Tafuta

2022.01.29  Papa amekutana na wajume wa Chama cha Italia cha wanakemia wa Ngozi 2022.01.29 Papa amekutana na wajume wa Chama cha Italia cha wanakemia wa Ngozi 

Papa kwa wataalamu wa Ngozi:vijana wanahitaji kazi ya kizamani,kukutana na wazee

Papa Francisko akikutana na wanachama wa Italia,wataalamu wa Ngozi,amebainisha juu ya changamoto ya wakati huu kuwa ni mkutano kati ya babu na wajukuu,labda kuwapita wazazi,lakini mkutano huo ni muhimu na lazima kufanya kazi ili vijana wakutane na wazee.Wataalamu hao wanaitwa kutoa mchango muhimu wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja ili kupunguza madhara ya mazingira.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 29 Januari 2022, Papa Francisko amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Chama cha Italia cha wataalamu wa Kemia wa Ngozi, hivyo ni  wanasayansi wa Kemia ambapo ametoa salamu na kumshukuru  Rais wa Chama hicho kwa kuwakilisha kazi yao,na kwamba anakutana nao kwa sababu tofauti. Lakini kabla ya kuanza hotuba hiyo, alisema anavyopendelea kuwaona wamama ambao wanabembeleza watoto. Ni vizuri wanapokuja na watoto wao. Na ikiwa wanataka watembee wangeweza kuwaachia huru wafanye watakavyo na kama wana njaa wale maana wao ni wafalme! Akiendelea Papa amesema, kwanza kabisa kwa sababu wao ni wafanyakazi maalum, ambao hutoa mchango wa asili na wa tabia katika sehemu nyingi kubwa ya jamii ya ulimwengu. Taaluma yao inatumia maarifa ya kisayansi na kiufundi kwa shughuli ya ufundi ambayo ina utamaduni wa zamani, nchini Italia na katika nchi nyingine, ikijumuisha hata nchi yake Argentina. Akiwa kijana Papa amesema alisomea katika taasisi ya kiufundi yenye mwelekeo wa Kemia,na hivyo  kidogo imemleta karibuna kazi yao.

Katika wakati wa mgogoro wa kichumi na kijamii ulio mgumu, ametumia fursa hiyo hata kwa ajili ya kuelezea ukaribu wake na wa Kanisa kwa ulimwengu wa kazi. Wengi wa wafanyazi wa kike na kiume na familia nyingi wanaishi katika hali ngumu zilizosababishwa na janga. Lakini janga haliwezi kuwa sababu ya kisingizio cha kutokujali haki au usalama. Kinyume chake, mgogoro unaweza kukabiliwa kama fursa ya kukua pamoja katika mshikamano na katika ubora wa kazi. Papa Francisko amesema kwamba mfano na maombi ya Mtakatifu Yosefu yawasaidie wasiangukie kukata tamaa katika kuthamanisha ubunifu wao wa talanta na uzoefu wao mkubwa wa kwenda mbele na kufungua njia mpya. Katika hili ni muhimu kufanya kukutana na hekima ya wazee na shauku ya vijana. Vijana waweze kukutana na ndiyo siri , Papa amesisitiza.

Katika hili Papa Francisko amefikiria vijana ambao wanapenda sekta halisi kama yao na wanahitaji kukutana na kazi za kizamani ambazo zina mambo mengi ya kujifunza, nasi katika mpango wa kiufundi, lakini pia hata wa kibinadamu. “Kwangu mimi changamoto ya wakati huu ni mkutano kati ya babu na wajukuu, labda kuwapita wazazi, lakini mkutano huo ni muhimu na lazima tufanye kazi ili vijana wakutane na wazee. Ni changamoto ya wakati huu”, amesisitiza. Mantiki nyingine ambayo Papa amependa kugusia  ni jambo muhimu sana ambalo yeye alikuwa anajua linawagusa kwa karibu, kwa sababu alilitaja hata Rais wa chama hicho. Ni muktadha wa mazingira ya kazi kama yao ambao wanatumia kemikali kutibu vifaa, kwa upande wao, ngozi zinazokusudiwa kuwa mifuko, viatu na kadhalika, vitu vingi tunavyotumiwa kila siku na kwamba hatufikirii juu ya kazi iliyo nyuma yake!

Kwa hiyo Papa akieleza kwa wataalamu hao wa ngozi na ambao amesema wanaitwa kutoa mchango muhimu wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja ili kupunguza madhara ya mazingira ya uzalishaji wa ngozi huku wakihifadhi urithi wao wa kitaaluma na wanaweza kufanya hivyo kwa namna ya kuweka umakini katika kazi zao. Kwa lengo hilo ni thamani kubwa kufanya ushirika ili kuweka pamoja fahamu, uzoefu kama ilivyo hata usasishaji kisheria na kiufundi; na kwa kufanya hivyo wanasaidiwa kukua pamoja katika mtindo mmoja wa uwajibikaji kijamii na kiikolojia. Hilo ni muhimu Papa amesisitiza. “Leo tunafahamu zaidi wajibu wa kiikolojia; tulikulia katika hili”. Kwa kuhitimisha Papa amewashukuru tena kufika kwao. Amewatakia kila mema katika kazi yao na shughuli za Chama chao, amewabariki na familia zao. Amewaomba wasisahu kusali kwa ajili yake.

29 January 2022, 13:09