Tafuta

Mwanzo wa Mafungo ya Kiroho Binafsi ya Papa Francisko na Curia ya Kirumi 6-11 Machi 2022 Mwanzo wa Mafungo ya Kiroho Binafsi ya Papa Francisko na Curia ya Kirumi 6-11 Machi 2022 

Mafungo ya Kiroho,Papa Francisko anaombea mahitaji ya Kanisa na ya wanadamu

Papa Francisko ameomba waamini kuwasindikizwa katika Juma la mafungo ya kiroho ya Kwaresima ambayo kuanzia tarehe 6 - 11 Machi 2022.Huu ni mwaka wa pili mfululizo, kutokana na dharura ya UVIKO-19 kutofanyika huko Ariccia katika nyumba ya mafungo pamoja na Curia ya Kirumi lakini kila mtu atafanya kwa njia yake binafsi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko anawaomba waamini kuwasindikiza katika juma la mafungo ya Kwaresima, kuanzia leo hadi tarehe 11 Machi 2022.  

Papa amesema:  “Mchana wa leo, pamoja na washiriki wa Curia ya Kirumi, tutaanza Mafungo ya Kiroho. Tunabeba maombi yetu kwa ajili ya mahitaji yote ya Kanisa na ya familia ya kibinadamu. Na ninyi pia, tafadhali, mtuombee”.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, amebainisha kuwa katika siku hizi, mipango yote ya Papa itasitishwa, ikijumuisha na Katekesi ya siku ya Jumatano tarehe 9 Machi. Ni mwaka wa pili mfululizo,  katika janga  la UVIKO ambalo limeweka masharti kiasi kwamba Papa anakosa kwenda mafungo ya kiutamaduni ili kuishi kijumuiya katika mafungo ya kiroho na Curia Romana katika nyumba ya mafungo ya kiroho ya ‘Divin Maestro’ huko Ariccia, nje kidogo ya Roma.

Kama mwaka jana kwa maana hiyo, Papa Francisko amewaalika makardinali wanaoishi Roma, wakuu wa mashirika na wakuu wa Mabaraza ya Kipapa kujitoa wenyewe, katika kufanya mafungo binafsi kwa sala kuanzia tarehe 6 hadi Ijuma tarehe 11 Machi 2022.

06 March 2022, 15:10