Tafuta

Papa:Neno linaibua mapya ya Mungu na kukupeleka kwa wengine bila kuchoka

Katika fursa ya maadhimisho ya Dominika ya III ya Neno la Mungu,23 Januari 2022,Papa ametoa Daraja dogo la Usomaji na huduma ya Katekista kwa waamini walei ikiwa ni kutimiza kile ambacho waamini wabatizwa wanapaswa kuliishi neno la Mungu kwa kushuhudia habari njema.Papa katika mahubiri:“Tuweke Neno la Mungu katikati hata Uchungaji na maisha ya Kanisa.Tulisikilize,tulisali na kuliweka katika matendo”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Januari 2021 ameongoza misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, katika Dominika ya III ya Neno la Mungu. Katika fursa hiyo  Baba Mtakatifu ametimiza kile alichokitangaza kwa Barua zake Binafsi “Motu Proprio”, “Spiritus Domini”, yaani “Roho wa Bwana” , kuhusu Utume wa Waamini Walei wabatizwa ” iiliyokuwa inaruhusa kutoa hata kwa wanawake kushiriki katika huduma ya usomaji na utumishi Altareni ambapo ametoa daraja dogo la usomaji (Msomaji, Lector) na utumishi Altareni (Akoliti, Acolyte) kwa baadhi ya waamini walei,  ikiwa ni pamoja kutimiza kile alichotoa katika Barua yake  binafsi ya “Motu Proprio”  ya “Antiquum ministerium” yaani “Huduma kale” ambayo ilikuwa inaanzisha Huduma ya Katekista kwa waamini walei , kwa hiyo wote wamepokea Injili kutoka mikononi mwa Baba Mtakatifu  na pia Msalaba kwa makatekista ili wote waweze  kuishi neno, kulitangaza neno na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu.

Ishara ya Esra na Yesu

Baba Mtakatifu akianza mahubiri yake amesema katika Somo la kwanza na Injili, tunakutana na mambo mawili yanayokwenda sambamba kuanzia na kuhani Esra ambaye anaweka kitabu cha sheria ya Mungu, alikifungua na kutangaza mbele ya watu wote;  Na Yesu katika Sinagogi ya Nazareth alifungua kitabu cha Andiko Takatifu na kusoma kifungu cha Isaya mbele ya wote. Ni matukio mawili ambayo yanatueleza hali halisi msingi. Kiini cha maisha ya watu watakatifu wa Mungu na safari ya imani, ambamo hatumo sisi, na nguvu ya maneno yetu badala yake  chanzo chake ni  Mungu na Neno lake! Yote yalikuwa na mwanzo wa Neno ambapo Mungu alituonesha. Katika Kristo, Neno lake la Milele, Baba alituchagua kabla ya uumbaji wa Mungu (Ef 1,4). Na kwa Neno lake aliumba ulimwengu. Yeye alizungumza na yote yakafanyika (Zab 33,9). Tangu nyakazi za kale, alizungumza nasi kwa njia ya manabii ( Eb 1,1); na mwisho katika utilifu wa nyakati ( Gala 4, 4) alimtumia  Neno lake yaani  Mwanae Mzawa wa kwanza. Baba Mtakatifu amesema  Yesu alipomaliza somo la Isaya, katika Injili alitangaza kitu ambacho hakikuwahi kusikika, na hicho ni  Leo hii ambayo imetimizwa Andiko hilo. (Lk 4,21). Limetimizwa Neno la Mungu, na  si tena ahadi, lakini limetimizwa kweli,  kwa njia ya Yesu aliyefanyika mwili. Kwa njia ya Roho Mtakatifu alikuja kukaa katikati nasi, ambaye anataka kujionesha ndani mwetu ili kutuliza matarajio yetu na kuponesha majeraha yetu. Baba Mtakatifu ameomba kukazia mtazamo kwa Yesu, kama watu wale wa Sinagogi ya Nazareth, walivyo kuwa  na mtazamo na yeye alikuwa mmoja wao; je ni mapya yapi? Je atafanya nini yanayo yozungumzwa sana? na kupokea Neno lake. Papa Francisko amesema ni kulitafakari leo hili kwa mantiki mbili zunazofungamana. Kwa maana ya Ahadi iliyooneshwa na Mungu na nyingine Neno ambalo linapeleka kwa Mtu. Ni kitovu; kinachoonesha Mungu na kutupeleka kwa binadamu.

MATUKIO YA MISA YA DOMINIKA YA NENO LA MUNGU

Mungu anajieleza ukaribu wake na kulia machozi na watu wake

Baba Mtakatifu kwa kufafanua juu ya  Neno liliooneshwa na Mungu amesema mwanzo wa Neno lake kwa kutafakari maana ya kifungu cha Isaya, anatangaza uchaguzi sahihi. Yeye “ alikuja kwa ajili ya kuwakomboa maskini na wanaokandamizwa. Na kwa njia ya Neno, linatuonesha uso wa Mungu kama wa Yule ambaye anatunza umaskini wetu na anazingatia hata hatima yetu. Huyo si Bwana aliyewekwa juu ya mbingu kusimamia lakini ni Baba ambaye anafuata nyayo zetu. Si mtazamaji wa ubaridi aliye mbali nasi  bali ni Mungu pamoja nasi  ambaye anapenda maisha yetu na kujihusisha  hadi kufikia kulia na machozi yetu. Si mungu hasiye na upendo, lakini yeye anachukua upendo kwa ajili yetu, kupiga magoti na kuteseka na uchungu wetu. Tazama hili ndilo tangazo la habari njema ambalo Yesu anatangaza mbele ya mtazamo na mshangao kwa wote. Mungu yupo karibu na anataka kunituma, kukutunza pia kwa wote,  Papa amesisitiza.  Hiyo ndiyo sura ya Mungu ya ukaribu,  Yeye mwenye anajieleza hivyo na anawambia watu katika kitabu cha Kutoka kuwa: “Ni nani aliye karibu nao kama jinsi nilivyo karibu yako! Kwa hiyo ni Mungu jirani. Kwa ukaribu huo wenye huruma na upole. Anataka kutuondolea mizigo ambayo inatubamizia; anataka kuwasha katika baridi zetu, anataka kutoa nuru katika siku zenye kiza, anataka kukusaidia katika hatua zako zisizo na uhakika. Na anafanya kwa njia ya Neno, kwa namna ambavyo anazungumza nao ili kuwasha kwa upya matumaini ya huzuni wako, kukujaza matumaini katika uchungu wa upweke wako. Anakufanya upende na si kama kuzunguka zunguka katika njia isyo na mahali pa kutokea, anakufanya uende katika mchakato wa safari ili kuweza kukutana naye zaidi kila siku.

Ni sura gani tunayotangaza Mungu katika Kanisa?

Baba Mtakatifu Francisko ameomba kujiuliza maswali: je ndani ya mioyo yetu tunachukua sura yenye ukombozi wa Mungu au tunawaza kama aliye mgumu, mwenye mipaka ya maisha yetu? Je Imani yetu ni ile inayozaa matumaini na furaha au bado imejazwa na hofu? Ni ni sura gani tunayotangaza Mungu katika Kanisa? Mwokozi anayetoa uhuru na kuponesha au wa kuogopwa ambaye anabamiza chini ya hisia za makosa?  Ili kuweza kumwongokea Mungu kweli, Yesu alituelekeza ni wapi tuanzie. Katika Neno lake.  Neno  linasimulia historia ya Upendo wa Mungu kwa ajili yetu,  linatupatia uhuru dhidi ya hofu na mantiki mbaya juu yake ambayo inazima furaha ya imani. Neno linapambana na miungu ya uongo, linaibua  sura ya uongo, na kuharibu uwakilishi wa kujifanya  Mungu kibinadamu na kutupeleka katika sura ya kweli na huruma yake. Neno la Mungu linamwilisha na kupyaisha imani. Kwa maana hiyo tuliweke katikati ya sala na maisha ya kiroho.

Neno linapeleka kwa Mungu

Mantiki ya pili ni Neno linapeleka kwa Mungu. Papa Francisko amesema, tunapogundua kuwa Mungu ni upendo wa huruma, tunashinda vishawishi vya kujifungia katika udini wa kitakatifu, ambao unakuwa ni ibada za kiju juu ambazo hazigusi na wala kubadili maisha. Neno linatusukuma kuingi a ndani mwetu ili kuanza kwa upya safari ya kukutana na Ndugu kwa nguvu pekee ya upole wa upendo unaookoa wa Mungu. Katika sinagogi ya Nazareth Yesu alituonesha hili: Yeye alitumwa kwenda kukutana na maskini, ambao ni sisi sote na kuwakomboa. Hatufundishi kuwa na  orodha na kanuni au sherehe rasmi za kidini, yeye alikwenda katika barabara za dunia ili kukutana na ubinadamu uliojeruhiwa kubembeleza sura zilizochimbwa na mateso, na kuponesha mioyo ya wenye mateso, kuvunja minyororo ambayo ilikuwa imewafunga roho. Kwa namna hiyo anatueleza ni ibada gani inayopendwa zaidi na Mungu, ile ya kumtumza jirani. Ni huzuni sana Papa Francisko amesema kusikia na kuona kaka na dada zetu wanakufa katika bahari kwa sababu hatutaki washuke na  hayo yote  wanayafanya na baadhi ya watu kwa jina la Mungu.

Neno la kweli linakutoa nje kukutana majeraha ya wengine

Kinyume chake Baba Mtakatifu amesema Neno la Mungu linatubadili. Linafanya hivyo kwa kupenyeza katika roho kama mshale ( Eb 4,12). Kwa sababu ikiwa kwa upande mmoja linafariji, kwa kuonesha uso wa Mungu, kwa upande mwingine linachochea na kukung’uta, katika vizingiti vyetu. Halituachi na utulivu, ikiwa tunalipa gharama ya utulivu huu, basi ni dunia iliyochanika na ukosefu wa haki, na wanaolipa gharama daima ni walio wanyonge zaidi. Neno linatuweka katika mgogoro wa kujihalalisha wenye haki ambao wanategemea kile ambacho daima hakiendi, kwa mmoja na wengine. Linatualika kujifunua wazi na siyo kujificha nyuma ya ugumu wa matatizo, nyuma ya kile kisemwacho hakuna cha kufanya au mimi ninaweza kufanya nini? Neno linatushauri kutenda, kuunganisha ibada ya Mungu na kutunza binadamu. Kwa sababu hatukupewa Andiko Takatifu kwa ajili ya kutunza sisi binafsi, kujibembeleza katika uroho wa kimalaika, badala yake kwa ajili ya kutoka nje kukutana na wengine na kukaribia majeraha ya wengine. Neno lililofanyika Mwili ( Yh 1,14) linataka kuwa mwili ndani mwetu. Halituondoi uzima, bali linatuweka katika uzima, katika hali za kila siku, kwa kusikiliza mateso ya ndugu, kilio cha maskini ,vurugu na ukosefu wa haki ambao unaikumba jamii na sayari, ili kutokuwa wakristo wasio jali bali wanaojibidisha, wabunifu na manabii.

Neno linakuwa mwili 'leo' hii na si kuishi kwa wazo

Yesu anesena Leo, limetimizwa andiko hili (Lk 4, 21). Neno linataka kuwa mwili leo hii, katika wakati ambao tunaishi, sio wakati ujao wenye wazo. Papa ametoa mfano kwamba mtu Mwenye ibada ya kina wa kifaransa wa karne iliyopita ambaye alichagua kuishi  Injili katika pembezoni, aliandika kuwa “Neno la Bwana sio barua iliyokufa, ni Roho na maisha(…)  sauti ambayo Neno la Bwana linahitajika kwetu ndiyo leo yetu: mambo ya maisha yetu ya kila siku na ulazima wa jirani”, (M. DELBRÊL, La gioia di credere, Gribaudi, Milano 1994, 258). Kwa kuongeza  Papa amesema, tujiulize kwa hiyo tunataka kumwiga Yesu, ili kugeuka kuwa wahudumu walio huru na faraja kwa wengine? Je sisi ni Kanisa lenye utamu wa Neno la Mungu? Kanisa moja ambalo liko kwa ajili ya kusikiliza wengine, lenye jitihada ya kutoa msaada kwa ajili ya kuwasaidia kaka na dada, kwa kile ambacho kinawakandamiza, kufungua vifundo vya hofu, kuwakomboa wadhaifu dhidi ya vifungo vya umaskini, vya uchovu wa ndani na huduma ambayo inazima maisha?

Neno linaibua mapya ya Mungu na kukupeleka kwa wengine bila kuchoka

Katika hitimisho la Papa Francisko amewageukia wale waliopata daraja dogo la kusoma neno la Mungu na Makatekista  na kusema: “Katika maadhisho ya baadhi ya kaka na dada ambao wamepewa daraja dogo la kusoma neno  na makatekista, wanaalikwa katika shughuli muhimu ya  kutoa huduma Injili ya Yesu, kuitangaza ili faraja yake, furaha yake, ukombozi wake uweze kuwafikia wote. Hii pia ni utume wa kila mmoja wetu wa kuwa watangazaji wanaoaminka, manabii wa Neno katika ulimwengu. Kwa maana hiyo kuwa na upendo mkuu wa Andiko Takatifu, kujiachia kuchomwa ndani na  Neno, ambalo linaibua mapya ya Mungu na kupelekea kupenda wengine bila kuchoka. Baba Mtakatifu amesisitiza “tuweke Neno la Mungu katikati hata Uchungaji na wa maisha ya Kanisa. Na kwa njia  hiyo tutaachiliwa huru dhidi ya tikadi kali ya Kipelagian, tutaondokana na  ugumu wowote, na tutaachiliwa huru dhidi ya  udanganyifu wa kiroho ambao unakufunga bila kutunza kaka na dada zako. Turudishe Neno la Mungu katika kitovu cha uchungaji na maisha ya Kanisa. Tulisikilize, tulisali na kuliweka kwenye matendo.”

MAHUBIRI YA PAPA DOMINIKA YA NENO LA MUNGU
23 January 2022, 14:51