Papa Francisko:msiache uendelezwe ukatili mbaya sana usioelezeka!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu mara baada ya tafakari na salamu kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Ukumbi wa Paulo VI, Vatican, amekumbusha juu ya siku ya kumbu kumbu ya 77 kimataifa kwa ajili ya waathirika wa mauaji ya kimbari wa kiyahudi ifanyikayo kila ifikapo tarehe 27 Januari ya kila mwaka. Kufuatia na hilo Papa amesema ni lazima kukumbusha maangamizi ya milioni za wayahudi na watu tofauti wa mataifa na imani za kidini. Hali hii isirudiwe kamwe ya ukatili usiolelezeka. Ametoa wito kwa wote hasa walimu na familia ili waweze kukuza katika vizazi vipya utambuzi wa tishio baya sana katika ukurasa mweusi wa historia. Hiyo haipaswi kusahaulika ili kuweza kujena wakati ujao mahali ambapo hadhi ya binadamu haikanyagwi tena, amesisitiza.
Hii ni kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yalotekelezwa dhidi ya Wayahudi, yaani ‘Holocaust’, ambayo hufanyika kila mwaka kwa kufunguliwa kwa kambi ya mauaji ya kimbari ya Auschwitz- Birkenau na kumbukumbu kwa wahanga wa mauaji hayo. Tangu wakati huo imebaki alama ya mauaji ya kimbari yaliyokatiza maisha ya binadamu. Pia mwaka jana, akikumbuka kwenye sala ya Malaika wa Bwana kuhusu mkasa huo Papa alisema: “Kutojali haukubaliki na kumbukumbu ni wajibu” na aliwaalika waamini kusali kila mtu moyoni mwake ili janga hili lisitkee tena.
Kwa hakika kamwe isitokee ingawa ilinyamazishwa kwa kupendelea ukimya wa ufasaha zaidi kuliko kila sentensi au hotuba, na ishara mbali mbali zilizotolewa na Papa hasa wakati wa hija yake ya maumivu kwenye kambi la Auschwitz-Birkenau, mnamo 2016 kwenda Poland. Katika sala mbele ya ukuta wa kunyongwa na mahali ambapo Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe alikaa dakika za mwisho wa maisha yake, kati ya kukumbatiwa na walionusurika na kutembea akiwa ameinamisha kichwa chake. Papa hakusema neno kutoka kinywani mwake bali ni sala moja tu ilikuwa katika nafsi ya Papa, ile ile aliyoiacha ameandika kwa Kihispania kwenye Kitabu cha Heshima cha kambi ya maangamizi:
“Señor ten piedad de tu pueblo. Señor, perdón por tanta crueldad!, "Yaani Vwaba uhurumie watu wako. Bwana hurumia kwa ukatili mwingi!"