Papa Francisko:Turuhusu Yesu apande mtumbwi wetu wa maisha
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Injili ya liturujia ya siku inatupeleka juu ya fukwe za Galilaya. Umati wa watu wanamzunguka Yesu wakati baadhi ya wavuvi wakiwa wamekata tamaa na miongoni mwao ni Simoni Petro ambaye anasafisha nyavu zake baada ya usiku wa uvuvi kwenda vibaya. Na tanatazama Yesu anapanda juu ya mtumbwi wa Simon na anamwalika kutweka kilindini tena (Lk 5,1-4). Ni maneno ya Papa Francisko wakati wa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwa kuongozwa na Injili, Dominika tarehe 6 Februari 2022 kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Pretro. Kwa mana hiyo Papa Francisko amependa kutafakari hatua mbili za Yesu, ya kwanza ni kupanda juu ya mtumbwi na pili kuwaalika watupe nyavu zao kilindini. Ulikuwa usiku uliokwenda vibaya bila kupata samaki lakini Petro anaamini na kutweka kilindini. Awali ya yote anapanda juu ya mtumbwi wa Simoni. Je kufanya nini. Kwa ajili ya kufundisha. Anapanda katika mtumbwi huo ambao haujajaa samaki kwa sababu umerudishwa ukiwa mtupu na ni usuku wa nyavu tupu mara baada ya usiku mzima wa kazi na kukata tamaa. Ni picha nzuri sana kwetu sisi Papa Francisko amesema.
Tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu
Kila siku mtumbwi wa maisha yetu utuacha katika fukwe za nyumba ili kujikita ndani ya bahari ya sughuli za kila siku; kila siku tunajikuta tunavua samaki, tunakuza ndoto na kupeleka mbele mipango, kulisha upendo katika mahusiano yetu. Lakini mara nyingi kama Petro, tunaishia kuvua usiku na nyavu zilizo tupu, kukata tamaa baada ya jitihada sana na kuona hakuna matokeo mazuri: tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu.(Lk 5,5). Ni mara ngapi hata sisi tunakuwa hivyo na maana hii ya kushindwa, wakati ndani ya moyo kunazaliwa kukata tamaa na uchungu! Minyoo miwili hatari sana! Papa amesisitiza.
Mtumbwi unageuka kuwa kiti cha Yesu, cha kutangazia neno lake
Bwana anafanya nini? Anachagua kiukweli kupanda katika mtumbwi wetu, kutoka hapo anataka kutangaza Injili Ulimwenguni. Ni pale penye mtumbwi mtupu, ishara ya ukosefu wa uwezo wetu, unageuka kuwa kiti cha Yesu, ambacho kinakuwa cha kutangazia Neno. Bwana anapenda kufanya hivyo. Bwana ni Bwana wa mshangao, wa miujiza katika mshangao; wa kupanda juu ya mtumbwi wa maisha yetu, ikiwa hatuna lolote la kumpatia; anaingia katika tupu zetu na kuzijaza na uwepo wake; anasaidiwa na umaskini wetu ili kutangaza utajiri wake, kwa ufukara wetu ili kutangaza utajiri wake.
Unatosha mtumbwi maskini mtupu tu ili kumkaribisha Bwana
Lazima kukumbuka hilo ya kwamba Mungu hataki Meli kubwa ya kitalii, kwani unatosha mtumbwi maskini tu ulio mtupu ili tumkaribishe. Hiyo hasa ya kumkaribisha. “Hana haja ya mtumbwi huo; tumkaribishwe. Lakini je sisi tunamwacha apande katika mtumbwi wa maisha yetu? Tunamwachia awe na uwezekano wa kile hata kidogo tulicho nacho? Papa ameuliza maswali hayo. Kwa kuongezea amesema: “Mara nyingi tunahisi tusiostahili kwake Yeye kwa sababu sisi ni wadhambi, lakini hiyo ni sababu ambayo Bwana hapendi, kwa sababu inamweka mbali nasi! Yeye ni Mungu wa ukaribu, ambaye hatafuti ukamilifu, lakini anayekaribisha. Hata kwako wewe leo hii anasema: “Ninaomba nipande juu ya mtumbwi wa maisha yako jinsi yalivyo”, Papa ameshauri.
Si kusimama juu ya mifumo ya kiuvuvi, bali juu ya mapya ya Yesu
Kwa njia hiyo Bwana anarudisha kwa upya imani ya Petro. Hata alipokwisha kunena, alisema “Tweka mpaka kilindini” (Lk 5,4). Mshangao ni kile kilichomsukuma kufanya kama Yesu alivyokuwa akimwagiza. Hayakuwa ni masaa yanayofaa kuvua samaki lakini Petro akaamini Yesu. Si kubaki kusimama juu ya mifumo ya kiuvuvi, ambayo ilikuwa inajulikana, lakini ni juu ya mapya ya Yesu. Ndiyo ilivyo hata kwetu sisi. Ikiwa tutamkaribisha Bwana, katika mtumbwi wetu, tunaweza kutweka hadi kilindini. Kwa kuwa na Yesu, inawezekana kupiga kasia katika bahari ya maisha bila woga, bila kuangaika na kukata tamaa hasa wakati hakuna samaki wa kuvua na bila kujiachia kusombwa na kile kisemwacho “hakuna lolote la kufanya”.
Yeye anafungua uwezekano mpya
Katika maisha binafsi daima kama yale ya Kanisa na ya kijamii, kuna jambo zuri na ujasiri ambao unaweza kufanyika. Daima inawezekana kuanza tena na daima Bwana anatualika kuthubutu kwa sababu ni Yeye anafungua uwezekano mpya. Kwa maana hiyo tupokee mwaliko na kutupilia mbali ugumu na ukosefu wa imani kwa kuanza kutweka kilindini na Yesu. Hata mtumbwi wetu mdogo na mtupu unaona uvuvi wa miujiza. Kwa kuhitimisha Papa amewaalika waamini kusali kwa Maria, kwa maana hakuna yeyote aliyepokea Bwana juu ya mtumbwi wa Maisha na ili yeye atutie ujasiri na kutuombea sisi.