Tafuta

Papa Francisko:imani inarithishwa na wazee kwa vijana

Katika mwendelezo Katekesi ya Papa Francisko kuhusu mada ya Uzee,kwa kupendekezwa na mfano wa Musa,akiwa katika siku zake za mwisho,anataja jina la Bwana na kurithishwa kwa vizazi vipya urithi wa historia aliyofanya uzoefu na Mungu.Papa ameshauri wazee waweze kusimulia historia zao kwa watoto na vijana kwani imani ya wazee ni katekisimu tosha kwa maisha ya kizazi cha vijana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 23 Machi 2022, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, kwa waamini na mahujaji waliofika, ameendeleza Katekesi yake kuhusu mada ya Uzee ambapo ameongozwa na Wimbo wa Musa. Akianza katekesi hyo Papa Francisko amesema: “ Katika biblia, simulizi ya kifo cha mzee Musa inatanguliwa wasifu wake  wa  kiroho, unaoitwa "Canticle of Moses", 'wimbo wa Musa'. Wimbo huu unahusu ungamo zuri la imani, na unasema hivi: "Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.” (Kumb 32:3-4). Lakini pia ni kumbukumbu ya historia aliyoishi na Mungu, ya matukio  ya watu ambao waliundwa kuanzia na imani katika Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Na kwa hiyo Musa pia anakumbuka uchungu na masikitiko ya Mungu mwenyewe: uaminifu wake daima kujaribiwa na ukosefu wa imani kwa  watu wake. Mungu mwaminifu na mwitikio wa watu wasio waaminifu: kana kwamba watu wanataka kujaribu uaminifu wa Mungu. Na yeye daima hudumu katika uaminifu, karibu na watu wake. Hiki ndicho kiini cha wimbo wa Musa: uaminifu wa Mungu ambao unatusindikiza katika maisha yetu yote.

Katekesi ya Papa 22 Machi 2022
Katekesi ya Papa 22 Machi 2022

Musa anapofanya ungamo hili la imani yuko kwenye kizingiti cha nchi ya ahadi na pia kukaribia kuaga maisha. Alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini, historia inasema, lakini macho yake hayakuzimika (Kumb 34,7). Uwezo huo wa kuona, yaani kuona pia kwa njia ya mfano, kama wazee wanavyoona, ambao wanajua jinsi ya kuona vitu, ya maana msingi zaidi ya vitu. Uhai wa macho yake ni zawadi ya thamani ambayo inamruhusu kurithisha urithi wa uzoefu wake wa muda mrefu wa maisha na imani, kwa uwazi muhimu. Musa anaona historia na kurithisha historia hiyo; wazee wanaona historia na kupitisha historia hiyo, Papa amesisitisha. Uzee ambao unapewa fursa ya ufahamu huu unato ni zawadi ya thamani kwa kizazi kijacho. Usikilizaji kibinafsi na wa moja kwa moja wa historia  ya imani iliyo hai, pamoja na misukosuko yake yote, hauwezi kubadilishwa. Kuisoma katika vitabu, kuiangalia kwenye sinema, kushauriana kwenye mtandao, hata hivyo ni muhimu, japokuwa haiweze kuwa sawa. Urithishwaji huo ambao ni utamaduni halisi, urithishwaji wa dhati kutoka kwa wazee hadi kwa vijana!  Hata hivyo Papa amebainisha kwamba urithishwaji  huu leo huu unakosekana sana kwa vizazi vipya. Je ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu ustaarabu huu mpya una wazo kwamba ya zamani ni taka, ya zamani lazima itupwe. Huu ni ukatili!  Na kumbe sivyo ilivyo.

Historia za moja kwa moja kutoka kwa mtu hadi mtu, una sauti na njia za mawasiliano ambazo hakuna njia nyingine zinaweza kuchukua nafasi hiyo. Mzee ambaye ameishi kwa muda mrefu, na anapata zawadi ya ushuhuda wa wazi na wa shauku wa historia yake, ni baraka isiyoweza kubadilishwa. Je, tuna uwezo wa kutambua na kuheshimu zawadi hii ya wazee?  Je, urithishwaji wa imani na wa maana ya maisha, unafuata njia hii ya kuwasikiliza wazee leo hii? Ni swali la Papa na ambaye amethibitisha kwamba “ Ninaweza kutoa ushuhuda wa kibinafsi. Nilijifunza kuchukia na hasira ya vita kutoka kwa babu yangu ambaye alikuwa amepambana kwenye vita ya mnamo mwaka wa 1914: Yeye aliniambukiza kuchukia vita hiyo. Kwa sababu aliniambia juu ya mateso ya vita. Na hii hujifunzi kutoka katika vitabu au kwa njia nyingine yoyote, unajifunza kwa njia hii, kurithishwa kutoka kwa babu hadi kwa wajukuu. Na hii haiwezi kubadilishwa yaani ya uenezaji wa uzoefu wa maisha kutoka kwa babu hadi kwa wajukuu. Leo hii kwa bahati mbaya sio hivyo na inadhaniwa kuwa babu ni nyenzo za kupoteza: na kumbe  hapana,  kwa sababu wao ni kumbukumbu hai ya watu na vijana na watoto lazima wasikilize babu na bibi zao.

Katekesi ya Papa 22 Machi 2022
Katekesi ya Papa 22 Machi 2022

Katika utamaduni wetu, ambavyo tunaweza kusema sahihi kisiasa, njia hii inaonekana kuzuiwa kwa njia nyingi kwa mfano katika familia, katika jamii, katika jumuiya ya Kikristo yenyewe. Hii ni kutokana na kwamba inafikia mtu hata anapendekeza kukomesha mafundisho ya historia, kama habari isiyo ya kawaida juu ya walimwengu ambao sio wa sasa, ambayo inachukua rasilimali kutoka kwa maarifa ya wakati wa sasa. Ni kana kwamba tulizaliwa jana! Urithishwaji wa imani, kwa upande mwingine, mara nyingi unakosa shauku ya “historia ya kuishi”. Kurithisha imani sio kusema maneno “blah-blah-blah”. Inamaanisha uzoefu wa imani. Na kwa maana hiyo inawezekana ngumu kuvutia watu kuchagua upendo milele, uaminifu kwa neno lililotolewa, uvumilivu katika kujitolea, kuwa na huruma kwa nyuso zilizojeruhiwa na zilizovunjika? Kwa hakika, historia za maisha lazima zigeuzwe kuwa ushuhuda, na ushuhuda lazima uwe mwaminifu. Itikadi inayopindisha historia kwa mifumo yake kwa hakika si ya haki; propaganda, ambayo inabadilisha historia kwa kuhamasisha kikundi cha mtu, sio haki; si haki kuweka historia katika mahakama ambayo yote yaliyopita yanahukumiwa na kila siku zijazo kukatishwa tamaa. Kusema haki ni kusimulia historia jinsi ilivyo, na ni wale tu ambao wamefanya uzoefu  wanaweza kusimulia vizuri. Ndiyo maana ni muhimu sana kusikiliza watu wazee, kusikiliza babu na bibi, na ni muhimu kwa watoto kuzungumza nao.

Injili zenyewe kwa uaminifu zinasimulia historia iliyobarikiwa ya Yesu bila kuficha makosa, kutoelewana na hata usaliti wa wanafunzi. Hii ni historia, huu ni ukweli, huu ni ushuhuda. Hii ni zawadi ya kumbukumbu ambayo wazee wa Kanisa urithisha tangu mwanzo kabisa, kwa kurithisha kutoka mkono hadi mkono kwa kizazi kinachofuata.  Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameomba kujiuliza maswali “ je, tunathamini kiasi gani njia hii ya kueneza imani, katika kupitisha ushuhuda kati ya wazee wa jumuiya na vijana wanaojifunguulia uwazi wa siku zijazo?  Papa amekumbuka jambo ambalo amelsema mara nyingi sana lakini akapenda kurudia tena. Je Imani inapitishwaje? Kwa kutoa mfano Papa amesema: “Ah, hapa kuna kitabu, jifunze”: hapana! Imani hawezi kurithishwa hivyo. Imani inapitishwa kwa njia ya kilugha, yaani, katika usemi unaofahamika, kati ya babu na bibi na wajukuu, kati ya wazazi na wajukuu. Imani daima urithishwa katika lugha ya kuzaliwa, ambayo kwa hakika inafahamika na ya uzoefu wa kujifunza kwa miaka mingi. Hii ndiyo sababu mazungumzo katika familia ni muhimu sana, mazungumzo ya watoto na babu na bibi ambao ni wenye hekima ya imani."

Katekesi ya Papa 22 Machi 2022
Katekesi ya Papa 22 Machi 2022

Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kwamba wakati mwingine yeye hutokea kutafakari juu ya hali hii isiyo ya kawaida. Katekisimu ya Kuanzishwa Ukristo inachota  kwa ukarimu  leo hii  Neno la Mungu na kusambaza habari sahihi juu ya mafundisho ya kweli, juu ya maadili ya imani na sakramenti. Hata hivyo, mara nyingi kuna ukosefu wa maarifa ya Kanisa unaotokana na kusikiliza na kushuhudia historia halisi ya imani na maisha ya jumuiya ya kikanisa, tangu mwanzo hadi kufikia nyakati zetu.  Kwa watoto tangu mwanzo hujifunza Neno la Mungu katika madarasa ya katekisimu; lakini Kanisa linajifunza kama vijana, katika madarasa na katika vyombo vya habari vya kimataifa. Masimulizi ya historia ya imani inapaswa kuwa kama  Wimbo wa Musa kama ushuhuda wa Injili na Matendo ya Mitume. Hiyo ni historia yenye uwezo wa kuibua baraka za Mungu kwa hisia na mapungufu yetu kwa uaminifu. Ingekuwa vizuri kama kungekuwa tangu mwanzo, katika ratiba za katekesi au katekisimu, pia tabia ya kusikiliza, kutokana na uzoefu wa maisha ya wazee, ungamo la wazi la baraka zilizopokelewa kutoka kwa Mungu, ambazo ni lazima tuzitunze, na ushuhuda wa uaminifu, kushindwa kwetu, ambako ni lazima kufanya toba na kurekebisha.

Katekesi ya Papa 22 Machi 2022
Katekesi ya Papa 22 Machi 2022

Wazee wanaingia katika nchi ya ahadi, ambayo Mungu anatamani kwa kila kizazi, wanapowapa vijana mwanzo mzuri wa ushuhuda wao na kusambaza historia ya imani, imani katika kilugha, yaani kliugha kinachojulikana na ambacho urithishwa kutoka kwa wazee hadi kwa vijana. Baadaye wakiongozwa na Bwana Yesu, wazee na vijana huingia pamoja katika Ufalme wake wa uhai na upendo. Lakini wote kwa pamoja. Kila mtu katika familia, na hazina hii kubwa ambayo ni imani inayorithishwa kwa njia ya  kilugha!

KATEKESI YA PAPA 23 MACHI 2022 KUHUSU WAZEE KURITHISHA IMANI KWA KIZAZI
23 March 2022, 11:29