Nia za sala ya Papa kwa mwezi Februari 2022:Utafiti wa kimatibabu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ujumbe kwa njia ya video wa Papa Francisko kwa mwezi Machi 2022 wa nia ya sala ambayo anaikabidhi kwa Kanisa Katoliki lote ulimwenguni, kupitia Mtandao wa Maombi wa Kimataifa wa Papa, umejikita katika changamoto mpya ambazo maadili ya kibiolojia inaleta katika ulimwengu mamboleo kwa kutoa mwaliko wa kuhakikisha kuwa inapaswa kukabiliwa pamoja siku zote na kuhamasisha ulinzi wa maisha kwa sala na matendo ya kijamii. Ujumbe huu kwa njia ya video umetengenezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Kipapa ya Maisha.
Viinitete vya binadamu si nyenzo 'zinazoweza kutupwa'
Baba Mtakatifu Francisko anatualika kusali ili tuweze kutoa jibu la Kikristo katika changamoto za maadili ya kibiolojia. “Ni wazi sayansi imeendelea na leo bioteknolojia inatuletea mfululizo wa matatizo ambayo lazima tuyajibu: hatuwezi kuficha vichwa vyetu kwenye mchanga kama mbuni. Matumizi ya kibayoteknolojia lazima kila mara yatumike kuanzia kwa heshima ya hadhi ya binadamu. Kwa mfano, viinitete vya binadamu haviwezi kushughulikiwa kuwa ni vitu vya kutupwa, na pia vinaingia katika utamaduni huu wa kutupa: hapana, hiyo haiwezekani! kwa kueneza utamaduni huu ambao hufanya uharibifu mkubwa! amesisitiza Papa.
Hadhi na maendeleo ya binadamu yanaenda pamoja
Ufafanuzi wa Papa Francisko uko wazi kwa maana amesema: “Hatuwezi kuruhusu faida ya kiuchumi kuweka hali ya utafiti wa matibabu”. Kwa maana hiyo mtazamo wake uko ndani ya mabadiliko lakini umakini wake umewekwa juu ya umuhimu wa utambuzi wa ndani zaidi, hata zaidi wa hila. “Si suala la kurudisha nyuma maendeleo ya kiteknolojia. Hapana, hili ni si suala la kusindikiza. Linahusu kulinda hadhi na maendeleo ya binadamu. Kwa maneno mengine, hatuwezi kulipagharama ya maendeleo kwa hadhi ya mwanadamu, la hasa! Papa amesisitiza. "Mambo hayo mawili huenda pamoja, kwa upatano pamoja. Kwa kukabiliwa na changamoto mpya zinazoletwa na kanuni za maadili, na hivyo tuombe kwamba Wakristo, kupitia maombi yao na matendo yao ya kijamii, waendeleze ulinzi wa maisha".
Maendeleo ya kiteknolojia sio adui
Papa Francisko kwa hiyo haoni maendeleo ya kiteknolojia kama adui, zaidi ya yote anatusihi tusiipinge kwa gharama yoyote ile au kujaribu kuizuia. Kwa mujibu wake Baba Mtakatifu, anabainisha kwamba maendeleo hayafanyiki kwa urahisi, kwa kujifanya kuwa hakuna kilichotokea. Jukumu la hatua za kijamii hazipaswi kupuuzwa. Wakristo, kwa hakika, wana jukumu la kushiriki katika mjadala wa hadhara kwa kutoa sauti zao: kwa lugha inayofaa na hoja zinazoeleweka katika muktadha wa sasa wa kijamii, kama Baba Mtakatifu alivyokumbusha hivi karibuni kwa Taasisi ya Kipapa ya Maisha lakini bila kupuuza yaliyomo na daima kuthibitisha hitaji la maendeleo fungamani ya binadamu.