Tafuta

2022.03.26 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Binti wa Maria Mtakatifu wa Bustani. 2022.03.26 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Binti wa Maria Mtakatifu wa Bustani. 

Papa kwa watawa:shuhudieni Mungu kwa walio maskini!

Papa Francisko akikutana na Watawa wa Shirika la Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani,amewashauri kupokee mbegu za ufalme wa Mungu zilizopo katika uhalisia,kwa kusimama na kutunza maskini,kusikiliza sana ili kuponya sintofahamu,upweke na kuweza kurudisha hadhi ya binadamu.Onyo wajizuie masengenyo ambayo uharibu utambulisho.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 26 Machi 2022 amekutana na Wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani katika fursa ya Mkutano Mkuu wa XX, ulioanza tarehe 18 Machi 2022 katika kesha la Mtakatifu Yosefu. Papa amesema sehemu hiyo kwa kila familia ya kitawa inawakilisha kipindi muhimu katika safari yao ya maisha, maana ya mkutano, mazungumzo, jukumu na muungano wa kiinjili. Ni imani ya Papa kwamba wamependelea kujikabidhi kwa Mtakatifu Yosefu kazi yao na ufanisi mzuri: Yeye ni fundi Seremala wa Nazareth ambaye kwa kazi yake alishiriki katika ishara ya wokovu na kuhudumia kwa imani, kama mwanaume aliyekuwa na haki. Mtindo huo wa Mtakatifu Yosefu, unapatikana hata kwa Mwanzilishi wa Shirika Mtakatifu Antonia Maria Gianelli ambaye pia alikuwa Mtume wa Injili ya Kazi msingi wa maisha ya mtu, familia na kijamii. Papa ameongeza kusema kuwa wengine walimwita “Mtakatifu wa chuma” lakini alikuwa wa kibinadamu. Chuma ni jinsi ya kuelezea utakatifu, lakini pia hata mtu mnyoofu na haitakiwi kukosea kwa tabia kama hiyo” na alikuwa na mfano mzuri.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani

Yeye alikuwa mfanyakazi bora katika uwanja wa Bwana na kujikita katika huduma ya Neno la Mungu, kwa kuhubiri na kwa kazi. Katika mahubiri alishuhudia na kutangaza imani ya Mungu mpaji. Katika huruma alionesh njia ya utakatifu na kuvutia kupitia, kwa kutoa mfano wa upendo wa dhati na huruma kwa walio wa mwisho na wa pembezoni mwa jamii. Kwa lengo hilo ndipo alianzisha mnamo 1829 akiwa paroko huko Chiavari huduma ya upendo na kuwakabidhi wanawake aliwaita “Mama wa Upendo ambapo lilianzia Shirika lao linalojuliakana Gianelline. Shirika hili kwa muda mfupi lilitawanyika sehemu mbali mbali za ulimwengu na walitafuta kutimiza wito walioupokea kwa kutimiza utume wa uinjilishi na kazi ya upendo.  Mada waliyochangia kuongoza mkutano huo mkuu ni “Umakini katika ulimwengu kwa moyo wa Mungu, na ambayo wamejaribu kutafsiri vizuri kama shirika la kutunzana na kufanya kutunza jirani, kutenda wema kwa kukita mizizi katika maisha ya wakfu kwa Bwana. Huu ni umakini wa kukaa na Mungu lakini pia kwenda pembezoni kwa wanaohitaji. Pale ni kushuhudia Mungu.

Hakika wamejiuliza wajibuje changamoto za sasa za utamaduni ambao hauko hivi, ni utamaduni wa kujitosheleza, ni utamaduni, unaweza kusema kidogo “makeup”, ambapo hakuna kukua, kuliko kwenda mbele; utamaduni wa kioo, wa kujirejea binafsi. Na hii ni mbaya. Utamaduni, huu wa kujirejea, ambao ni wa kiburi kidogo, kwenye kutojali, wengine, kutazama upande mwingine, kwa ubinafsi, na hii inasumbua mpangilio wa uhusiano wa kibinadamu na inafungua njia nyingi za mkato za utumwa wa dhuluma, unyonyaji, unaodhalilisha utu wa watu. Kwa maana hiyo wao wanafanya kazi maishani, kwa utambuzi kuwa leo hii kuna unyonyaji kiasi gani katika tamaduni huu dhidi ya vijana, watoto hata ajira za watoto, wanawake walionyonywa, hata wazee: njia moja ya kuwanyonya ni kuwaacha kandoni. Na dhidi ya utamaduni huu kuna taasisi yao ambayo kwa upendo inaweza kwenda mahali popote. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha walivyo katika nchi mbali bali na wanakutana na hali nyingi za mateso, za umaskini, na ugumu…

Hata utume wao wa kiinjili Papa amesema unakutana na vizingiti na lakini kwa mfano wa Mtakatifu Antonio Ganelli, badala ya kukata tamaa, wanakabiliana kwa imani na tumaini matatizo haya kwa kutambua kwamba wao ndiyo maskini wa kwanza na wanye kuhitaji Mungu. Tabia hii ya kinyenyekevu na kijasiri inafanana na ile ya Bikira Maria mbele ya majaribu yake. Hayo yanawafanya kila mmoja wao kuwa ardhi nzuri mahali ambapo inawezekana kuota mbegu ya upendo, ambayo wao wanaalikwa kuimwagilia kila siku kwa sala, hasa kwa kuabudu, na kubaki na moyo wa Mungu kama inavyosema kauli mbiu yao. Kutoka katika moyo wa uliokita ndani ya Mungu ndipo matumaini ya maisha ambayo yanatoa manukato ya Injili, yenye utajiri wa kuelewa kindugu, wa huruma, furaha na kujitoa binafsi. Ulimwengu una kiu ya maisha mema, lakini yenyewe haiwezi kuitoa, kwa sabababu inahitaji kuona ushuhuda na si watu mashuhuri, lakini watu rahisi, wenye vikwazo na wadhaifu lakini pamoja na hayo walio jaa nguvu ya Roho Mtakatifu. Kwa mizizi hiyo na uthabiti wa kina, Baba Mtakatifu amethibitisha kwamba wanaweza kwenda njia za ulimwengu na wanaweza kufanya kama walivyopendekeza kuwa makini katika ulimwengu. Baba Mtakatifu Franciski akifafanua nini maana hiyo amewashauri mifano miwili ya kutafakari na kutembea nayo.  Awali ya yote ni kuwa makini uliomwenguni kwa maana ya kiinjili yaani anayejua kushangaza anayejua kujifungilia wazi ili kupokea mbegu za Ufalme wa Mungu uliopo katika hali halisi, kwa sababu anatambua kuwa Roho Mtakatifu daima anafanya kazi na anafanya kwa huru na kwa namna ambayo mara nyingi analeta mshangao. Umakini kwa maana hiyo sio kama angalisho au kuhukumu, sio kama shuku au kutoamini au hofu, lakini anajua ukweli, urahisi, anajua kuchukulia hali halisi na watu namna jinsi walivyo.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Maria Mtakatifu wa Bustani

Ushauri wa pili ni ule ambao unasisitiza umakini wa ulimwengu kwa yule ambaye habaki katika balaza hachungulii kutoka mbali, lakini anakaribia na kuinama, anagusa kwa mkono. Hiyo ni moja ya mambo ambayo ni mabaya; mkristo wa kukaa katika ubalaza. Papa ametumia mfano kuwa kwa Kihispania anayeitwa balconea, ni mtazamo wa kuangalia mambo kwa mbali tu ambapo yeye hana mawasiliano na ulimwengu. Hivyo amewaomba wasikae kwenye balcony, wasitazame kwa umbali na vizuizi badala yake wakaribie, wainame, waguswe kwa mikono yao. Tendo la kugusa kwa mkono litufanye kuwa binadamu. Kawaida, katika kuungamisha au katika mazungumzo, Papa Francisko amebainisha anavyopenda kuuliza maswali mtu, iwapo anapaokuwa anatoa sadaka,  kwa maskini anamapatia akiwa anamgusa kwa mkono na  kutazama uso  kwa uso?  Na kama hafanyi hivyo basi sadaka hiyo ni ya kinadharia, sio sadaka kwani ukiwa na uwezo wa kugusa, kutazama machoni, ndiyo mambo mazuri. Hiyo ni muhimu na kwa maana hiyo amesisitiza kuwa ni lazima kutoka katika  balcony, kwenda kugusa kwa mkono na kutazama uso wa mtu huyo.

Umakini kwa maana hiyo ni ukaribu wa kujifanya jirani, na kutunza. Baba Mtakatifu amewapongeza jinsi walivyo na shule ya mwanzilishi alivyo wakabidhi kuwa wasamaria wema, daimwa wanaosafiri lakini wako tayari kusimama na kutunza maskini, waliojeruhiwa maisha, kufunga majeraha na kusikiliza sana, ili kuweza kuponya sintofahamu, upweke na kurudisha hadhi. Na hili ni kuanzia na familia binafsi yaani Jumuiya zao, Papa amekazia. Swali la Papa “Ninawezaje kuwa makini ulimwenguni, ikiwa sina uwezo wa kuwa makini kwa aliye karibu ya chumba changu, ninayefanya kazi pamoja? Roho Mtakatifu, kwa maombezi ya Bikira Maria aweze kusaidia ili Jumuiya yao iweze kuendelea kwa hali tulivu ya udugu, joto la ukaribu, uwelewa na wema. Hata kati yao amebainisha katika nyumba zao kuna majeraha, kuna upekwe, kuna ugumu wa kiafya na kiakili.

Papa Francisko kutoa onyo amerudia kusema: “Adui wa udugu huo ni masengenyo. Najua hamjui, ninyi nyote ni watakatifu… Lakini ni rahisi sana kuingia kwenye masengenyo! “Kwa mfano “Umeona kile ambacho huyo alisema?”.  Na kwa hivyo mazungumzo huanza ... Na maskini huzikwa na maneno yetu. Kwa hilo, niwatawapatia zawadi. Ni utafiti mdogo wa Balozi wa Kitume alifanya juu ya masengenyo. Papa ameomba kusoma kwani kitawasaidia. Gumzo huharibu utambulisho. Amehitimisha kwa kuwashukuru tena kwa kuwa katikati ya Watu wa Mungu na ukaribu na maskini. Matatizo na shida visiwaogopeshe na waendelee mbele kwa imani kwa Mungu na daima wawe waaminifu kwa karama yao asili. Imani ya ubunifu, inayoongozwa na mang’amuzi ya uvumilivu, hekima, ujasiri, na kuangazwa daima na Neno la Mungu, mafundisho ya Kanisa na ushauri wa kiroho kwa wataalam na wenye ujuzi. Amewabariki kwa moyo. Waendele mbele kwa furaha, kuwa makini kwa ulimwengu kwa moyo wa Mungu. Wasisahau kusali daima kwa ajili yake.

HOTUBA YA PAPA KWA SHIRIKA LA BINTI WA MARIA MTAKATIFU WA BUSTANI
28 Machi 2022, 09:35