Tafuta

Papa Francisko:Kamwe usimhukumu mtoto na wazazi msiogope!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake katika Ukumbi wa Paulo VI,Vatican,ameendeleza mada ya sura ya Mtakatifu Yosefu kusu kusikiliza Mungu kwa njia ya ndoto na kufafanua hatua za nne za ndoto zilizoelezwa katika Injili kuhusu Yosefu.Amewaalika wazazi wafanye kama alivyo fanya Mtakatifu huyo kwa namna ya pkee kukabiliana na matatizo.Bwana haruhusu kamwe matatizo bila kutoa msaada wa lazima wa kukabiliana nayo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Katekesi yake, Jumatano tarehe 26 Januari 2022, kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, ameendelea kutazama sura ya Mtakatifu Yosefu kama mwanaume ambaye anaota ndoto. Katika Biblia na kama ilivyo katika tamaduni za watu wa kale, Baba Mtakatifu anasema ndoto zilikuwa zinafikiriwa kama zana ambayo Mungu alikuwa anajionesha. Ndoto ni alama ya maisha ya kiroho ya kila mmoja wetu kwa ile nafasi ya undani, ambayo kila mmoja anaitwa kuikuza na kuilinda, mahali ambapo Mungu anajionesha na mara nyingi anazungumza. Lakini Papa amebainisha kwamba lazima kusema kuwa hata ndani ya kila mmoja hakuna sauti moja tu ya Mungu, kwa maana kuna sauti nyingi. Kwa mfano, sauti za hofu zetu, sauti za uzoefu uliopita, sauti za matumaini; na kuna hata sauti mbaya ambazo zinatudanganya na kutuchanganya.

Katekesi ya Papa:Ndoto kwa  Yosefu
Katekesi ya Papa:Ndoto kwa Yosefu

Ni muhimu kwa maana hiyo kuzijua ili kung’amuu sauti ya Mungu katikati ya sauti nyingi.  Yosefu, anajionesha kujua namna kukuza ukimya wa lazima na hasa kujua namna ya kuchukua maamuzi sahihi mbele ya Neno ambalo Bwana alimwambia kiundani. Baba Mtakatifu ameshauri kwamba itakuwa vizuri leo hii kuzitazama ndoto nne zilizotlewa  katika Injili na ambazo ziko mstari wa mbele, ili kujua jinsi gani ya kujiweka mbele ya maonesho ya Mungu. Injili zinasimulia ndoto nne za Yosefu. Ndoto ya kwanza (Mt 1,18-25), ni kwamba Malaka anamsaidia Yosefu kutatua suala zito ambalo linamgusa mara baada ya kujua Maria kubeba mimba na akamwambia: “usihofu kumchukua Maria mchumba wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao”.Mt 1,20-21).

Na jibu la haraka: "Naye alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; (Mt 1, 24)". Papa Francisko ameongeza kusema kwamba mara nyingi maisha yanatuweka katika hali ambazo hatuzielewi na utafikiri hazina suluhisho. Kitu muhimu wakati huo ni kusali . Hii ina maana ya kuacha Bwana ajenge kile kinachofaa. Kwa hakika mara nyingi ni sala ambazo zinafanya kuzaa ndani mwetu ile njia ya kupitia, na namna ya kupata suluhisho la hali kama hiyo. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa: “Bwana haruhusu kamwe matatizo bila kutupatia msaada wa lazima wa kukabiliana nayo. Hatutupi pale peke yetu katika tanuru la moto. Hatutupi katikati  ya wanyama. Hapana! Bwana anapotufanya tuone matatizo au kutuonesha tatizo hayo, Yeye  anatupatia daima njia, msaada na uwepo wake ili kuweza kuondokana nao katika kupata suluhisho”.

Katekesi ya Papa:ndoto kwa Yosefu
Katekesi ya Papa:ndoto kwa Yosefu

Na ndoto ya pili iliyooneshwa kwa Yosefu, ni pale ambapo maisha ya mtoto yalikuwa hatarini. Papa amesema ujumbe huko wazi: “Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.(Mt 2,13). Injili Inasema kuwa Yosefu bila kusita, alitiii  kwani: “Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; akakaa huko hata alipokufa Herode”(Mt 2, 14-15). Baba Mtakatifu Francisko amesema,  katika maisha sisi sote tunafanya uzoefu wa hatari zinazotishia uwepo wetu au wa wale tunaowapenda. Katika hali kama hizo, kusali ina maana ya kusikiliza sauti ambayo inaweza kuzaliwa ndani mwetu ujasiri kama wa Yosefu, ili kukabiliana na shida bila kumezwa nazo. Huko Misri, Yosefu alisubiri kutoka kwa Mungu ishara ya kuweza kurudi nyumbani; na ndiyo hiyo ndoto ya tatu, Papa amekazia. 

Malaika alimwonesha kuwa wamekufa wale waliokuwa wanaitafuta roho ya mtotona kuwaamuru waondoke na Maria na Yesu kurudi kwao, (Mt 2,19-20). Na Injili inasema: “Yosefu akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli" (Mt 2, 21). Lakini wakati wa safari ya kurudi, aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya na tazama ambapo alienda akakaa katika mji ulioitwa Nazareti ( Mt 2, 22 -23) na ndiyo ndoto ya nne. Hata hofu ni sehemu ya maisha, na hata hiyo inahitaji sala zetu. Mungu hatupi ahadi kwamba hatutakuwa na hofu, lakini kuwa kwa msada wake huo hautakuwa mantiki ya maamuzi yetu. Yosefu alijaribiwa na woga, Mungu akamwongoza kwa njia ya woga huo. Nuvu za sala zinafanya kuingiza mwaka katika hali za kiza.

Katekesi ya Papa:Ndoto kwa  Yosefu
Katekesi ya Papa:Ndoto kwa Yosefu

Papa Francisko kutokana na hilo amefikiria watu wengi ambao wamebamizwa na uzito wa maisha na hawawezi tena na wala kutumaini, hata kusali. Ameomba ili Mtakatifu Yosefu aweze kuwasaidie na kuwafungulia mazungumzo na Mungu,  ili wapate mwanga, nguvu na amani. Papa pia amefikiria wazazi mbele ya matatizo ya watoto. "Watoto na magonjwa wengi,  hata kwa magonjwa ya kudumu. Kuna maumivu kiasi gani. Wazazi ambao wanaona mwelekeo tofauti wa kijinsia wa watoto wao; jinsi gani ya kusimamia hili na kuwasindikiza watoto na si kujificha katika tabia ya kulaani. Wazazi wanaoona watoto wao wanakufa kwaugonjwa  pia, inasikitisha zaidi, kwani tunasoma kila siku kwenye magazeti, juu ya  vijana wa kiume na  wakike wadogo ambao wanafanya michezo mibaya na kuishia kwenye ajali za gari. Wazazi wanaoona watoto wao ambao hawaendi shule na hawajui jinsi ya kufanya...".

Papa Francisko akiendelea amesisitiza kuwa yapo matatizo mengi ya wazazi. "Hebu fikirie juu yao na jinsi ya kuwasaidia". Na kwa wazazi hawa amesema: "Msiogope. Ndiyo, kuna maumivu mengi. Lakini mfikirie Bwana, fikiria jinsi Yosefu alivyotatua matatizo na kumwomba Yosefu awasaidie".  Papa ametoa ushauri  kuwa: “Kamwe usimhukumu mtoto”  kwa kutoa mfano kwamba yeye mara nyingi amekuwa mpole sana na huruma  wakati alipokuwa Buenos Aires,hasa wakati  anasafiri kwenye busi na kupitia mbele ya gereza. Kulikuwa na foleni ya watu ambao walipaswa kuingia kuwatembelea wafungwa. Na hao walikuwa ni akina mama. "Na niliwaonea sana huruma mbele ya matatizo ya mtoto ambao wamekosa na wamefungwa, lakini hawawachi peke yao, wanaona  nyuso zao na kuwasindikiza . Huo ndiyo ujasiri, wa baba na mama ambao wanasindikiza watoto wao daima". Baba Mtakatifu Francisko ameomba tusali kwa Bwana kwa ajili ya baba na mama wote ili awape ujasiri huu kama alivyompatia  Yosefu. Na kuomba, Bwana ili atusaidie katika nyakati hizi. Hata hivyo, maombi kamwe si ishara ya kudhahania au ya undani undani, kamawafanyavyo baadhi ya harakati za kiroho za Kikristo zinazoibuka. Hapana, sivyo! Maombi daima yanaunganishwa bila kutenganishwa na upendo wa kweli.

Katekesi ya Papa:Ndoto kwa  Yosefu
Katekesi ya Papa:Ndoto kwa Yosefu

Ni wakati tunapounganisha upendo tu katika maombi, upendo kwa watoto katika kesi ambazp Papa Francisko amezibainisha au upendo kwa jirani ndipo tunaweza kuelewa ujumbe wa Bwana. Yosefu aliomba, alifanya kazi na kupenda, mambo matatu mazuri ambayo yanaweza kufanywa na wazazi na kwa sababu hiyo alipokea kila mara kile kilichohitajika ili kukabiliana na majaribu ya maisha. Papa kwa kuhitimisha amesema" tujikabidhi kwake na maombezi yake: Mtakatifu Yoseph, wewe ndiye mtu anayeota, utufundishe kurejesha maisha ya kiroho kama mahali pa undani ambapo Mungu hujidhihirisha na kutuokoa. Usituondolee kamwe wazo kwamba kuomba ni bure; bali inasaidia kila mmoja wetu kuendana na kile ambacho Bwana anatuonesha.Mawazo yetu yaangaziwa na nuru ya Roho, mioyo yetu itiwe  nguvu zake na hofu zetu zimeokolewa kwa huruma zake. Amina.

KATEKESI PAPA 26 JANUARI 2022
26 January 2022, 12:57