Papa Francisko:Tofauti zilizopatanishwa:mprotestanti katika gazeti la Papa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Duka la vitabu Vatican, (Lev) kimechapishwa kitabu kimoja chenye kichwa “Tofauti ziliozopatanishwa”. Mprotetanti katika gazeti la Papa kilichondikwa na Marcelo Figueroa kwa ajili ya “Uekumene wa matumbo”. Kitabu hicho kinakusanya kwa namna ya pekee makala nyingi zenye mchango mbali mbali na mahojiano yaliyochapishwa na mtunzi huyo katika gazeti la Osservatore Romanao. Kitabu hicho kina dibaji ya Papa Francisko ambapo mtunzi huyo alisaini tangu 2016 ambaye ni mprotestanti wa kwanza katika historia ya kila siku katika gazeti la Osservatore Romano. Zaidi ya miaka 20 ni rafiki binafsi wa Papa Bergoglio, Kuhani wa kanisa la Kipresbiteriani nchini Argentina, Figueroa anakabiliana na mada nyingi ambazo zumekuwa kiongozi katika muktadha wa safari ya kiekuemene kati ya Makanisa.
Baba Mtakatifu katika dibaji yake anandika akionesha furaha kubwa ya kazi hiyo ya fasihi ambayo ina mwonekano zaidi, mwanzoni, wa kitabu cha mazungumzo kati ya dini, lakini ndani yake mtu anagundua, kwa kuifuata, karibu hija ya kiekumene ambayo ni halisi, ya kibinafsi na zaidi ya yote, ya kiroho. Yeye binafsi amependa neno ambalo kuhani Marcelo Figueroa alitumia aliponiwasilisha rasimu ya kazi yake: “Niliiandika kutoka katika matumbo yangu!”. Kwa miaka mingi, na unaweza kuuona katika kitabu hicho, kuna uekumene wa kivumishi kama uekumene wa upendo, matumaini, huruma, mshikamano, amani. “Mimi mwenyewe nilitumia usemi wenye nguvu, nikijaribu kuamsha uhalisia unaotuunganisha kuanzia kwenye mishipa iliyo wazi ya ndugu wengi sana na Neno aliyefanyika mwili mwenyewe, akiteseka na kuomba kwa ajili ya umoja (taz. Yh 17:1), ule wa “uekumene wa damu”.
Baba Mtakatifu aidha anafaikiriU ekumene kutoka kwa matumbo kama ufafanuzi unaoweza kuashiria mtindo wa kuelewa udugu wa kibinadamu uliounganishwa kwa sura na mfano wa Mungu ambaye kutoka moyoni mwake alitupenda sisi sote, chini ya uongozi wa Roho wake, kwa mwili wa Mungu. Mwana na, kwa jinsi baba anavyowapenda watoto wake, “kutoka matumbo. Kitabu hiki kinaelezea bandari tofauti za safari yake kwa mwelekeo wa Uekumene ambao unatafuta kuzunguka bahari ya wazi ya wanadamu wote, shida zake za kweli, wasiwasi wake na utafiti wake wa juu zaidi. Uekumene ambao Figueroa anasisitiza kuunganishwa katika uumbaji na ulimwengu kama sehemu ya mfumo ikolojia unaopatana, uliounganishwa na unaotegemeana. Hili lipo sana sana katika Nyaraka zake za Laudato si ' na Fratelli tutti, zote za kiekumene! Kazi hii pia inaleta ladha nzuri ya mtu aliyeelimishwa katika Ufalme wa Mbinguni ambaye anajua jinsi ya kupata hazina katika mambo mapya na ya kale (rej. Mt 13:52).
Papa amebainisha alivyomfahamu kuhani wa kipresibitiani Marcelo Figueroa kwa zaidi ya miaka ishirini. “Mimi ni shuhuda wa jitihada zake muhimu kwa mazungumzo ya kweli na mkutano wa kiekumene, ambao tulishiriki urafiki wa kindugu wenye kuimarisha sana na hata kipindi cha televisheni huko Buenos Aires, Biblia, mazungumzo yanayotumika, pamoja na Mkuu wa Kiyahudi Abraham Skorka”. Haipaswi kupuuzwa kwamba msomi huyu wa Kibiblia wa Kiprotestanti anapendekeza katika kitabu hiki uteuzi wa makala mia moja zilizochapishwa katika Osservatore Romano katika miaka sita iliyopita. Inanijaza furaha kwamba ukweli huu wa kihistoria na uwazi halisi wa kiekumene wa gazeti la Vatican umekuja na upapa wangu! Kila mara huwa nasoma kwa makini makala za Marcelo na nitaendelea kuzisoma kwa sababu zinanisaidia kuangalia njia ya kiekumene niliyoipitia na ile ambayo bado inapasa kufanyika, kwa macho ya ndugu anayejaribu kusoma tena na kufasiri upapa wangu kwa mtazamo wa kiekumene. Nimefurahishwa na maono ambayo kaka yangu anayatoa ya uekumene na napenda kukumbuka kwamba ni dhana iliyojikita katika misingi ya Upapa wangu, kwani ni njia ya kujaribu kuwa Kanisa moja lililoanzishwa katika Kristo Bwana na, kuanzia kutoka hapa, kwa kila usemi wa Imani; kama safari tunayofanya pamoja katika sala, katika matendo ya upendo na katika ushuhuda, chini ya mtazamo wa Mungu.
Baba Mtaakatifu Francisko aidha anauchukulia mwelekeo huu wa kila siku wa uekumene kuwa kama sehemu kuu ya Majisterio ya Kipapa, yaani (mafundisho) inayofuata njia iliyofunguliwa na Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kuanzia ushuhuda wa kitume wa Kibiblia na ambao ulitajirishwa sana na watangulizi wake kwa msukumo wao uliotolewa kwa mazungumzo na kujitolea kwa kiekumene. Papa anatumia fursa hiyo kupendekeza kwa shauku na kusindikiza na kitabu hicho cha “Tofauti zailizo patanishwa”. Mprotestanti katika gazeti la Papa, kumtumia baraka. “Bwana wa upatanisho wa aina mbalimbali amtumie kuangazia macho ya shauku, kupanua upeo wa kiroho zaidi ya kuwa wa imani na kukumbatia mioyo isiyotulia, kuelekea kwa Mungu aliye pamoja na kila mtu na zaidi ya yote katika nyumba moja ya pamoja!
Hata hivyo katika Kitabu hicho kitawakilishwa mjini Roma siku ya Jumanne tarehe 15 saa 9.00 alasiri katika Ukumbi wa Marconi kwenye Jumba Pio, na Marco Impagliazzo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Lorenzo Fazzini, mhusika mhariri wa Lev. Andrea Monda, Mkurugenzi wa Osservatore Romano, na atakayefunga mkutano na mratibu ni Silvina Pérez, mhusika wa Gazeti la kila juma la Kihispanaia. Tumiko litaendeshwa mwa mtindo wa waina mbili moja kwa moja na kwenye mtandao kupitia: www.vaticanews.va.