Tafuta

Mwaka Mtakatifu ujao 2025 Mwaka Mtakatifu ujao 2025 

Papa Francisko ametangaza Jubilei ya 2025:Jubilei ijayo irudishe tumaini!

Katika barua ambayo amemwandikia Askofu Mkuu Fisichella,Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishai mpya,baraza lililokabidhiwa kuandaa Mwaka Mtakatifu anaelezea kuhusu maandalizi kwa njia ya sala na tafakati na kugusa mateso na hofu kutokana na janga.Jubilei ijayo inaweza kusaidia sana kurudisha hali ya tumaini na imani katika ishara za upyaisho wa kuzaliwa upya na ambapo kila mmoja anatamani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 11 Februari ametumia barua kwa Askofu Mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Uinjilihsji mpya kwa asili ya Jubilei inayotarajiwa kufanyika 2025. Papa anaandika kwamba Jubilei daima inawakilisha katika maisha ya Kanisa tukio moja kubwa ambalo linagusa kiroho, kikanisa na kijamii. Papa anasema kuwa tangu Papa Boniface VIII, mnamo 1300 alipoanzishwa Mwaka wa kwanza Mtakatifu kwa tukio la kijamii ambalo baadaye likawa ndiyo mtindo  wa kibiblia wa miaka hamsini na kwa maana hiyo ikawekwa kwa kila miaka ishiri na mitano,Watu waamini wa Mungu waliishi maadhimisho haya kama moja ya zawadi maalum ya neema, yenye tabia la msamaha wa dhambi na kwa namna ya pekee ya Rehema, kielelezo kabisa cha huruma ya Mungu. Waamini mara nyingi katika mchakato wa hija yao ndefu, wanachota tunu ya kiroho ya Kanisa kwa kupitia MlangoMtakatifu na kuheshimu masalia ya Watakatifu Petro na Paulo walinzi wa Makanisa Makuu ya Roma. Milioni na milioni ya wanahija, katika mchakato wa karne, wameweza kufika katika maeneo haya matakatifu kwa kutoa ushuhuda hai wa imani daima.

Mtakatifu Paulo II alikuwa na shauku ya jubiei 2000

Baba Mtakatifu Francisko anandika kwamba Jubilei kubwa ya mwaka 2000 iliwekwa na Kanisa la Milenia ya tatu ya historia yake. Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa anaisubiri sana na shauku, na  matumaini kwa wakristo wote, kwamba kwa kushinda migawanyiko ya kihistoria, wangeweza kuadhimisha pamoja miaka elfu mbili ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo Mwokozi wa ubinadamu. Na sasa mtazamo uko karibu wa miaka ishirini na tano ya kwanza ya Karne ya XXI, na tunaalikwa kujiweka katika tendo la maandalizi ambayo yanaruhusu watu wakristo kuishi Mwaka Mtakatifu kwa jitihada zote za kichungaji. Ni hatua yenye maana na kwa namna ya kwamba Jubilei maalum ya Huruma iweze kuruhusu kugundua kwa upya nguvu zote na upole wa upendo wa huruma ya Baba na ili kuweza kuwa mashuhuda kwa mara nyingine tena.

Janga la miaka miwili na sayansi kupata mbadala

Katika miaka miwili ya mwisho hata hivyo, hakuna nchi hata moja ambayo haikukumbwa na janga la ghafla na ambalo zaidi ya kufanya kuguswa kwa mkono janga la mauti na upweke, ukosefu wa uhakika na asili ya muda ya kuwepo, limebadilisha namna yetu ya kuishi. Kama wakristo tumeteseka pamoja na ndugu kaka na dada wote mateso sawa na vizingiti. Makanisa yetu yalibaki yamefungwa, kama ilivyokuwa shule, viwanda, maofisi, maduka, na maeneo yote husika yanayotumiwa wakati watu wako huru. Wote tuliishi vizingiti vya baadhi ya uhuru na janga zaidi ya kuleta uchungu, limesababaisha hata mashaka makubwa katika roho, hofu  na mahangaiko. Wanaume na wanawake wa kisayansi hata hivyo, kwa uharaka wake wa wakati waliweza kupata mbadala ambao taratibu taratibu uliruhusu kurudi katika ukawaida wa maisha ya kila siku.  Papa anaongeza kusema:“tunayo imani kuwa janga linaweza kushindwa na dunia kuweza kurudia katika tamu tamu zake na uhusiano kibinafsi na maisha ya kijamii. Lakini hiyo itakuwa rahisi zaidi kutokana na hatua ambazo zitachukuliwa za mshikamanao, ili watu walio maskini zaidi wasisahauliwe,na wakati huo huo  uvumbuzi wa kisayansi na dawa zinazohitajika ziweze kushirikishwa ka wote.

Jubilei ijayo inaweze kusaidia kurudisha hali ya tumaini na imani

Papa Francisko amebainisha juu ya  kuzingatia kuendelea kuwa na mipango ya matumaini ambayo tulipewa, na kufanya kila njia ili kila mmoja aweze kupata nguvu na uhakika wa kutazama wakati ujao kwa moyo ulio wazi, moyo wa imani na akili ya matazamio ya mbele. Katika Jubilei ijayo inaweza kusaidia sana kurudisha hali ya tumaini na imani katika ishara za upyaisho wa kuzaliwa yote ambayo kila mmoja anatamani. Ndiyo maana Baba Mtakatifu amesema alichagua kauli mbiu: “Hija ya Matumaini”. Hayo yote lakini yatawezekana ikiwa tutakuwa na uwezo wa kurudisha mana ya udugu wa kibinadamu, na ikiwa hatutafumba macho mbele ya janga la umaskini ulisambaa ambaounazuia mamilioni ya wanaume, wanawake, vijana na watoto kuishi kwa namna inayostahili kibinadamu. Papa amefikiria hasa wakimbizi wengi wanaolazimaka kuacha nchi zao, Sauti za maskini ziweze kusikilizwa katika wakati wa kuandaa Jubileio ambauo kwa mujibu wa amari ya kibiblia n kurudishia kila mmoja uwezekanao wa matunda ya nchi “ Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumwa wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe; na kwa hayawani wako, na kwa wanyama walio katika nchi yako; maongeo yote yatakuwa ni chakula chao. (Mambo ya Malawi 25,6-7).

Mwelekeo wa Jubilei unaalika kuwa na uongofu

Kwa hiyo, mwelekeo wa kiroho wa Jubilei ambao unatualika katika uongofu unafungamanishwa na mantiki hizi msingi za kuishi kijamii, kwa ajili ya kujenga umoja wa kweli. Kwa kujihisi kuwa sisi sote ni wanahija katika nchi ambayo Bwana alituweka ili tuilime na kuitunza (Mw 2,15), tusiidharau, katika mchakato mrefu wa safari, wa kutafakari uzuri wa uumbaji na kutunza nyumba yetu ya Pamoja. Ni matarajio ya Baba Mtakatifu kwamba Mwaka ujao wa Jubilei uadhimishwe na kuishi hata kwa malengo hayo. Kiukweli idadi kubwa inayozidi kuongezeka ya watu, mongoni mwao ni  vijana wengi wadogo wanaotambua kuwa utunzaji wa kazi wa uumbaji ni kielelezo msingi cha imani kwa Mungu na kutii mapenzi yake. Baba Mtakakatifu Francisko kwa maana hiyo anamkabidhi kaka huyo uwajibikaji wa kutafuta mitindo inayofaa ili Mwaka Mtakatifu uweze kuandaliwa na kuadhimishwa kwa imani ya kina, matumaini hai na upendo wa dhati. Baraza la kipapa ambalo linahamasisha uinjilishaji mpya, Papa ameandika kuwa litatambua namna ya kufanya wakati huo wa neema kuwa hatua muhimu kwa ajili ya uchungaji wa Kanisa mahalia, Kilatino na Mashariki ambao kwa miaka hii wote wanaalikwa kuzidisha juhudi za Sinodi. 

Kanisa ni ishara hai na chombo cha umoja

Katika muktadha huo, hija kuelekea Jubilei itaweza kuongeza nguvu na kujieleza pamoja katika safari ya Kanisa ambalo linaalikwa kutimiza daima na zaidi na kuwa ishara bora na chombo cha umoja katika maelewano kwenye utofauti. Baba Mtakatifu Francisko anasema itakuwa muhimu kusaidia kugundua mahitaji ya wito wa ulimwengu katika kushiriki uwajibikaji, katika kuthamanisha karama na huduma ambazo Roho Mtakatifu hakosi kamwe kuzitoa katika ujenzi wa Kanisa moja. Na kwa Hati Nne za Mtaguso wa II  wa Vatican, zilizounganishwa na mafundisho haya kwa makumi ya miaka zitaendelea kuelekeza na kuongoza Watu watakatifu wa Mungu ili waendelee katika utume wa kupeleka kwa wote furaha ya kutangaza Injili. Kulingana na desturi za Hati ya maelekezo ambayo yatatolewa kwa wakati ufaao, itakuwa na taarifa zinazohitajika kusherehekea Jubilei ya 2025. Katika wakati huu wa maandalizi, Papa Francisko anafurahi kufikiria kwamba itawezekana kufanya mwaka unaotangulia 2024 kuwekwa wakfu kwa ajili ya tukio hilo la Jubilei kwa maelewano makuu ya sala.

Mwaka 2024 utakuwa ni mwaka wa sala

Papa Francisko amefafanua kuhusu mwaka wa Sala kwamba, awali ya yote ili kurejesha shauku ya kuwa katika uwepo wa Bwana, kumsikiliza na kumwabudu. Sala, zaidi  ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi nyingi za upendo wake kwetu na kusifu kazi yake katika uumbaji, pia ni ambayo inawapa kila mtu heshima na hatua thabiti na ya kuwajibika kwa ajili ya ulinzi wake. Sala kama sauti ya moyo mmoja na roho moja (Mdo 4,32), ambayo inajifafanua katika mshikamano na katika kushirikishana mkate wa kila siku. Sala ambayo inaruhusu kila mwanaume na mwanwamke wa ulimwengu huu kumgeukia Mungu mmoja, ili kumweleza kile ambacho kimo ndani ya siri ya moyo. Sala kama njia mwalimu kuelekea utakatifu na ambayo inaelekeza kuishi kwa kutafakari hata katikati ya matendo. Kwa mahiyo  utakuwa ni  mwaka wa kina wa kusali ambamo mioyo inafunguka kupokea neema nyingi kwa kufanya Baba Yetu  sala ambayo Yesu alitufundisha, mpango wa maisha ya kila mfuasi wake. Papa anahitimisha akiomba Bikira Maria awasindikize Kanisa katika safari ya kujiandalia tukio la Neema ya Jubilei na kwa shukrani kutoka moyoni anamtumia Yeye na wahudumu wake Baraka za kitume.

BARUA YA PAPA KWA AJILI YA JUBILEI 2025
11 February 2022, 12:31