Papa aomba kuendeleza kwa ajili ya Ukraine na mazungumzo ya kidiplomasia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Jumatano tarehe 9 Februari 2022, mara baada ya katekesi yake kwa waamini n wamhujaji waliofika katika ukumbi wa Paulo VI amependa kuwashukuru watu na jumuiya zote ambazo tarehe 26 Januari iliyopita waliungana kwa pamoja katika sala kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ya Ukraine. Papa amemewaomba kundelea kuomba Mungu wa amani ili mivutano na hatari za vita viweze kushindwa kwa njia ya mazungumzo ya kweli na ili kwa lengo hilo liweze kuchangia hata mazungumzo mengine ya muundo wa Normandy. Papa ameongeza kusema wasisahau kuwa "vita ni uwendawazimu".
Viongozi wa Urusi na Ufaransa kukutana
Hata hivyo nguvu za kidiplomasia zinahitajika kwa sababu vivutano kati ya Urusi na Ukraine imekuwapo kwa miaka mingi sasa. Hivi karibuni nchini Urusi ilianza kutuma wanajeshi wake na vifa karibu na mipaka ya Ukraine, kwa kupanua kile kiitwacho nguvu za uvamizi. Na katika matukio ya hivi karibuni, juhudi za kidiplomasia zimekuwa zikishika kasi katika jitihada za kutuliza hali hiyo. Kufuatia mazungumzo na Rais Vladimir Putin, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumanne 8 Februari kwamba anaamini hatua zinaweza kuchukuliwa kupunguza mzozo huo na kutoa wito kwa pande zote kuwa watulivu. Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy walikuwa wamesema wamejitolea kwa kanuni za makubaliano ya amani ya 2014, wakiongeza kuwa mpango huu, unaojulikana kama makubaliano ya Minsk, ambao ulitoa njia ya kusuluhisha mizozo yao inayoendelea.
Macron na Kansela wa Ujerumani
Wakikutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz baadaye mjini Berlin, Macron na kansela walisema, kwamba Lengo lao la pamoja ni kuzuia vita barani Ulaya. Macron na Scholz pia walikutana mjini Berlin na Rais wa Poland Andrzej Duda. Ofisi ya rais wa Ufaransa ilisema baada ya mazungumzo hayo kuwa viongozi hao watatu walionesha uungaji mkono wao wa pamoja kwa ajili ya uhuru wa Ukraine.
Marekani na UE kutaka kuweka vikwazo kwa Urusi
Marekani na Umoja wa Ulaya zimeitishia Urusi kuwekea vikwazo iwapo itaishambulia Ukraine. Hata hivyo, Moscow kwa kiasi kikubwa imepuuza vikwazo vipya kama tishio tupu. Rais wa Marekani Joe Biden alionya Jumatatu iliyopita kwamba ikiwa Urusi itaivamia Ukraini, “hakutakuwa tena Nord Stream 2” akimaanisha bomba jipya la gesi lililojengwa, ambalo bado halijafunguliwa hadi Ujerumani.