Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekuwa mtu wa mazungumzo kati ya watu Baba Mtakatifu Francisko amekuwa mtu wa mazungumzo kati ya watu 

Miaka 9 ya Upapa wa Francisko katika njia ya uinjilishaji wa mazungumzo

Katika kumbukizi la miaka tisa ya upapa wa Fransisko limejikuta katika saa ya giza katika historia,inayotazama mzozo nchini Ukraine.Lakini kuanzia tarehe 13 Machi 2013 hadi leo,Jorge Mario Bergoglio amekuwa akifanya kazi daima kwa ajili ya amani na upatanisho kati ya watu,na kuleta matumaini ya Injili katika kila pembezoni mwa dunia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vita ni wazimu ambavyo vimeanza kati ya Urusi na Ukraine mnamo tarehe 24 Machi 2022 kwa kuengezea huzuni katika siku ambayo  inajikita kutimiza mwaka wa 9, tangu Papa Francisko achaguliwa kuwa kiongozi Kharifa wa Mtume Petro  mnamo tarehe 13 Machi 2013.  “La guerra è una pazzia”, yaani vita ni wazimu alirudia mara nyingi Papa akiomba kusitisha umwagaji wa mito ya damu na machozi, akiomba kufungua njia za kibidamu ili kuwasaidia watu. Lakini katika wazimu huo wa vita, Papa Francisko aliwawaalika kujibu kwa njia ya  upendo wa kiinjili ambao unajaza moyo na maisha kamili kwa yule anayekutana na Yesu.

Papa Francisko anatimiza miaka 9 ya Upapa
Papa Francisko anatimiza miaka 9 ya Upapa

Miito ya amani

Kwa kupitia katika mchakato wa miaka inayokaribia kumi ya Upapa wa Bergoglio, yote yanaoneshwa wazi. Mnamo 2021 ulifunguliwa na kufugwa kwa kuomba amani hasa shukrani kwa ziara mbili za kitume: moja mwezi Machi huko  Iraq (quello in Iraq)  ma mwezi Desemba huko Cyprus na Ugiriki (quello a Cipro e in Grecia). Safari zote mbili, Papa Fracisko aliwaalika kupambana dhidi ya vurugu na kurudi katika kisima cha ubinadamu na udugu. Ni maneno ambayo aliweza kurudia mwezi Septemba huko Budapest na Slovakia (a Budapest e in Slovacchia), mahali ambapo Papa alilaani kila aina ya uharibifu wa hadhi ya binadamu.

Janga na wito wa kidugu

Mwaka 2021 umeunganishwa na mwaka 2020 wa janga la Uviko- 19. Papa Franncisko ameshauri mara nyingi (esorta costantemente)  kutoa ruhusu ya Hati miliki kwa ajili ya utengenezaji wa chanjo zaidi na kuwaalika ulimwengu kujikabidhi kwa Bwana.  “Kukumbatia msalaba wake  alisisitiza hayo katika njia ya msalaba  “Statio Orbis” ya tarehe  27 Machi  2020 kwamba  kuna maana ya kuruhusu aina za udugu”.  Na ndiyo kweli udugu unasikika katika Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu ukiwa ni Waraka wa Tatu wa Kipapa uliotiwa saini tarehe 3 Oktoba 2020 huko Assisi mji wa Mtakatfiu maskini Francis. Katika barua hiyo anabainisha juu ya urafiki wa kijamii na kukataa vita.

Nyanyaso za kijinsia

Hata kwa mwaka 2019 unasikika mwangwi wa maneno ya udugu katika Hati juu ya Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya Amani ulimwenguni na kuishi pamoja (“Fratellanza Umana per la Pace Mondiale e la convivenza comune”, iliyotiwa saini huko Abu Dhabi kati ya  Papa na  Imam  kuu wa Al-Azhar Ahamad al-Tayyib. Hati hiyo kwa hakika inashutumu vurugu na ugaidi na kuwakilisha hatua msingi katika mahusiano kati ya ukristo na Uislamu. Hata hivyo katika mwaka huo 2019 kuna hata mapambano dhidi ya nyanyaso, ambalo mwezi Februari, ulifanyika mkutano kuhusu ulinizi wa watoto ulio waona hata maarais wa Mabaraza ya maakofu na  ambao uliona uandishi wa Barua binafsi ya Motu proprio Vos estis lux mundi,  ambamo wanaelezea mchakato tisa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa maaskofu na wakuu wa mashirika wanaelewa vzuri shughuli yao, iwe ya kuondoa siri ya kipapa all’abolizione del segreto pontificio  katika kesi za manyanyaso ya kijinsia. Mnamo tarehe 20 Agosti 2018 zaidi ya hayo Papa Francisko aliandika barua kwa Watu wa Mungu (Lettera al popolo di Dio), mahali ambapo alikuwa anabainisha njia ya ukweli, haki, kuzuia na kutibu manyanyaso ya kijinsia na kusisitiza ukaribu wa Kanisa kwa Waathirika.

Maskini, huruma na utunzaji wa Mazingira

Kwa hakika mnamo 2017 kinyume chake iliona hatua ya neno la maskini kwa kujikita na Siku ya I ya Maskini Ulimwenguni. Siku hiyo ilitolewa na Papa kwa barua yake ya kitume ya huruma na amani (Lettera apostolica Misericordia et misera)  ambayo ilikuwa inahitimisha Jibilei maalum ya Huruma iliyoanza mnamo 2016 kwa njia ya  kwa ufunguzi wa Mlango Mtakatifu  kila Kanisa la Ulimwengu. Na wakati huyo Yeye alifungua Mlango akiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ulinzi wa Kazi ya uumbaji ni mada iliyokuwa ya mwaka 2015 kwa kuangaziwa na Waraka wa laudato Si, kuhusu Utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja (Laudato si’ sulla cura della casa comune) na kuanzishwa kwa siku ya Kuombea kazi ya Uumbaji(Giornata mondiale di preghiera per la cura del Creato). Matukio yote mawili yalikuwa ni kutoa msisitizo wa ulazima wa kuhamasisha Ikolojia fungamani ambaye iweze kuweka pamoja utunzaji kwa mazingira na usawa kwa maskini.

Papa Francisko anatimiza miaka 9 ya Upapa
Papa Francisko anatimiza miaka 9 ya Upapa

Kati ya mwaka 2015 na 2014 mtazamo wa Baba Mtakatifu ulikuwa wa familia ambapo Baba Mtakatifu alijikita na Sinodi mbili, mmoja maalum na nyingine ya kawaidia, ambamo kulikuwa na wasiwasi wa Papa kwa mashambulizi dhidi ya familia katika jamii mamboleo ambayo daima inazidi kumezwa na ubinafsi. Kama dawa dhidi ya tabia hiyo, ulitolewa Wosia wa kitume kuhusu Furaha ya Upendo ndani ya familia wa (Amoris Laetitia) wa 2016, ambapo Papa aliweza kuhimiza uzuri wa familia unaojikita juu ndoa isiyotengenishwa kati ya mume na mke. Umuhimu huo ulisisitizwa sana baadaye katika Mwaka Maalum wa Familia Amoris Laetitia ambao utahitimishwa mwaka huu mwezi Juni 2022 mjini Roma katika Mkutano wa X wa dunia wa Familia  (il decimo Incontro mondiale delle Famiglie).

Mambo mengine mapya

Mwaka 2013 ulikuwa mwaka wa mambo mapya, kwa mfano kwamba Kardinali Bergoglio kuchagua jina la Francisko, kwa sababu kabla yake hapatokea Papa hata mmoja aliyekuwa amechagua jina hili na kama ilivyokuwa kwamba hapakuwahi kuwapo Papa hata mmoja kutoka katika Shirika la Yesu (Jesuit) na wala mwenye asili ya Amerika Kusini, na wala katika kipindi cha kisasa, kuchanguliwa mara baada ya mtangulizi wake kung’atuka madarakani. Yote hayo yalikuwa ni mambo mapya ya mwaka huo wa kuchaguliwa kwa Upapa wake. Ushirikishaji ndiyo muhuri na mtindo wa Bergoglio katika utawala katika Kanisa la Ulimwengu. Kwa hilo mnamo 2013 , Papa alianzisha Baraza la Makardinali Washauri  “Consiglio di Cardinali” wakiwa na jukumu la kumsaidia katika shughuli na utendaji wake hasa katika mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Kitume ya “Pastor bonus” yaani “Mchungaji mwema” kuhusu Cuaria Romana, iliyotiwa saini mnamo 1988 na  Papa  Wojtyła yaani Mtakatifu Yohane Paulo II.  Muswada wa Katiba Mpya ya Kitume ulipewa jina la muda : “(Praedicate evangelium, yaani “Tangazeni Injili” ambao hasa sasa huko katika mchakato wa maandalizi.

Mageuzi ya Kanisa

Papa kwa sasa anatazama sana juu ya mageuzi ya Kanisa, kwani katika Wosia wa Kitume wa Evangelii gaudium yaani ‘Furaha ya Injili’ wa 2013,  Papa Francesco anatumaini upyaisho wa miundo ya kikanisa kwa maana ya kimisionari, hata katika muktadha wa kiuchumi. Inatosha kutaja tu Barua binafsi ya Motu proprio “Kuhusu uwezo fulani katika masuala ya kiuchumi na kifedha” (“Circa alcune competenze in materia economico-finanziaria”),  ambapo usimamizi wa fedha na mali za Sekretarieti ya Nchi zilihamishiwa kwa APSA na jukumu la usimamizi la Sekretarieti ya Uchumi kuimarishwa. Pia hata mapambano dhidi ya rushwa (la lotta alla corruzione) kwa ajili ya kuweza uwazi katika usimamizi wa fedha za umma. Katika mkutadha wa kichungaji, baadaye Papa aliongeza nguvu za majukumu ya walei na wanawake katika maisha ya Kikanisa. Mnamo 2018, Dk.  Paolo Ruffini alikuwa Mlei wa kwanza kuteuliwa kuwa Mwwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano, wakati mnamo 2021 , Sr  Nathalie Becquart akateuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu, na kwa barua yake Binafsi ya  Motu proprio Baba Mtakatifu Francisko Spiritus Domini yaani “Roho wa Bwana”: Utume wa Waamini Walei kutoka katika Ubatizo”, na  Antiquum Ministerium, ) yaani “Huduma ya kale” alifanya marekebisha ya utoaji huduma kwa walei  kwa kupewa daraja la usomaji na utumishi Altareni akiweka hata ile ya Makatekista. Zaidi ya hayo kuna hata katiba ya kitume ya Pascite gregem Dei, ambayo  inasasisha sekta ya haki ya hukumu katika Kanisa.

Wahamiaji na utamaduni wa kukutana

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuwa makini sana kwa wahamiaji ambapo alionesha hili katika ziara yake tangu  alipokwenda Lampedusa (viaggio a Lampedusa)  mnamo 2013 na ziara mbili kwa Kisiwa cha Lesvos mnamo  (nel 2016 na nel 2021; ikiwa ni pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kukutana ambao ameweka nuru kwa mfano mnamo mwaka 2014 katika jitihada akiwa mstari wa mbele Papa alijikita kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba (l’allacciamento delle relazioni diplomatiche tra gli Stati Uniti e Cuba). Hata sasa, katika nyakati hizi ngumu za vita nchini Ukraine, Papa hachoki kabisa, (il Papa non si è risparmiato) kufanya  juhudi zozote zile  katika kushughulikia makabiliano ya amani kati ya pande hizo mbili, binafsi amekwenda katika ubalozi wa Urusi uliopo Vatican na kumwita hata  Rais wa Ukraine Zelenskyi.

MIAKA 9 YA UPAPA WA BABA MTAKATIFU FRANCISKO
12 March 2022, 17:50