Tafuta

Baba Mtakatifu anawaalika Maaskofu, Mapadre na waamini walei kuungana pamoja naye kwa sala Ijumaa tarehe 25 Machi 2022. Baba Mtakatifu anawaalika Maaskofu, Mapadre na waamini walei kuungana pamoja naye kwa sala Ijumaa tarehe 25 Machi 2022. 

Barua ya Papa Francisko Kwa Maaskofu Wote: Wakfu Urussi na Ukraine Kwa B. Maria

Kwa kuitikia kilio cha watu wa Mungu, Baba Mtakatifu anasema, anapenda kuziweka wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria, Urussi na Ukraine ambazo kwa sasa ziko katika vita kali. Ibada hii itafanyika tarehe 25 Machi 2022 Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu. Ni Siku ya kuombea amani inayobubujika kutoka katika toba, wongofu na msamaha.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake kwa Maaskofu Katoliki Duniani kote iliyochapishwa Jumatano tarehe 23 Machi 2022 anaelezea kuhusu mwaliko kwake kwa Maaskofu kujiunga pamoja naye kwa ajili ya kusali na kuombea amani duniani sanjari na kuziweka wakfu Urussi na Ukraine kwa Moyo Safi wa Bikira Maria, Anasema, takribani mwezi mmoja umegota tangu vita kati ya Urussi na Ukraine vilipofumuka, kiasi cha kutishia amani, ustawi na maendeleo ya Jumuiya ya Kimataifa. Mama Kanisa katika nyakati hizi za giza, anasukumwa kumwendea Mfalme wa Amani sanjari na kujenga udugu na ujirani mwema na wale wote wanaoendelea kuathirika kutokana na vita hii. Baba Mtakatifu anawashukuru na kuwapongeza wale wote wanaojisadaka kwa njia ya kufunga, kusali na matendo ya huruma kwa ajili ya wakimbizi wa kivita.

Tarehe 25 Machi 2022: Siku ya Kuombea Amani Duniani.
Tarehe 25 Machi 2022: Siku ya Kuombea Amani Duniani.

Kwa kuitikia kilio cha watu wa Mungu, Baba Mtakatifu anasema, anapenda kuziweka wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria, Urussi na Ukraine ambazo kwa sasa ziko katika vita kali. Ibada hii itafanyika tarehe 25 Machi 2022 Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu. Ni Siku ya kuombea amani inayobubujika kutoka katika toba, wongofu wa ndani na msamaha. Ibada hii ya kuwekwa wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria litaadhimishwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuanzia Saa 11: 00 kamili jioni kwa Saa za Ulaya sawa na Saa 1: 00 Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati. Ibada ya Wakfu inatarajiwa kuanza Saa 12:30 Jioni sawa na Saa 2: 30 za Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki. Hili ni tukio linalopaswa kuonesha ushiriki wa Kanisa la Kiulimwengu, katika kipindi hiki kigumu, linataka kukiweka mbele ya Mwenyezi Mungu kwa njia ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa.

Kilio cha watu wa Mungu ili vita ikome nchini Ukraine.
Kilio cha watu wa Mungu ili vita ikome nchini Ukraine.

Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kanisa linataka kumpelekea Mwenyezi Mungu kilio cha watu wote wanaoteseka kutokana na vita, ili hatimaye, aweze kukomesha vita. Kanisa linapenda kumkabidhi Bikira Maria Malkia wa Amani, matarajio ya amani ya binadamu. Kumbe, Ijumaa tarehe 25 Machi 2022 Baba Mtakatifu Francisko anawaalika Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waamini Walei, kusali kwa pamoja kama Jumuiya katika maeneo ya Ibada, ili kweli sala ya watoto wa Mungu iweze kupaa na kumfikia Mwenyezi Mungu kwa njia ya Bikira Maria. Baba Mtakatifu anapenda pia kuwapatia nakala ya Sala iliyotafsiriwa kwa lugha mbalimbali ili waamini waweze kuisali Siku ya Ijumaa tarehe 25 Machi 2022.

Barua Maaskofu

 

23 March 2022, 12:02