Papa Francisko:Watoto wamepokea utambulisho wa Kikristo,ulindwe
Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.
Katika mazingira ya ajabu na mazuri sana chini ya ukumbi wa Kikanisa cha Sistine mjini Vatican ambapo mtazamo mara nyingi unaswa na picha ya mchoraji Michelangelo na uchoraji wa kuonesha Hukumu ya mwisho, watoto wachanga 16 wametabatizwa, Dominika ya Siku Kuu ya Ubatizo wa Bwana tarehe 9 Januari 2022 ambao ni watoto wa wafanyakazi wa Vatican. Mwaka 2021 Papa hakuweza kutoa Sakramenti ya Ubatizo kwa watoto wa kike na kiume kutokana na janga la uviko. Katika Kikanisa cha Sistine chenye uzuri wa kuashangaza palizinduliwa na Papa Julius II mnamo mwaka 1512, na ndimo hufanyika Mkutano wa kuchagua Papa. Katika mazingira hayo ya ajabu, zaidi ya watu milioni tano hustaajabishwa kila mwaka, (isipokuwa katika kipindi hiki kilichotikiswa na janga hili la UVIKO-19,) kwa kazi nzuri sana za kisanii ambazo zinatoka katika chanzo cha Biblia Takatifu.
Watoto ni kama roho zilizo wazi kupokea nguvu ya Mungu
Kwa maana hiyo Mara baada ya masomo, Papa Francisko ametoa mahubiri yake kwa kukumbusha kuwa “leo ni siku ya kukumbuka ubatizo wa Bwana. Kuna wimbo katika liturujia ambao ni mzuri katika siku kuu kama leo hii, ambao wanasema kwamba watu wa Israeli walikuwa wanakwenda Jordan kwa miguu peku na moyo peku, ikimaanisha moyo ambao ulikuwa unataka kuloweshwa na Mungu ambao haukuwa na utajiri wowote na ambao ulikuwa unahitaji Mungu”. Papa Francisko amefafanisha wimbo huo kama watoto wadogo hao kuwa , "Watoto hawa wamekuja hapa kama vile roho zilizo peku, ili kupokea haki ya Mungu, nguvu ya Yesu, nguvu ya kwenda mbele katika maisha, kupokea utambulisho wa Kikristo. Kwa urahisi ndiyo hilo", amesisitiza. Kwa kuongezgezea amesisitiza tena: “Watoto wenu watapokea leo hii utambulisho wa Kikristo. Wazazi na wasimamizi wa ubatizo mnapaswa kulinda utambulisho huo. Hiyo ndiyo kazi yenu wakati wa maisha yenu, wa kulinda utambulisho wa watoto wenu”. Na kwa kusisitiza kwamba ni kazi yao ya kila siku kuwafanya watoto wakue katika mwanga ambao wameupokea. "Hili ndilo nilipenda kuwaambia. Huo ni ujumbe wa leo wa kulinda utambulisho wa kikristo ambao ninyi mmewaleta leo hi watoto wenu ili waweze kuupokea”.
Watoto kuhisi mazingira wasiyo jua
Papa Francisko kama kawaida yake katika fursa kama hii akiendelea kuelezea kuhusu watoto amesema, sherehe hiyo ni ndefu kidogo japokuwa watoto wanajihisi kuwa katika mazingira wasiyo yajua. Kwa maana hiyo amebainisha kwamba wao ndiyo walio mstari wa mbele wa sherehe. Watafute namna ya kutowafanya wawe na joto sana, kwa kuwapunguza mavazi mengi waliyovaa, ili waweze kukaa vema na wakiwa na njaa wanyonyeshwe kwa utulivu hapo, mbele ya Bwana. Hakuna matatizo.
Kutunza utambulisho wa Kikristo
Na ikiwa wanapiga kelele waache wapige, kwa sababu wana roho ya jumuiya na kwamba "tunaweza kusema roho ya bendi, roho ya kuwa pamoja na inatosha tu aanze mtoto mmoja na wote wanaanza muziki na kutengeneza tamasha haraka". Papa amewaomba waache watoto walie kwa utulivu kwani wanahisi kuwa huru, lakini wasihisi joto sana na wala njaa. Na kwa amani hiyo ndiyo waendele mbele na maadhimisho bila kusahau kuwa watapokea utambulisho wa Kikristo na kazi yao ni ile ya kutunza utambulisho wa kikristo, amehitimisha.
Ubatizo kwa watoto wa wafanyazi ulianzishwa na Mtakatifu Yohnae Paulo II
Katika uzuri wa ubatizo watoto kumi na sita wadogo katika kikanisa cha Kipapa, kwa mikono ya Baba Mtakatifu, kuna Jina Maria ambalo limechukua nafsi kuu miongoni mwa watoto hao wa kike, kwa mfano, limesikika jina la Sofia Maria Leticia, Ludovica Maria, Vittoria Maria, Camilla Maria, Carlotta Maria na Caterina Maria. Utamaduni wa kubatiza watoto wa wafanyakazi wa mji mtakatifu ulianzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, mnamo tarehe 11 Januari 1981 na Misa iliongozwa katika Kikanisa cha Pauline katika Jumba la Kitume. Mwaka 1983 Papa Wojtyła (Yohane Paulo II) aliongoza kwa mara ya kwanza Misa yenye ibada ya ubatizo kwa baadhi ya watoto ndani ya kuta za Kikanisa cha Sistine. Misa Takatifu yenye ibada ya ubatizo imefunguliwa na maandamano kuelekea altareni. Baada ya salamu za mwanzo yalianza, mazungumzo na wazazi, na wasimamizi wao kike na kiume. Kisha ibada ya Ishara ya msalaba kwenye paji la uso wa watoto ilianza na baada ya utangulizi huo wa Baba Mtakatifu, kinanda kilipigwa kwa mlio wa chini chini. Wazazi, pamoja na watoto wao, wakamkaribia Papa ambaye, alikuwa amesimama na mitra yake na kuwaweka alama kwa kila mtoto kwa ishara ya msalaba.
Ishara mbali mbali wakati wa ubatizo
Ishara ya Papa ilifuatiwa na ishara sawa na wazazi wawili, kwanza mama na kisha baba. Masomo yalisomwa na baadhi ya waamini na kuhitimishwa na mahubiri ya Papa, lakini pia hata sala za waamini. Baada ya litania ya watakatifu, sala ya kutoa pepo na upako kabla ya ubatizo kuanza. Kinanda kilipigwa kwa mlio wa chini hadi Papa alipofika karibu na sehemu ya ubatizo. Wakati huo huo, maaskofu wawili walimsaidiza Papa walikaribia watoto kuwapaka mafuta. Baada ya Kukanushwa yaani kumkataa Shetani na kukiri Imani yao kwa Mungu muumba mbingu na dunia, Papa ali msalaba wa kichungaji mkononi mwake, wakati wazazi, pamoja na watoto, walikaribia mbele ya kisima cha Ubatizo. Kinanda kwa mlio wa chini chini kilindikiza ibada ya Ubatizo ambayo ni msingi wa maisha mapya ya Kikristo.
Baada ya Ubatizo, maaskofu wawili wanaomsaidia Papa, pamoja na mashemasi wawili, wamewapaka watoto mafuta ya Krisma. Baba Mtakatifu alitanguliza ibada ya Utoaji wa vazi jeupe na mshumaa uliowashwa. Kisha mababa wa watoto waliobatizwa walikwenda kuwasha mshumaa wao katika ule wa Pasaka. Kinanda kilisindikiza hadi mshumaa wa mwisho unawaka. Baada ya Ibada ya Effata, Misa Takatifu iliendelea kama kawaida. Makuhani wanaotoa Komunio wakati wa kuimba wimbo wa Mwanakondoo, walichukua pyxes kutoka altareni kwa kusindikizwa na mshereheshaji kwenda kwenye maeneo waliyooneshwa.