mtakatifu wa daraja la juu, na kwa ajili ya Kanisa, wenzi wetu. Sisi ni wa Yesu, na sisi ni kama Kampuni”. “Tusichoke kuomba nguvu ya kujenga na kulinda ushirika, kuwa 'chachu ya udugu' kwa Kanisa na kwa ulimwengu. Sisi si waimbaji wa pekee katika kutafuta kusikiliza, lakini ndugu waliopangwa katika kwaya. 'Tunajisikia pamoja na Kanisa', tunakataa jaribu la kutafuta mafanikio ya kibinafsi na kutengeneza kamba. Tusikubali kuingizwa kwenye upadre unaokaza na itikadi zinazogawanyika”.
Haya ni maneno ambayo Papa Francisko yalisikika mwangi hasa alipowafafanua watakatifu wanaokumbukwa kuwawao ni 'nguzo za ushirika' kwani “wanatukumbusha kwamba huko Mbinguni, licha ya kutofautiana kwa wahusika na mitazamo, tunaitwa kuwa pamoja”. Ni kifungo hiki cha uzima wa milele ambacho tumeahidiwa kwamba tunaweza kuanza kuupitia sasa hivi”, amependekeza Papa. Akiendelea pia amejikita kwenye kitenzi cha kupaa kwa kutumia taswira za kufikirika. Papa amesema: “Njia ya Yesu sio mteremko, ni mpando kwani nuru ya kugeuka sura haifikii uwanda, lakini ni baada ya safari yenye uchovu. Kumfuata Yesu kwa hiyo ni lazima kuacha tambarare za wastani na miteremko ya faraja; ni muhimu kuacha tabia ya mtu ya kumtuliza ili kufanya 'harakati ya kutoka'. Kupanda kuelekea msalaba kunaongoza kwenye lengo la utukufu, na kwamba kuwa na majaribu ya ulimwengu ni kutafuta utukufu badala yake bila kupitia msalaba. Na akitazama jinsi Bwana alivyomtoa Ibrahimu katika nchi yake, anaeleza:
"Tungependa njia zinazojulikana, zilizonyooka na zilizo sawa, lakini ili kupata nuru ya Yesu ni muhimu kuendelea kutoka nje ya nafsi yako na kupanda juu nyuma yake. Kwa kufafanua vema jambo hili katikamahububiri yake amekumbuka jinsi katika Maandiko kwamba "kilele cha milima kinawakilisha mwisho, kikomo, mpaka kati ya dunia na mbingu". Na kwa hiyo amerudia kutoa mwaliko huo huo kwa: “Tumeitwa tutoke twende pale pale, ‘kwenye mpaka kati ya dunia na mbingu’, ambapo mwanadamu humkabili Mungu kwa shida; anamkabili Mungu kwa sababu ya matatizo; kushiriki utafutaji wake usio na wasiwasi na shaka yoyote ya kidini. Tunapaswa kuwa pale na kufanya hivyo tunahitaji kutoka na kupanda. Ingawa adui wa asili ya mwanadamu anataka kutushawishi turudi nyuma kwa hatua zile zile, zile za kurudia-rudia, za kustarehesha, zile ambazo tayari zimeonekana, Roho hupendekeza fursa, hutoa amani bila kuacha amani, huwatuma wanafunzi kwenye mipaka iliyokithiri. Kwa kutoa mfano ameomba kumfikiria Francis wa Xaveri” amesisitiza Papa.
Papa Fransisko katika hilo amekumbuka jinsi Ibrahimu alivyopambana kutengeneza njia hiyo. Na amerudia kusema jinsi ilivyo muhimu kupambana ili kulinda njia hii, njia hii ya kujiweka wakfu kwa Bwana". Papa Francisko ametazama kwa kina njia ya mpando daima, katika kila zama, inayojionesha kwa kila mfuasi. Anabainisha hatari ya imani tulivu na ametumia neno imeegeshwa ili kufafanua kwa njia ya kitabia. Amekwenda mbali na kusema kuwa anaogopa kutaja pete za harusi zilizoegeshwa. Hatari iliyopo ni kujiona kuwa wanafunzi wenye adabu, ambao kiukweli hawamfuati Yesu bali wanabaki kimya, bila kufanya kitu na kama Injili Tatu zinavyoeleza waliosinzia na kulala.
Hata huko Gethsemane, wanafunzi hawa walilala. Kwa njia hiyo wale wanaomfuata Yesu sio wakati wa kulala, yaani kuruhusu roho iwe na madawa ya kulevya, kupigwa na hali ya hewa ya kisasa ya walaji na ya mtu binafsi, na kufanya kana kwamba maisha ni sawa ikiwa mimi niko sawa, ambayo kwayo tunazungumza na kinadharia, lakini tunapoteza kuona mwili wa ndugu, ambao ni usahihi wa Injili. Janga la wakati wetu ni kufumba macho yetu juu ya ukweli na kugeuka kisogo. Papa Francisko aidha amemwomba Mtakatifu Teresa, ili atusaidie kutoka ndani yetu na kupanda mlima pamoja na Yesu, kwa kutambua kwamba Yeye pia anajidhihirisha kupitia majeraha ya ndugu zetu, kazi ya ubinadamu, ishara za nyakat". Papa ametualika tusiogope kugusa majeraha, kwa sababu amesema ni majeraha ya Bwana. Kwa hiyo anachosema Papa kuhusu kuomba hakiwezi kushindwa kurejea katika wakati huu wa vita. Na hivyo mambo yanaweza kuwa mazoea na ndiyo ametoa mwaliko wa kujiuliza maana yake, baada ya miaka mingi ya huduma, hasa kwao kama wanashirika kwamba ni lazima wasali.
Labda nguvu ya mazoea na ibada fulani ilitufanya tuamini kwamba sala haibadili mwanadamu na historia. Badala yake, kusali ni kubadilisha ukweli. Ni utume hai, maombezi endelevu. Sio umbali kutoka kwa ulimwengu, lakini mabadiliko ya ulimwengu. Kuomba ni kuleta mpigo wa moyo wa habari kwa Mungu ili macho yake yafunguke katika historia. Itatufaa Papa amebainisha kujiuliza ikiwa maombi yanatuzamisha katika mabadiliko haya; ikiwa yanatoa mwanga mpya kwa watu na kubadilisha hali. Kwa sababu ikiwa sala ni hai, inapasha ndani, inawasha tena moto wa utume, inawasha tena furaha, hutuchokoza mara kwa mara ili tufadhaike na kilio cha mateso ya ulimwengu. Papa ameomba tujiulize maombi yetu yakoja katika vita inayoendelea. Anasema hayo mara mbili, Papa Francisko: ”Je tunaomba namna gani kuhusiana na vita? Papa ameomba kuwa na mtindo kama ule wa Mtakatifu Filippo Neri ambaye moyo wake ulipanuka kwa kumfanya afungue milango kwa watoto wa mitaani, ambaye anaweza kuwa msaada. Au ile ya Mtakatifu Isidori, ambaye aliomba shambani na kuleta kazi ya kilimo katika maombi.
Hatimaye, Papa Francisko amejikitakatika kifungu cha kibiblia chaliturujia ya Injili iliyosomwa yaani sura hiyo ya Yesu inayobaki. Papa amesema "Injili inahitimishwa kwa kuturudisha kwenye yale yaliyo muhimu ambapo mara nyingi tunajaribiwa, katika Kanisa na ulimwenguni, katika hali ya kiroho kama ilivyo katika jamii, kufanya mahitaji mengi msingi yawe ya pili. Kwa maneno mengine, Papa ameeleza kuwa tunahatarisha kuzingatia mila, desturi na tamaduni ambazo huweka moyo juu ya kile kinachopita na kutusahaulisha kinachobaki au kudumu milele. Kwa njia hiyo ni jinsi gani ilivyo muhimu kufanya kazi kwa moyo, ili kujua jinsi ya kutofautisha kile kinacholingana na Mungu, na kinadumu, kutoka katika kile kinachoendana na ulimwengu, na kinapita! Maombi la mwisho Papa amembusha kwamba urithi wa thamani ambao ni utambuzi wa Ignatius yaani Mtakatifu Ignatius utusaidie kutunza, hazina ya milele inayomiminwa juu ya Kanisa na juu ya ulimwengu. Ni ile lenzi inayoturuhusu kuona mambo yote mapya katika Kristo. Papa amehitimisha mahubiri yake kwa kueleza imani umuhimu ya utambuzi, kwa ajili yetu wenyewe na kwa ajili ya Kanisa. Hapo aamemnukuu Pietro Favre: "Mema yote yanazoweza kutimizwa, kwa kufikiria au kupangwa, lazima yafanywe kwa roho nzuri na sio ile mbaya" (Memorial, Paris 1959, n. 51).
Matashi mema ya Padre Sosa kwa Papa kwa miaka tisa ya upapa wake
Mwishoni mwa Misa Takatifu, Mkuu wa Shirika la Yesu akizungumza kwa niaba ya wote wanashirika ametoa shukrani kwa Bwana ambaye anaendelea kuwasindikiza katika uongofu huu wa kina wa mambo ya ndani: “Kwa niaba ya Wajesuit na familia nzima ya Ignatius, tunamshukuru Baba Mtakatifu kwa uwepo wako katika maadhimisho haya, ambayo ni ishara ya usindikizaji wako wa kudumu na wa kuzingatia katika huduma ya Kanisa”. Na, katika mkesha wa kumbu kumbu ya mwaka wa tisa wa kuchaguliwa kwake kuwa askofu wa Roma, Padre Sosa ameomba neema nyingi katika kutimiza huduma yake ya Mtume Petro. Zaidi ya hayo, Mjesut ameomba, kulingana na amelekezo ya Loyola mwenyewe, “neema ya kuona mambo yote katika Kristo katika wakati huu na kwambaa iliyojaa mshangao ambao tunaishi.
Kwa kuongezea tena, sala kwa Maria wa Nazareti ambaye kwake hakuna lisilowezekana. Hatimaye, Padre Sosa aliwasilisha kwa Papa wanawake kumi wanaokimbia vita na mateso waliokaribishwa katika kituo cha Astalli cha kijesuit. Wamemzawadia Papa Francisko orodha ya maonesho ya picha ya Nyuso kwa siku zijazo, ishara ya kujitolea kwa wanaume na wanawake katika miaka arobaini ya shughuli kwa ajili ya wakimbizi, na begi ya turubai ya rangi iliyotengenezwa pamoja katika kipindi cha janga: tunda, pia hili la kujitolea mara kwa mara kwa ajili ya amani.