Papa Francisko:wazazi wahangaikiao watoto wao ni mashujaa na jasiri
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko anawaita mashujaa wazazi wale wanaangaika katika janga; wale ambao wanatafuta wakati ujao kwa ajili ya watoto wao kwa kuhamia sehemu nyingine na wale ambao wanateseka sana. Amefafanua kuwa ujasiri wa wazazi hao ni wa kishujaa. Baba Mtakatifu Francisko amesema hayo katika mahojiano yaliyofanywa na vyombo vya habari Vatican kwa kutayarishwa na Mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano, Andrea Monda, na Makamu mhariri wa Baraza la Kipapa kwa Mawasiliano Dk. Alessandro Gisotti. Katika mahojiano hayo yametazama hasa mwaka Maalum wa Mtakatifu Yosefu uliohitimishwa hivi karibuni mnamo tarehe 8 Desemba 2021 kwa mzunguko wa katekesi ambazo zimeanza tangu tarehe 17 Novemba 2021, ambapo Papa bado anaendelea kujikita na sura hii ya Msimamizi wa Kanisa la Ulimwengu. “Ninahisi sana ukaribu wa balaa la mababa na mama wengi ambao wako wanaishi kwa namna ya pekee na matatizo ambayo yamesababishwa hasa na janga. Ninaamini kuwa hayo sio mateso yaliyo rahisi ya kukabiliana nayo, hasa yale ya kutokuweza kuwapatia watoto wao binafsi mkate na kuhisi mabegani uwajibikaji wa maisha ya wengine”. Kwa wote hao,Papa anawakikishia sala zake, ukaribu na msaada na kwamba si tu wa kibinafsi, lakini pia hata wa Kanisa zima. Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema:“ wazazi msijihisi peke yenu! Papa hawasahau!
Mateso ya wazazi wakimbizi na watoto wao ni sawa na familia takatifu
Wazo la Papa kuhusu wanawake na wanaume, na familia nyingi ambazo zinakimbia vita na ambao wamekataliwa hata mipakani mwa Ulaya lakini pia hata wale ambao wanaishi hali ya uchungu, ya ukosefu wa haki na ambao hakuna anayezingatia hali hiyo mbaya au kuidharau kwa utashi tu. “Papa amesema: “Ninataka kusema kuwa kwangu mimi hao ni mashujaa kwa sababu ninaona katika wao ule ujasiri wa kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya upendo wa watoto wao na familia zao”. Papa Francisko kwa maana hiyo anatazama sura ya Mama Maria na Yosefu ambao walifanya uzoefu wa kukimbia katika Nchi ya ugenini ili kukimbia vurugu za Mfalme Herode. Mateso yao, yanawafanya kuwa kama mateso hayo hasa ya wale ndugu ambayo leo hii wanateseka namna hiyo hiyo na majaribu. Papa Francisko anatoa mwaliko kwa mababa wote ili waweze kumgeukia kwa imani kuu Mtakatifu Yosefu kwa utambuzi kuwa, yeye kama baba aliweza kufanya uzoefu huo wa ukosefu wa haki. Anawatia moyo wa kutohisi peke yao kwa sababu Papa amekumbusha kwamba yeye yuko nao na daima inapowezekana anatoa sauti kwa niaba yake ili kutowasahu kamwe!
Mtakatifu Yosefu ni shuhuda angavu katika nyakati za giza ya Yesu Maria na Yosefu
Papa Francisko akiendelea na mahojiano hayo amebainisha kuhusu sura ya Baba mlinzi wa Yesu ambaye anadai kujisikia kuwa na maelewano ambayo yalianza akiwa mdogo na kuendeleza zaidi katika huduma yake ya Upapa na ambayo kwa hakika alianza mnamo tarehe 19 Machi 2013, katika sikukuu ya Mtakatifu Yosefu. Sambamba na hiyo, Papa Francisko amefafanua juu ya kuwa na ibada kuu sana na aliamini daima kwamba Mtakatifu Yosefu angeweza kumsaidia. Akifafanua amesema “Akiwa Mtu wa kawaida lakini pia muhimu wa historia ya wokovu, Mtakati fu Yosefu ni yule aliyemlinda na kumfanya mtoto akue. Katika yeye kuna mtu wa nyakati nguvu ambaye anajua kuchukua uwajibikaji na hasa kwa kuunganisha tabia mbili za kutambua kusikiliza Mungu na tabia ya kukabiliana na matatizo bila kuhisi kuonewa. Mbele ya vizingiti, Mtakatifu Yosefu anakabiliana navyo kwa kumwamini Mungu tu ili kupata suluhisho kwa namna ya ubunifu. Na hiyo ni katika nyakati za giza, ambazo zimesababishwa na janga, na yeye ni shuhuda angavu ambaye anatusaidia kupata njia Papa amesisitiza.
Hawazaliwi mababa bali wanageuka kuwa mababa
Ubaba hauzaliwi zaidi ya kugeuka kuwa Baba, Papa amesisititiza tena na kwa maana hiyo mababa wa leo hii wanashauriwa kutazama Mtakatifu, mlinzi na msimamizi wa Yesu kama mfano wa kuigwa, kwani anasema: “ Mtakatifu Yosefu kwa hakika alifanya vema kuwa baba hadi Yesu kufikia kupata upendo na katika ubaba wa mtu huyo kuwa mfano mzuri ambao Mungu Baba alimkabidhi mwanae. Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema kuwa watoto wa leo hii ambao watakuwa mababa wa kesho wanapaswa wajiulize maswali, je baba zao walikuwa namna gani, na je wao wanataka kuwa baba wa namna gani, ili wasiweze kuona nafasi ya ubaba inageuka kuwa ya bahati mbaya ai kwa urahisi matokeo ya wakati uliop, bali wa kuamua kuwa na upendo mkuu.
Baba wasiwe kizingiti cha watoto wao bali kuwa mfano wa kuigwa
Baba Mtakatifu Francisko baadaye amejikita kuulezea kitovu cha uhuru, ambayo ni moja ya tabia iliyo nzuri sana ya upendo na si tu kwa ubaba kwa sababu kama Mtakatifu Yosefu alivyo mtunza Yesu, bila kummiliki, bila kutaka kumwendesha, kwa namna hiyo, alikuwa baba mwema ambaye alijua kurudisha hatua yake nyu kwa wakati unaofaa ili mtoto aweze kuibuka na upekee wake, na wito wake. Kimsingi maamuzi sahihi ya upendo wa Yosefu kwa Yesu ni unyenyekevu wake, na ile tabia ya uficho wale ili Yesu aweze kuangaza kwa utume wake na kupata kutoka mfano wa Baba mlinzi mzuri ambao kamwe hakuwa kizingiti.
Kanisa sio la kimama tu lakini pia la kibaba
Mantiki ya ubaba inatazama hata Kanisa ambapo Papa anasema kwamba pia ni mama katika mazoezi ya huruma lakini ambayo inapaswa daima kuwa na ubaba wenye uwezo wa kuweka watoto katika kuchukua uwajibikaji, kwa kufanya mzaoezi ya uhuru wake na chaguzi zake. Katika kipindi cha historia ya sasa, ambacho vijana mara nyingi wanaogopa kuchagua, na kuthubutu, ni kazi ya Kanisa kuwatia moyo na kuwawezesha wawe na chaguzi kubwa. Ni kama afanyavyo kila baba ambaye hamwambii mtoto kwamba kila kitu kitakwenda vizuri lakini ambaye anasema utaweza kukabiliana na kuishi kwa heshima na hata kwa kukabiliana na matatizo na kushindwa yoyote.
Umuhimu wa baba wa kiroho na mama wa kiroho katika kufanya mang’amuzi
Baba Mtakatifu Francisko katika mahojiano amejikita kufafanua hata kuhusu ubaba wa kiroho na jinsi gani Makuhani wanapaswa wajifunze kidogo kidogo kuwa mababa, kwa kuanzia awali ya yote kujitambua wao wenyewe ya kuwa ni wana wa Mungu na wa Kanisa. Ikiwa Baba ni baba mwema ni kwa sababu anasaidia mtoto kujikamilisha mwenyewe na kwa kufanya iwezekanavyo awe na uhuru wake kwa kumsukuma katika kufanya maamuzi makubwa.Vile vile baba mwema wa kiroho anapochukua nafasi ya kutunza dhamiri ya watu wanaojikabidhi kwake, lazima aweza kuwa na busara na awe thabiti na inapowezekana aoneshe njia, na kusaidia kufanya mang’amuzi. Zawadi ambayo inazaliwa hasa kutokana na uzoefu ya ubaba wa kiroho leo hii ni ya lazima sana kuliko hapo awali, Papa Francisko amesisitiza kwa sababu ipo dharura kubwa ya kuwa na mahusiano yenye maana sana. Papa Francisko kwa njia hiyo amesisitizia hata wamama wa umama wa kiroho ambao unayo nafasi ya kusindikiza na ambayo inawahusu sana watawa wengi wa kile na walei ambao wanashirikishana sana mizigo mikubwa ya uzoefu.