Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kardinali Antonios Naguib, Patriaki wa Kanisa la Kikoptic, la Alexandria lililoko nchini Misri. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kardinali Antonios Naguib, Patriaki wa Kanisa la Kikoptic, la Alexandria lililoko nchini Misri. 

Kardinali Antonios Naguib Mfano Bora Wa Kuigwa: 1935-2022. RIP

Hayati Kardinali Antonios Naguib alizaliwa tarehe 18 Machi 1935 huko Samalout. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 30 Oktoba 1960. Tarehe 26 Julai 1977 akateuliwa kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 9 Septemba 1977 kwa ajili ya Jimbo la Minya. Tarehe 30 Machi 2006 akateuliwa kuwa Patriaki wa Kanisa la Kikoptic la Alexandria. Ukardinali ni Tarehe 20 Novemba 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na kifo cha Kardinali la Alexandria Antonios Naguib, Patriaki wa Kanisa la Kikoptic, la Alexandria nchini Misri kilichotokea tarehe 28 Machi 2022 akiwa na umri wa miaka 87. Baba Mtakatifu katika salam za rambirambi alizomtumia Patriaki Ibrahim Isaac Sedrack wa Kanisa la Kikoptic la Alexandria anamwomba amfikishie salam zake za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito. Anapenda kuwahakikishia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake katika kipindi hiki kigumu kilicholikumba Kanisa la Kikoptic nchini Misri. Baba Mtakatifu anamkumbuka sana Hayati Kardinali Antonios Naguib, ambaye katika maisha na utume wake aliongozwa na kauli mbiu “Veritas Caritas” yaani “Ukweli katika upendo. Kwa hakika alikuwa ni mtu wa imani thabiti, ari na mwamko wa pekee kwa Mapadre wake kiasi kwamba, akajitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya majiundo awali na endelevu ya Mapadre wake, kama kipaumbele chake cha pekee. Alikuwa ni kiongozi aliyejisadaka kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, kiasi cha kuanzisha Kikundi cha Huduma ya Upendo kwa ajili ya maskini na wale wote waliokuwa wanateseka: kiroho na kimwili. Kwa hakika alikuwa ni mfano bora wa Mchungaji mwema.

Hayati Kardinali Antonios Naguib alikuwa ni mgfano bot wa kazi za kichungaji.
Hayati Kardinali Antonios Naguib alikuwa ni mgfano bot wa kazi za kichungaji.

Hata katika Kanisa la Kiulimwengu alitekeleza dhamana yake bila wasi wasi kwani wakati wa Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofi Mashariki ya Kati, alipewa dhamana ya kuwa ni Mwezeshaji mkuu. Baba Mtakatifu anapenda kuchukua nafasi hii, kumkumbuka na kumwombea Hayati Kardinali Antonios Naguib, ili kwa maombezi ya Bikira Maria, aweze kupokewa Yerusalemu ya mbinguni na Jeshi la Malaika na Watakatifu wote wa Mungu. Itakumbukwa kwamba, Hayati Kardinali Antonios Naguib, Patriaki wa Kanisa la Kikoptic, la Alexandria nchini Misri alizaliwa tarehe 18 Machi 1935 huko Samalout. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 30 Oktoba 1960. Tarehe 26 Julai 1977 akateuliwa kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 9 Septemba 1977 kwa ajili ya Jimbo la Minya. Tarehe 29 Septemba 2002 akang’atuka kutoka madarakani. Tarehe 30 Machi 2006 akateuliwa kuwa Patriaki wa Kanisa la Kikoptic la Alexandria, nchini Misri. Tarehe 20 Novemba 2010 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedkto XVI akamteuwa na kumsimika kuwa Kardinali.

Tarehe 15 Januari 2013 akang’atuka kutoka madarakani. Na ilipogota tarehe 28 Machi 2022 akafariki dunia akiwa na umri wa miaka 87. Katika umri huu, amelitumia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 61. Kama Askofu akiwa na dhamana ya kuwaongoza, kuwafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa miak 44 na kama Kardinali kwa miaka 11. Takwimu zinaonesha kwamba, kwa kifo cha Kardinali Antonios Naguib, Patriaki wa Kanisa la Kikoptic, la Alexandria nchini Misri, kwa sasa Baraza la Makardinali linaundwa na Makardinali 211 kati yao 119 wakiwa na haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Waliobaki 92 hawana tena haki ya kupiga wala kupigiwa kura wakati wa uchaguzi.

Tanzia

 

 

29 March 2022, 15:49