Tafuta

2022.03.21 Papa amekutana na Wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu". 2022.03.21 Papa amekutana na Wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu". 

Papa Francisko:Kwani nini vita badala ya suluhisho la mazungumzo

Ni kiasi gani kinachotumika kununua silaha:haisemekani!Sijui ni asilimia ngapi ya Pato la Taifa,sijui,sipati takwimu halisi,lakini asilimia ni kubwa.Na inatumika kununua silaha za kufanya vita sio hiyo tu,ambayo ni mbaya sana na ambayo tunapitia sasa na tunahisi zaidi kwa sababu iko karibu,lakini katika Afrika,Mashariki ya Kati na huko Asia vita vinaendelea.Amesema hayo Papa wakati wa Kukutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea”Nilikuwa na kiu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 21 Machi 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea liitwalo: “Nilikuwa na kiu” ambapo ameanza kwa kushukuru Rais kwa maneno yake na furaha ya kuwapokea wakiwa wanafanya kumbukizi ya miaka kumi tangu kuanza uzoefu wao wa kujitolea. Tangu mwanzo walianza kuunganika  kwa lengo wazi  na la dharura hasa  la kupeleka maji safi kwa yule hasiye kuwa nayo. Na maneno ya Yesu: “Nilikuwa na Kiu” (Mt 25, 23)  Papa Francisko amesema ndiyo yamekuwa jina na kauli mbiu yao, kwa maana hiyo anawapongeza.  Kupatika kwa maji kwa namna ya pekee maji safi na salama imekuwa ni changamoto kubwa la wakati huu na wakati ujao wa familia ya kibinadamu (taz. Laudato 27-31). Ni suala la kutoa kipaumbele cha maisha ya sayari na kwa ajili ya amani kati ya watu. Ni suala linalowatazama watu wote, amesisitiza Papa. Japokuwa  amesisitiza katika ulimwengu hasa barani Afrika, kuna watu ambao zaidi ya wengine wanateseka sana na ukosefu wa wema msingi huo. Kwa maana hiyo wametimiza mpango wao wa kibinadamu barani Afrika katika nchi na kanda tofauti za bara. Hiyo ni nzuri. Kama vile hata jambo zuri sana ambalo kazi inafanywa na wa watu mahalia na kwa ushirikiano na wamisionari na jumuiya za kikanisa mahalia, amesema.

Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"
Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"

“Nilikuwa na kiu mkanipa maji ya kunywa, anasema Yesu na kuongeza: “Yote mliyowatendeammoja wa wale ndugu zangu walio wadogo zaidi, mlinitenda mimi” (Mt 25,35.40). Baba Mtakatifu Francisko amesema, kiu haifanya kuugua ikiwa kuna wingi wa maji ya kunywa. Lakini tunatambua kuwa na kiu yanapokosa na kukosa kwa muda mrefu, kiu inaweza kuvumiliwa. Maisha katika dunia, yanategemea maji; hata sisi kama binadamu. Ili kuweza kuishi wote tunahitaji dada maji! Baba Mtakatifu ameuliza swali kama ndiyo hivyo je ni kwa nini kufanya vita kwa migogoro ambayo tunapaswa kusuluhisha kwa kuzungumza kama watu? Kwa nini tusiungane pamoja na nguvu zetu na rasilimali zetu ili kupambana pamoja kwa ajili ya kuwa na mapambano ya kistaharabu, kama vile mapambano dhidi ya njaa na dhidi ya kiu; mapambano dhidi ya maradhi na majanga, badala yake kufanya sehemu kubwa ya manunuzi ya silaha, ambazo zinawakosesha hata kile wanachosa cha lazima.

Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"
Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"

Papa Francisko ameongeza kusema “Na hii ni kashfa: matumizi ya silaha. Ni kiasi gani kinachotumika kununua silaha: haisemekani! Sijui ni asilimia ngapi ya Pato la Taifa, sijui, sipati takwimu halisi, lakini asilimia ni kubwa. Na inatumika kununua silaha za kufanya vita na hivyo sio hiyo tu, ambayo ni mbaya sana na ambayo tunapitia sasa, na tunahisi zaidi kwa sababu iko karibu, lakini katika Afrika, Mashariki ya Kati, na huko Asia  vita, vinaendelea ... Hii ni mbaya”, Papa amesisitiza. “Ni mbaya. Kujenga dhamiri kwamba matumizi ya silaha, na kununua silaha, na ambazo huchafua nafsi, huchafua moyo, huchafua ubinadamu”. Papa Francisko ameuliza tena: “Je inasaidia nini juhudi za wote pamoja, kwa kwa dhati, katika ngazi ya kimataifa, katika kampeni dhidi ya umaskini, dhidi ya njaa, dhidi ya uharibifu wa sayari, ikiwa basi tutarudi kwenye enzi za zamani za vita, katika mkakati wa zamani wa nguvu ya silaha, ambayo inarudisha kila kitu na kurudi nyuma? Vita daima inakurudisha nyuma na kila wakati.  Ni kutembea kurudi nyuma na kulazimika kuanza kwa wakati mpya”, Papa Francisko amebainisha.

Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"
Papa amekutana na wajumbe wa Shirika la Kujitolea "Ho avuto sete" yaani "Nilikuwa na kiu"

Baba Mtakatifu amesema kwamba kama wanavyoweza kuona, shirika lao   kwa hakika ni dogo likilinganishwa na matatizo haya makubwa, hata hivyo, limefanya kazi kwa hatua muhimu na linafanya vizuri, na kwa njia sahihi; kama mashirika mengine mengi ya kujitolea yanavyofanya, nchini Italia na Ulimwenguni kote na kwa maana hiyo ameshukuru Mungu.  Baba Mtakatifu merudia kusema kwamba yeye alipata mshangao mkubwa kukuta nchini Italia juhudi na nguvu ya watu wa kujitolea kwa sababu hajawahi kuona sehemu nyingine zaidi namna hiyo.  Huo ni urithi wao wa kiutamaduni, wa Kiitaliano, ambao lazima uulindwe vizuri.  Wao wanajitolea vizuri. Kwa hilo amewashuru tena na kuwatia moyo wa kuendelea mbele katika jitihada zao. Amewabariki kwa moyo wote na wale ambao katika sehemu mbali mbali za mipango yao wanafanya kazi pamoja. Ameowamba zawadi moja ya kumwombea na kuwabariki.

HOTUBA YA PAPA KWA WAJUMBE WA SHIRIKA LA KUJITOLEA "NILIKUWA NA KIU"
21 March 2022, 16:29