Papa Francisko:watoto askari wanapaza kilio kwa mungu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Janga, uhalifu wa kuchukiza. Kwa miaka mingi, Papa Francisko amekuwa akitoa sauti yake kila mara kuhusu balaa la watoto askari hivyo kujifanya kuwa mtafsiri wa uchungu wa watoto wengi, walioraruliwa kutoka katika utoto wao na kulazimishwa kuchukua silaha mikononi na kuwa vyombo vya kifo. Katika ujumbe wake mfupi kwenye mtandao @Pontifex, uliochapishwa tarehe 12 Februari 2022 katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga matumizi ya watoto kama askari katika nchi zenye vita, Papa Francisko ameandika kwamba “watoto maakari wameibiwa utoto wao, wasio na hatia, wakati wao ujao, na mara nyingi maisha yenyewe. Kila mmoja wao kilio kinapaa kwa Mungu na ambaye pia anawalaumu watu wazima wanaowaweka bunduki kwenye mikono ya walio wadogo.
Ni watoto wengi walio ajiliwa
Watoto wameajiriwa kama wapiganaji lakini pia wapishi, wapagazi, walinzi, wajumbe wa kutumwa. Wasichana wanaojihusisha na shughuli mbalimbali kama vile usafiri, usaidizi wa matibabu, kupika, kusafisha na kutunza watoto wengine lakini ambao wanaweza kushiriki kikamilifu katika nigogoro hiyo, kama vile Afrika ambapo karibu asilimia 40% ya wasichana waliandikishwa na jeshi na makundi ya silaha, vikundi vinavyo shiriki moja kwa moja katika uhasama au katika Mashariki ya Kati ambapo kuna vitengo vya wanawake tu vya matumizi ya silaha za kimbinu.
Mnamo 2020 watoto zaidi ya 8,500
Walakini, wote wawili ni waathirika wa utekaji nyara, vitisho, na ulaghai. Wengine wanasukumwa na umaskini, wakilazimika kutafuta mapato kwa ajili ya familia zao. Bado wengine huunganisha nguvu ili kuishi au kulinda jamii zao. Bila kujali kuhusika kwao, kuandikishwa na kutumiwa kwwa watoto na vikosi vya kijeshi, Shirika la la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linasisitiza kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto na sheria za kimataifa za kibinadamu. Katika kuadhimisha Siku hiyo, Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba mwaka wa 2020 kuna zaidi ya wanajeshi 8,500 walioandikishwa na kuajiriwa katika maeneo ya vita, ikiwa ni ongezeko zadi ikilinganishwa na kesi 7,750 zilizorekodiwa mwaka wa 2019.
Takriban asilimia 75 ya migogoro inahusisha kuajiriwa kwa watoto
Zaidi ya watoto 93,000 kati ya 2005 na 2020, miaka miwili tu iliyopita. Umoja wa Mataifa ulithibitisha ukiukwaji mkubwa 26,425. Takriban asilimia 75 ya migogoro inahusisha kuajiriwa kwa watoto na zaidi ya nusu ya migogoro hiyo ni pamoja na wasichana. Wanachoteseka watoto ni aina nyingi za unyonyaji na unyanyasaji ambao pia huwa ni ngono kwa wasichana. Ndoa za utotoni ni chombo kingine kinachopendelewa na baadhi ya pande zinazopigana, kwa sababu wasichana wanalazimishwa kuolewa na wapiganaji wa kiume na kuishi chini ya udhibiti wao, mara nyingi hufanyiwa ukatili wa kijinsia kila siku.
Kupinga Matumizi ya Watoto katika nchi zenye vita ilitangazwa 12 Februari 2002
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Watoto katika nchi zenye vita ilitangazwa tarehe 12 Februari 2002, tarehe ambayo Itifaki ya Hiari ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto, ambayo inakataza kuhusika kwa watoto katika migogoro ya silaha, ilianza kutumika.”Ingawa watoto hawana jukumu kubwa katika vita, mamilioni miongoni mwao wanajikuta katikati ya machafuko ambayo sio watazamaji bali walengwa”, ulimsea wakati wa kuzindua muongozo wa kuwalinda watoto katika hali za vita. Laura Battaglia ni mwandishi wa habari, mtengenezaji wa filamu fuip, mwandishi wa ripoti nyingi nchini Yemen, na akizungumza amekumbusha Vatican News kwamba kuna nchi ambapo utoto si utoto na ambapo watoto, wanapozaliwa, tayari ni watu wazima. Ni muktadha mgumu sana kuelewa na kubadilika kwa sababu watoto wadogo wameajiriwa kila mara katika baadhi ya kazi, wasichana kuolewa mapema sana au wanaume kutumiwa kwa njia mbalimbali na Wanamgambo au katika majeshi. Usikivu unahitajika, anasema mwandishi wa habari, lakini pia huruma inayotokana na kugusa kidonda hiki moja kwa moja.