2022.02.27 Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro katika sala ya malaika wa Bwana 2022.02.27 Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro katika sala ya malaika wa Bwana 

Papa Francisko:silaha zisimame,anayefanya vita amesahau ubinadamu!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa ametoa wito kwa ajili ya Ukraine:“watu wa kawaida wanataka amani lakini wanalipa gharama katika ngozi yao kutokana na weu wa vita.Mikondo ya kibidanamu inahitajika kwa wanaotafuta kukimbia.Papa amekumbuka hata migogoro ya Sria,Ethiopia na Yemen:"Mungu yuko pamoja na wapatanishi wa amani,si pamoja na wale wanaotumia vurugu”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na wahujai waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican, Dominika tarehe 27 Februari 2022 Papa Francisko ametoa wito kwa mara nyingine tena kwa ajili ya Ukraine kwamba: “Katika siku za hivi karibuni tumeshtushwa na jambo la kutisha: vita. Na mara kadhaa tumeomba kwamba njia hii isichukuliwe. Na hatuachi kuomba, kinyume chake, tunazidi kumwomba Mungu kwa bidii zaidi. Kwa sababu hiyo, ninarudia kutoa mwaliko wangu kwa wote, tarehe 2 Machi ambayo ni Jumatano ya Majivu, iwe  siku ya maombi na kufunga kwa ajili ya amani katika nchi ya Ukraine. Siku moja ya kuwa karibu na mateso ya watu wa Ukraine, kuhisi ndugu wote na kumsihi Mungu akomeshe vita”.

Papa atoa wito tena wa kuombea amani nchini Ukraine
Papa atoa wito tena wa kuombea amani nchini Ukraine

Papa Francisko akiendelea amesisitiza kwamba:  “Yule anayefanya vita, yule anayechochea vita, anasahau ubinadamu. Haviaanzii kutoka kwa watu, haviangalii maisha halisi ya watu, lakini anayeweka mbele ya kila kitu masilahi na madaraka. Anajikabidhi katika mantiki ya kishetani na potovu ya silaha, ambaye yuko  mbali zaidi na mapenzi ya Mungu. Na anajiweka mbali na watu wa kawaida, wanaotaka amani; na katika kila mzozo ndiyo wathirika wa kweli, yaani ambae hulipa makosa ya vita kwenye ngozi yao wenyewe. Papa ameongeza kusema: “ Ninawafikiria wazee, wale wanaotafuta kimbilio katika saa hizi, akina mama wanaokimbia na watoto wao… Wao ni kaka na dada ambao ni  kuna uharaka wa kuwafungulia mikondo ya kibinadamu na ambao lazima wapokelewe”.

Wanajeshi huko Ukraine
Wanajeshi huko Ukraine

Papa Francisko kutokana na hiyo amesema kwamba “Kwa moyo uliovunjika kwa kile kinachotokea Ukraine na tusisahau vita katika sehemu nyingine za ulimwengu, kama vile Yemen, Siria, Ethiopia…, ninarudia: zikomeshwe silaha zao! Mungu anasimama pamoja na wapatanishi, si pamoja na wale wanaotumia nguvu. Kwa sababu wale wanaopenda amani, kama Katiba ya Italia inavyosema: “hukataa vita kama chombo cha kukera uhuru wa watu wengine na kama njia ya kusuluhisha mizozo ya kimataifa” (Ibara ya 11).

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amekumbusha jinsi ambavyo Jumamosi tarehe 26 Februari, huko Granada, Hispania, Padre Gaetano Giménez Martín na wafia dini wenzake kumi na watano, waliouawa kutokana na chuki ya imani yao katika mazingira ya mateso ya kidini ya miaka ya 1930 nchini Uhispania, walitangazwa kuwa wenyeheri. Kwa maana hiyo “Ushuhuda wa wanafunzi hawa mashujaa wa Kristo uamshe shauku yote ya kuitumikia Injili kwa uaminifu na ujasiri. Kwa shangwe tuwapigie makofi wenyeheri wapya…

Kanisa Kuu la Granada nchini Hispania
Kanisa Kuu la Granada nchini Hispania

Hatimaye Baba Mtakatifu amewasalimia waamini wa Mungu kutoka Italia na mahujaji kutoka las niñas Quinceñeras wa Panamá; vijana wanafunzia wa chuo kikuu kutoka Jimbo la Porto; waamini wa Merida-Badajoz na Madrid, Hispania; wa Paris na Poland; vikundi vya Reggio Calabria, Sicilia na Na kikundi cha Umoja wa Kichungaji wa Alta Langa; Wanakipaimara kutoka Urgnano na vijana kutoka Petosino, jimbo la Bergamo, Italia.

Siku ya Maadhimisho ya Magonjwa adimu 28 Februari
Siku ya Maadhimisho ya Magonjwa adimu 28 Februari

Salamu za Papa pia  maalum kwa wote waliofika kwenye tukio la Siku ya Magonjwa Adimu, ambayo itaadhimishwa Jumatatu tarehe 28 Februari. Kwa wao wote amesema “Ninawatia moyo vyama mbalimbali vya wagonjwa na familia zao, pamoja na watafiti wanaofanya kazi katika uwanja huu. Niko karibu nanyi! Aidha amewasalimu watu wote waliokuwa hapo maana aliota hata bendera nyingi za Ukraine! (kwa Kiukreni) Tumsifu Yesu Kristo! Na kuwatakia wote Mlo mwema na siku njema, wasisahau kusali kwa ajili yake.

WITO WA PAPA KWA UKRAINE
27 February 2022, 15:40