Ujumbe wa Papa kwa Chuo Kikuu Crakow:Mafunzo yatimize ndoto za vijana
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Katika Ujumbe wa Papa wa matashi mema kwa kutumiza miaka 625 kwa ajili ya Kitivo cha Kitaalimungu cha Chuo Kikuu cha kipapa cha Yohane Paulo II huko Krakow nchini Poland aliyoilekeza kwa Askofu Mkuu Marek Jędraszewski Kansela Mkuu wa Chuo Kikuu hicho na kusema kwamba ilikuwa ni tarehe 11 Januari 1397 kwa maombi ya Malkia, Mtakatifu Edwige na Mme wake Ladislao, Papa Bonifacio IX, kwa barua yake ya “Eximiae devotionis affectus”, ikimaanisha“kuwa na hisia nzuri za ibada” kilianzishwa Kitivo cha Kitaalimungu cha wakati huo, cha Elimu huko Krakow na baadaye Chuo Kikuu Jagellonica. Uendelezwaji wake kwa sasa ni Kitivo cha Kitaalimungu cha Kipapa cha Chuo Kikuu cha Yohane Paulo II. Kwa maana hiyo imepita miaka 625 tangu tukio hilo la wakati na ambalo lilitoa mwanzo wa historia ya Chuo cha Kipapa kwa cha sasa.
Hakuna kusahau utamaduni katika nyakati za sasa
Papa Francisko amesema pamoja nao anamshukuru Mungu kwa utamaduni wa karne sita ambao umeweza kupatikana wa kisayansi na kitaaluma na kama ilivyo tasaufi yake uliyoundwa na watakatifu waanzilishi, maprofesa na wanafunzi. Historia yao wanayoijenga, wakati huu ni kubwa mno na muhimu, lakini wakati huo huo yenye kuhitaji umahili. Nyakati za sasa, Papa amebainisha zinahitaji kila mmoja hasisahau utumaduni, na wakati huo huo kutazama kwa matumaini wakati ujao na kuunda wakati ujao.
Mazingira ya Vyuo vikuu yanaunganisha utume wa Kanisa ili kueneza Injili duniani
Kauli mbiu ya Chuo kikuu inaitwa “Nendeni na mkawafanye wafuasi wangu” (Mt 28,19), na hati kuhusu utume wake inathibitisha kwamba shughuli zake zinajikita kutafakari kisayansi kuhusu masuala ya Maonesho, kwa kutumia njia ya utafiti wa kizamani na kisasa. Mtakatifu Yohane II alisisitizaia ulazima wa huduma ya wazo na kwamba mazingira ya Vyuo vikuu yanaunganisha utume wa Kanisa ili kueneza Ujumbe wa Kristo katika ulimwengu. Kutokana na hilo Papa Francisko amesisitiza kwamba kwa kuwa na imani ya utamaduni wa kale, wasome ishara za nyakati, wapokee kwa ujasiri changamoto mpya ili kuweza kupeleka kwa dhati Ukweli wa Injili kwa mwanadamu wa sasa na ulimwengu.
Kujifungulia kile ambacho ni muhimu, kinachodumu na kisichopita.
Chuo kikuu chao Papa Francisko ameongeza kusema kiweze kuwa mahali pa mafunzo kwa vizazi vipya vya kikristo, si kwa ajili ya kupitia mafunzo ya kisayansi na tafiti za ukweli tu, lakini pia kwa njia ya shuhuda kijamii ya kuishi kwa imani. Na iwe Jumuiya ambayo zinapatikana fahamu zinazo unganisha na kuhamasisha heshima ya kila mtu kwa ajili ya upendo wa Mungu ambaye alimuumba na kujali mafunzo ya mioyo kwa kujifungulia kile ambacho ni muhimu, kinachodumu na kisichopita.
Wazo na tafiti la ukweli katika Kanisa la Poland na ulimwenguni
Papa amesisitiza kuwa “Vijana wana ndoto zao na hatima zao na Chuo Kikuu Katoliki kinapaswa kuwasaidia kuzitimiza kwa msingi wa ukweli, wa wema na wa uzuri walio nao katika kisima cha Mungu. Kazi yake ya kuunda wazo na utafiti wa ukweli ni wa lazima leo hii katika Kanisa nchini Poland na ulimwengu mzima. Papa Francisko amewahimiza wapeleke mbele kwa maana ya uwajibikaji ili kuwa waaminifu wa utume wao, wao usemao: “Enendeni na mkawafanye wafuasi! Kwa kuhitimisha Ujumbe wa matashi mema Papa Francisko amekabidhi sala zake kwa Mungu kwa ajili ya Gambera, Maprofesa, wanafunzi na wahudumu wa Chuo Kikuu hicho, huku akiomba kwa maombezi ya Mtakatifu Edvige na Malkia, mwanzilishi wa Kitivo hicho na maombezi ya Mtakatifu Yohane Paulo II amewatumia kwa moyo wote Baraka za Kitume kwa wote.