Tafuta

Kila tarehe 11 Februari ni siku ya wagonjwa duniani Kila tarehe 11 Februari ni siku ya wagonjwa duniani 

Papa Francisko akumbusha Siku ya 30 ya Wagonjwa duniani

Wakati wa Katekesi yake Papa Jumatano,amewakumbusha Siku ya Kimataifa ya Wagonjwa na sala maalum kwa wanaoteseka kiroho na kimwili na ambao wanawasaidia.Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 160 tangu kutambuliwa kwa Bikira Maria kutokea Lourdes.Papa amesema:“Natamani kila mmoja amwige Bikira Mbarikiwa kwa kuonekana kwa mapenzi ya Mungu.Mfano wake na maombezi yake yawe kichocheo cha kuimarisha ushuhuda wa Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 11 Februari ni Siku ya 30 Kimataifa kwa ajili ya Wagonjwa ambayo ilianzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kwa kutaka kuwatia moyo Watu wa Mungu, Taasisi Katoliki za kiafya na za kiraia ili kuongeza utambuzi na umakini kwa ajili ya wagonjwa na wale wote ambao wanawatunza. Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya mwaka huu ni: “Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma” (Lk 6:36): Kuwa karibu na wale wanaoteseka kwenye njia ya upendo”.

Miaka 160 ya kutokea kwa Bikira Maria wa Lourdes

Katika kufanya kukumbuka ya siku hii na ambayo inakwenda sambamba na  Kumbu Kumbu ya Mtakatifu Bikira Maria wa Lourdes, Papa amependa kuwakumbuka wagonjwa wote na ili wote waweze kuhakikishiwa tiba ya kiafya na kusindikizwa kiroho. Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya kaka na dada hao, kwa ajili ya familia, kwa ajili ya wahuduma wa afya na kichungaji na wale wote wanaoendelea kuwatunza wagonjwa hao. Hata hivyo katika kuelekea siku kuu hiyo, Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 160 tangu kutambuliwa kwa Bikira Maria kutokea Lourdes, hivyo Papa amesema: “Natamani kila mmoja amwige Bikira Mbarikiwa kwa kuonekana kwake kikamilifu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Mfano wake na maombezi yake yawe kichocheo cha kuimarisha ushuhuda wa Injili”. Katika ujumbe wake wa wa kuadhimisha Siku ya Wagonjwa Duniani mwaka 2022, Papa Francisko anasisitizia utume wa kuwakaribisha na kuwasindikiza wagonjwa.

Mgonjwa daima ni muhimu zadi kuliko ugonjwa wake

Papa anasema kwamba: “Mgonjwa daima ni muhimu zaidi kuliko ugonjwa wake na hii ndiyo sababu mbinu yoyote ya matibabu haiwezi kupuuza kusikiliza ... Tunawezaje kusahau kukumbuka katika suala hili, wagonjwa wengi ambao, wakati wa janga wameishi yao”. Papa pia anasisitiza kwamba: “Hata wakati uponyaji hauwezekani, lakini utunzaji unawezekana kutolewa kila wakati. Daima inawezekana kufariji, kila mara inawezekana kufanya watu wahisi ukaribu ambao unavutiwa zaidi na mtu kuliko ugonjwa wake. Siku ya 30 ya Wagonjwa Ulimwenguni haitafanyika huku Arequipa, nchini Peru, kama ilivyokuwa imepangwa, kwa sababu ya janga la UVIKO kuendelea. Maadhimisho ya Misa Takatifu sasa yatafanyika tarehe 11 Februari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

09 February 2022, 16:32