Papa Francisko:Mwombee adui na usiye mpenda!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akianza tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 20 Februari 2022 kwa mahujaji na waamini waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican amesema: “Injili ya liturujia ya siku, Yesu anawapa wafuasi wake baadhi ya maelekezo msingi ya maisha. Bwana anagusia hali ngumu zaidi zile ambazo zinajiwakilisha kama benki ya majaribu, yale ambayo yanatuweka mbele ya yule adui na mgumu, yule ambaye anatafuta kutufanyia mabaya. Katika kesi kama hizi wafuasi wa Yesu wanaalikwa wasiangukie katika hisia za mwanzo na chuki, wasiamini, lakini kwa ajili ya kwenda mbele zaidi na zaidi ya hisia za haraka za chuki. Baba Mtakatifu amesema, Yesu anasema hivi: “pendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wanawachukia” (Lk 6,27). Na bado anaongeza “anayekupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie la pili (6,29). Sisi tunapohisi hili, utafikiri kwamba Bwana anatuomba kisichowezekana. Isitoshe, kwa nini uwapende maadui? Ikiwa hutaguswa na wanyanyasaji, kila unyanyasaji unapewa njia huru na hii sio haki. Lakini ni kweli hivyo? Je, kweli Bwana anatuomba mambo ambayo hayawezekani na kwa hakika yasiyo ya haki? Ndio hivyo? Papa anauliza maswali.
Tufikirie awali ya yote maana ya ukosefu haki ambao tunahisi katika kugeuza shavu jingine? Na tufikirie Yesu. Wakati wa mateso, katika mchakato wake usio na haki mbele ya kuhani Mkuu, wakati huo alipigwa kofi na mmoja kati ya walinzi. Je yeye alifanyaje? Hakumtukana, hapana! Alimwambia mlinzi huyo: “ikiwa nimezungumza vibaya, nioneshe ubaya wangu. Lakini ikiwa nimezungumza vema, kwa nini kunipiga?” (Yh 18,23). Papa ameongeza kusema , Yesu anaomba kupokea kwa kadiri ya ubaya wake. Kugeuza shavu jingine, haina maana ya kuteseka kwa ukimya, kukubali ukosefu wa haki. Kwa sababu awali ya yote Yesu anasema kile ambacho si haki. Lakini anafanya hivyo bila hasira wala vurugu, badala yake kwa ukarimu. Hataki kujiingiza katika mjadala, lakini kujiondoa katika kiburi. Kwa maana hiyo Papa ameongeza kwamba ni muhimu kuzima pamoja na chuki ukosefu wa haki kwa kutafuta kurudisha ndugu mkosaji. Hiyo ndiyo maana ya kugeuza shavu jingine, na kwa upole wa Yesu ni jibu la nguvu zaidi la mtu ambaye aliyempiga kofi. Hiyo sio rahisi, lakini Yesu alifanya hivyo na anatuomba kufanya hata sisi hivyo. Kugeuza shavu jingine haina ya kushindwa, lakini ni tendo la yule ambaye ana nguvu kubwa zaidi za ndani, kugeuza shavu jingine ni kushinda ubaya kwa wema ni yule ambaye anafungulia wazi moyo adui na kumwondolea uongo wa chuki usio na maana. Hiyo ndiyo tabia, hiyo ndiyo maana ya kugeuza shavu, na haiamriwi na hesabu au chuki, lakini kwa upendo. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa ni upendo wa bure na usiostahili tunaoupokea kutoka kwa Yesu na ambao unazaliwa katika moyo kwa namna ya kufanya uwe sawa na wake na ambao unakataa kila aina ya kulipiza visasi. Kwa kuongeza amesema “Na tumezoea kulipiza kisasi: “Ulinifanyia hivi, nitakufanyia kingine ...” au kuweka chuki hii moyoni, chuki inayoumiza, huharibu mtu”.
Papa akiendelea ameuliza swali je kwa upande mwingine inawezekana mtu kufikia kupenda adui wake? Ikiwa inatokana na sisi wenyewe, isingewezekana. Lakini tukumbuke kuwa ikiwa Bwana anaomba chochote, maana yake anataka kutoa. “Ikiwa ananiambia nipende maadui, anataka kunipa uwezo wa kufanya hivyo. Tukumbuke kuwa kamwe Bwana atuombi kitu ambacho yeye kwanza hajatoa”. Bila uwezo huo sisi hatuwezi, lakini yeye mwenyewe anatueleza kupenda na yeye anakupatia uwezo wa kupenda. Mtakatifu Agostino alikuwa anasali sala nzuri sana kwamba: “Bwana unipatie kile nikuambacho na uniombe kile ambacho unataka (taz. maungamo X, 29.40). Lakini kwa nini ulinipatia kwanza. Je ni kitu gani cha kumwomba? Je ni kitu gani Mungu anafuraha ya kutuzawadia? Papa ameuliza swali na anajibu kuwa ni “nguvu ya kupenda, ambayo sio kitu, lakini ni Roho Mtakatifu. Nguvu ya kupenda ni Roho Mtakatifu na kwa Roho wa Yesu, tunaweza kujibu ubaya kwa wema, tunaweza kupenda yule anayetutendea vibaya. Kwa hilo ndivyo wanavyo fanya wakristo”. Papa Francisko ameongeza kusema: “Kwa jinsi gani ilivyo na huzuni kuona watu ambao wanajidai kuwa wakristo hasa na wanawaona watu wengine kama maadui na wanafikiria kufanya vita! Ni huzuni sana.
Swali jingine ambalo Papa ameuliza: “Na sisi je tunajaribu kuishi kwa mujibu wa mialiko ya Yesu? Tufikirie mtu ambaye aliyetufanyia vibaya. “Kila mmoja afikirie mtu mmoja maana hii ni hali ya pamoja tuliyo nayo haraka ya ubaya wa mtu, tukirie mtu yule. Labda bado kuna hasira ndani mwetu. Na kwa maana hiyo hasira hiyo tuiweke karibu na picha ya Yesu, mnyenyekevu wakati wa mchakato wake baada ya kupigwa kofi”. Na baadaye tuombe Roho Mtakatifu atende katika moyo wake. Mwishowe tumwombee mtu yule, tuombe kwa ajili ya yule aliyetutendea vibaya (Lk 6,28), ndiyo jambo la kwanza kwa ajili ya kubadili ubaya kwa wema kwa sababu sisi mara tunapotendewa vibaya, tunakwenda haraka kuwasimulia wengine na kuhisi kuwa waathirika kwa maana hiyo ni vema tusimane na kumwombea mtu yule, ili Mungu atusaidie ili hisia za chuki zinaweza kupungua katika kusali kwa ajili ya yule aliyetufanyia vibaya. Bikira Maria atusaidie kuwa wahudumu wa amani kwa wote, hasa kuelekea yule aliye mgumu kwetu na hatumpendi.