Tafuta

Papa Francisko:Chukua Biblia mfukoni na Neno likubadilishe!

Mara baada ya maadhimisho ya asubuhi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Dominika ya Neno la Mungu,Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari na kuwawasalimia mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya Malaika wa Bwana na kuwashauri kusoma Injili kila siku ili kuvutiwa na kugeuzwa kwa upya na furaha ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika siku ya maadhimisho ya Dominika ya III ya Neno la Mungu, mara baada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa Francisko amefanya tafakari nyingine kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Dominika tarehe 23 Januari 2022. Papa Francisko akianza mahubiri amesema,  Injili ya liturujia ya siku tunamwona Yesu ambaye anazindua mahubiri yake (Lk 4,14-21) kwani yalikuwa ni mahubiri ya kwanza.  Alikwenda Nazareti mahali alipokulia na kushiriki katika sala kwenye Sinagogi. Alisimama na kupewa kitabu kusoma cha Nabii Isaya akatafuta mahali palipo andikwa habari za Masiha na kutangaza ujumbe wa faraja na uhuru kwa maskini na  walioteswa (Is 61, 1-2). Baada ya kumaliza kusoma watu wote waliokuwa katika Sinagogi wakamkazia macho. Na Yeye akaanza kuwaambia leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu!

Papa amependa kufafanua juu ya neno ‘Leo’.  Ni neno la kwanza la mahubiri ya Yesu ambalo limeoneshwa na Injili ya Luka. Lilitamkwa na Bwana akielekeza 'Leo' ambayo inapita kila kipindi na kubaki daima inafaa.Papa ameongeza kusema Neno la Mungu daima ni la leo hii. Linaanza na leo, wakati ukisoma Neno la Mungu katika roho yako linaanza na leo hii, hasa ukiwa unaelewa vizuri leo hii. Unabii wa Isaya ulitokea karne za kwanza, lakini Yesu kwa uwezo wa Roho,  linalifanya lile hasa kutimiza na kueleza namna ya kupokea Neno la Mungu. Si kama historia ya zamani. Hapana. Ni leo hii ambayo inazungumza katika moyo wako".

Wanakijiji wa Yesu walishangazwa sana na neno lake. Hata kama walikuwa na giza na walikuwa hawamwamini, walitambua kwa haraka kuwa mafundisho yake yalikuwa ni tofauti na walimu wengine, na kutambua kuwa katika Yesu kuna jambo kuu zaidi. Je kitu gani? Kuna upako wa Roho Mtakatifu. Wakati mwingine inatokea kuwa mahubiri yetu na mafundisho yetu yanabaki kwa ujumla, ya kijujuu, hayagusi roho na maisha ya watu. Kwa nini? Kwa sababu yanakosa nguvu ya leo hii, ambayo Yesu anajaza maana, kwa nguvu ya Roho. Leo hii,  Yesu anazungumza na wewe.

Papa Francisko amesema:“inasikika katika mikutano na hotuba zilizoundwa, ambazo lakini hazikung’uti moyo na yote yanabaki kama mwanzo”.  Na hata mahubiri mengi,  Papa amesema kwa kutamka na heshima, lakini kwa uchungu, kwamba yanakuwa mbali badala ya kuamsha nyoyo zilizo sinzia. Wakati waamini wanaanza kutazama saa na kujiuliza kuwa huyu mtu anamaliza saa ngapi, na wanaanza kulala”. Mahubiri yanakabiliwana hatari hiyo, bila kuwa na upako wa Roho, Neno la Mungu linakuwa maskini, linaangukia kwenye uroho na mantiki za juu juu; linakuwa Injili isiyo na mshiko kama vile iko nje ya wakati, mbali na uhalisia. Lakini neno ambalo halitoa nguvu ya leo hii halistahili kuwa la Yesu na halisaidii maisha ya watu. Kwa maana hiyo anayehubiri ni wa kwanza kushuhudia ‘leo hii ya Yesu’,   kwa namna ya kuweza kuwasilisha leo hii kwa wengine. Papa ameongeza kusema ikiwa unataka kufundisha, kufanya mkutano unaweza kufanya lakini ufanyie sehemu nyingine na siyo wakati wa mahubiri  yaani mahali pa kutoa Neno la Mungu ambalo linakung’uta mioyo.

Baba Mtakatifu Francisko amesema  katika Dominika ya Neno la Mungu anapendelea kuwashukuru wahubiri na watangazaji wa Neno la Mungu. Na kwamba wabaki waaminifu wa Neno ambalo linakung’uta mioyo na kubaki waamini wa leo hii. Ameomba kusali kwa ajili yao, kwa sababu waweze kuishi leo ya Yesu, utamu wa nguvu ya Roho yake ambayo inafanya Neno kuwa hai. Neno la Mungu kwa hakika ni hai (Eb 4,12), linatubadili, linaingia katika mambo yetu, linatuangazia kila siku yetu, linafariji na kuweka mambo kwenye mstari sawa. Tukumbuke: Neno linatubadilisha kwa siku ya kila siku ambayo Mungu anazungumza nasi

Papa ametoa ushauri kwamba ni bora kuchukua IBiblia mkononi kila siku na kusoma kwa utaratibu sehemu ya Injili. Kaadiri ya siku zinavyopita ndivyo tunagundua maneno yale yaliyofanywa kwa makusudi kwa ajili yetu, kwa ajili ya maisha yetu. Yatatusaidia kupokea kila siku kwa mtazamo uliobora, wa utulivu zaidi kwa sababu Injili inaingia katika leo hii, na Mungu anaijaza. Papa amependeleza katika dominika ya mwaka wa liturujia,  Injili ya Luka kwamba ni Injili ya huruma. Kwa sababu gani usisome binafsi, na yote hayo hatua kwa hatua ndogo kila siku?  Kuzoea na Injili itatupelekea mapya na furaha ya Mungu. Neno la Mungu ni taa pia linatuongoza katika mchakato wa Sinodi iliyoanzishwa kwa Kanisa zima. Wakati tunajitahidi, kusikilizana na umakini, na kufanya mang’amuzi, tusikilize pamoja Neno la Mungu na Roho Mtakatifu. Mama Maria atusaidie katika yote  na kutulisha kila siku Injili.

23 January 2022, 15:48