Papa:Biashara ya binadamu ni majeraha ya mwili wa Kristo na ubinadamu
Na Angella Rwezaula
Baba Mtakatifu ametuma ujumbe wake kwa njia ya video katika Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu, inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 Februari, sambamba na Mama Kanisa kufanya kumbukumbu ya Mtakatifu Josephine Bakhita. Ujumbe wake ameulekeza kwa waandaaji wa Siku hii ya kimataifa ambao ni Umoja wa Mama Wakuu wa mashirika ya Kimataifa wa Umoja wa Wakuu wa Mashirikia ya kiume, kwa kushirikiana na kiikundi cha Talitha Kum ambacho kinaratibu mpango huo na kushirikiana na mashirika mengi mahalia na kimataifa. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video amesema kauli mbiu inayoongoza maadhimisho haya mwaka huu ni: “Nguvu za Kutunza, Wanawake, uchumi na biashaara haramu ya Binadamu”: na ambayo inatoa mwaliko wa kufikiria hali za wanawake na wasichana, ambao wako chini ya mitindo mingi ya unyonyaji, hata kwa njia ya ndoa za kulazimishwa, utumwa wa kinyumbani na kazi. Maelfu ya wanawake na watoto wa kike wanauzwa, na kuthibitish janga kubwa na matokeo ya mitindo inayohusu hali hiyo kuhusu ubaguzi na unyonyaji. Sio kutia chumvi lakini ni maelfu na malfu”, Papa amesema.
Muundo wa Kijamii katika ulimwengu, bado uko mbali kuangazwa na kutambua uwazi zaidi ya kujua kuwa wanawake wana hadhi sawa na haki sawa na wanaume. Kwa bahati mbaya imeoneshwa kuwa mara dufu wanawake wanateseka na hali hii ya kubaguliwa, kutendewa vibaya, na vurugu kwa sababu mara nyingi wanajikuta wana uwezo mdogo wa kutetea haki zao (taz. Waraka wa Fratelli tutti, 23). Biashara haramu wa watu, kupitia unyanyasaji wa nyumbani na ule wa kingono, na ukatili huwarudisha wanawake na wasichana kwenye jukumu lao linalodhaniwa kuwa ni wasaidizi wa utoaji wa huduma za nyumbani na ngono, kwa jukumu lao kama watoa huduma na watoa raha, ambao wanapendekeza tena muundo wa uhusiano uliowekwa alama na uwezo wa jinsia ya kiume kuhusu mwanamke. Hata leo hii kuna kiwango cha juu sana . Na Biashara haramu ya watu ni ukatili! Ukatili anaopata kila mwanamke na kila msichana ni jeraha lililo wazi katika mwili wa Kristo, katika mwili wa wanadamu wote, ni jeraha kubwa ambalo pia linampata kila mmoja wetu, Papa amesisisitiza. Wanawake ni wengi ambao wanaujasiri wa kujikomboa na vurugu. Papa Francisko ameongeza kusema kuwa: “Hata sisi wanaume tunaalikwa kufanya hivyo na kusema hakuna kufanya vurugu ya kila aina, ikiwemo dhidi ya wanawake na watoto wa kike. Na kwa pamoja tunaweza na lazima kupambana kwa sababu haki za binadamu ziweze kuwapo mtindo maalum katika heshima ya utofauti na utambuzi wa hadhi ya kila mtu na moyo kwa namna ya pekee ambaye amekanyagwa haki zake msingi.
Papa anasema Mtakatifu Bakhita, anatuonesha njia ya kubadilika. Maisha yake yanasimulia kuwa mabadiliko yanawezekana ikiwa unaacha kubadilishwa na utunzaji wa Mungu alio nao kwa kila mmoja wetu. Ni utunzaji wa huruma, ni utunzaji wa upendo ambao unatubadili kwa kina na kutufanya kuwa na uwezo wa kuwakaribisha wengine kama kaka na dada. Ni tendo la kwanza la utunzaji wa kutambua hadhi. Na utunzaji ni mwema kwa wote, wanaotoa na wale wanaopokea kwa sababusio tendo linaloelekeza sehemu moja bali linaelekezana. Mungu alimtunza Josephine Bakhita, akamsindikiza katika mchakato wa uponyaji wa majeraha yaliyosababishwa na utumwa hadi kumfanya moyo wake, akili yake na umbu lake kuwa na uwezo wa kujipatanisha, wa uhuru na wa huruma.
Papa Francisko anawatia moyo kila mwanamke na kila msichana ambaye anajitihidi kubadilika na kutunzwa, katika shule, familia na katika jamii. Na anawatia moyo kila mwanaume na kila mvulana asibaki nje ya mchakato huo wa kufanya mabadiliko, kwa kukumbuka mfano wa Msamaria mwema ambaye hakuona aibu ya kumwinamia kaka yake na kumsaidia. Kutunza ni utendaji wa Mungu katika historia, yetu binafsi na anamtunza kila mmoja wetu katika historia ya binadamu; Mungu alijifanya hivyo kutunza na anatoa kwa kila mmoja daima. Kutunza pamoja na wanaume na wanake ni mwaliko wa Siku ya Kimataifa kwa ajili ya sala na tafakari dhidi ya biashara ya bunadamu; pamoja tunaweza kufanya kukua uchumi wa kutunza na kupinga kila aina ya nguvu za mitindo ya unyonyaji wa biashara ya binadamu
Kwa kuhitimisha, Papa Francisko anatambua jinsi wanavyoshiriki wengi katika Siku hii ya sala na tafakari, katika nchi mbali mbali na katika tamaduni nyingi za kidini. Kwa wote Papa anatoa shukurani na kuwatia moyo wa kuendelea mbele katika mapambano dhidi ya biashara ya watu na kila aina ya utumwa mamboleo na unyonyaji. Ninawaalika nyote kuweka hasira hai, weka hasira hai! - na kila siku kupata nguvu ya kujitolea kwa uamuzi juu ya suala hili. Usiogope mbele ya kiburi cha jeuri, hapana; usijisalimishe kwa ufisadi wa pesa na madaraka. Papa amewaomba wasikate tamaa, wabarikiwe na amewapa baraka kwa kazi yao.