Tafuta

2022.01.13 Papa amekutana na Wawakilishi wa Harakati ya Matendo Katoliki nchini Ufaransa 2022.01.13 Papa amekutana na Wawakilishi wa Harakati ya Matendo Katoliki nchini Ufaransa 

Papa Francisko:Harakati ya Matendo Katoliki iwafikie vijana mahali walipo

Papa Francisko akikutana wajumbe wa Chama cha vijana Wakatoliki kutoka Ufaransa amefafanua umuhimu wa kutumia njia ya kuona,kuhukumu na kutenda kwa kuacha waongozwe na Injili na kukubali kubadilishwa ubinadamu wetu na Umungu wa Kristo Msulibiwa.Amewaomba wawafikie vijana walipo kwa kuwasaidia wawe mstari wa mbele wa maisha yao na ya Kanisa. Vijana wakikua kwa upendo wa Kristo ulimwengu utabadilika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 11 hadi 16 Januari 2022 viongozi arobaini wa Harakati  Chama cha  Matendo ya Kikatoliki nchini Ufaransa,kwa maana nyingine Chama cha Vijana Katoliki, wako Mjini Vatican katika hija yao ambapo  tarehe 13 Januari 2022 wamekutana na Papa Francisko, na watakutana na Katibu wa Vatican pia na viongozi wakuu wa baadhi ya Mabaraza ya Kipapa. Katika hija yao wamewasilisha Hati yenye kauli mbiu: “Kuwa mitume leo”, ambayo ni tunda la kazi ya miaka miwili. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake amewasalimu wote na kumshukuru Askofu Fonlupt, msimamizi wa Chama hicho kwa maneno yake. Amefurahi kukutana nao katika fursa ya hija yao Roma na kwa niaba ya uongozi huo  amewatumia  wajumbe wote wa Chama cha Vijana Katoliki nchini Ufaransa akiwaomba wawahakikishie  kuwa anawakumbuka katika  sala zake na ukaribu wake. Papa Francisko amebainisha kwamba ni utamaduni wa kizamani wa harakati yao kuja roma kukutana na Papa. Tayari mnamo 1929, Papa Pio XI alikuwa amekutana na wawakilishi wa Chama cha Matendo ya Kitume na alikuwa amewasalimia na kupyaisha na uendelezwaji wa kile ambacho wakristo wa kwanza, walikuwa wakitangaza Ufalme wa Mungu na katika ushirikiano walei na Mitume (12 Juni 1929).

Mada ya hija: “Mitume wa leo”: Kuona, kuhukumu na  kutenda

Amewashukuru kwa kuchagua mada ya hija yao isemayo ‘Mitume wa leo’. Kwa kuongozwa na hiyo amepata kutafakari na wao juu ya wito wa kuwa mitume wa leo kuanzia na kile walichoachiwa na sura ya mwaharakati  mkubwa  wa Matendo ya Kikatoliki ‘abbé Cardijn,’ yaani, “marekebisho ya maisha”. Wanafunzi waliotembea pamoja na Yesu njiani kuelekea Emau (rej. Lk 24:18-35), walianza kwa kukumbuka matukio waliyopitia; baadaye wakatambua uwepo wa Mungu katika matukio hayo na hatimaye, walitenda kwa kurudi Yerusalemu kutangaza ufufuko wa Kristo. Kuona kuhukumu na kutenda ni mambo ambayo  wao wanajua maneno haya matatu vizuri! Papa amesisitiza.  Papa Francisko amependelea kuyafafanua maneno hayo akianza na ‘kuona’. Hatua hii ya kwanza ni ya msingi ambayo inajumuisha kutazama matukio yanayounda maisha yetu, kile kinachojumuisha historia yetu, familia zetu, tamaduni na mizizi ya Kikristo. Ufundishaji wa Chama cha Matendo Kikatoliki daima huanza na wakati wa kumbukumbu, kwa maana ya nguvu zaidi ya neon la “ anamnesis”, yaani, kuelewa kwa mtazamo wa mbali kwa maana ya kile ambacho  mtu anacho na kile ambacho ameishi na kutambua jinsi alivyo sasa kila wakati. Ujanja na umaridadi wa utendaji wa Bwana katika maisha yetu wakati mwingine hutuzuia sisi kuuelewa kwa kitambo tu, na inachukua muda mrefu kufahamu uthabiti wake Papa Francisko amefafanua. Waraka wa Fratelli tutti yaani, Wote, Ndugu ambao vikundi vyao vimejifunza, unaanza kwa kuangalia hali ya wakati ambayo kwa hakika inatia wasiwasi wa ulimwengu wetu. Na inaweza kuonekana kuwa ni ya kukatisha tamaa, lakini ni muhimu kusonga mbele kwani bila kumbukumbu, hakuna kukua na kuwa na kumbu kumbu fungamani na mwangaza (Ft 249).

Kuhukumu ni wakati ambao tunajiruhusu kujiuliza

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa “Hatua ya pili nikuhukumu au, mtu anaweza kusema, kupambanua. Ni wakati ambao tunajiruhusu kujiuliza, kujiweka kwenye mjadala”. Ufunguo wa hatua hii ni kumbukumbu ya Maandiko Matakatifu. Ni suala la kukubali kwamba maisha ya mtu yamepitishwa kwa uchunguzi wa Neno la Mungu, ambalo, kama Waraka kwa Waebrania unavyosema, “Neno la Bwana li hai, lina nguvu, lina makali kuliko upanga wowote ukatao kuwili; […] linatambua hisia na mawazo ya moyo” (Heb 4:12). Katika Waraka wa Wote ni ndugu, Papa amesema alichagua mfano wa Msamaria Mwema ili kujihoji kuhusu uhusiano wetu na ulimwengu na wengine hasa maskini zaidi. Katika mpambano kati ya matukio ya ulimwengu na maisha yetu, kwa upande mmoja, na Neno la Mungu, kwa upande mwingine, tunaweza kutambua swali ambalo Bwana anatuuliza.

Sinodi inaongozwa na Roho Mtakatifu anayeoneshwa katika Neno la Mungu

Papa amesisitiza kuwa Chama chao cha Matendo Katoliki kimehamasisha katika historia yao, mazoezi ya kweli ya sinodi, hasa katika maisha ya kikundi, ambayo huunda msingi wa uzoefu wao. Kanisa kwa ujumla nalo limeanza mchakato wa Sinodi, na Papa amesema kuwa anawategemea mchango wao. “Tukumbuke, katika suala hili, kwamba sinodi sio mjadala rahisi, na sio kivumishi, eh? Sinodi sio hata kutafuta maridhiano ya walio wengi, hii inafanywa katika bunge, na kama ifanyikavyo na wanasiasa. Sio mpango, katika utekelezaji”. Badala yake sinodi ni mtindo wa kudhaniwa, ambamo mhusika mkuu ni Roho Mtakatifu, ambaye anaoneshwa zaidi ya yote katika Neno la Mungu, kusomwa, kutafakariwa na kushirikishwa pamoja. Kwa maana hiyo amewaomba wachukue picha halisi ya Msalaba ambayo “ina mkono wima na mkono wa usawa. Mkono wa usawa ni maisha yetu, historia yetu, na ubinadamu wetu. Mkono ulio wima ni Bwana anayekuja kututembelea kwa Neno lake na Roho wake, ili kutoa maana kwa kile tunachoishi. Kwa kuwekwa juu ya msalaba wa Yesu, kama vile Mtakatifu Paulo anavyosema (taz. Gal 2:19), kiukweli ina maana ya kukubali kuweka maisha yetu maskini chini ya umungu wake unaobadilisha”. Baba Mtakatifu ameomba kila wakati waache nafasi muhimu kwa ajili ya Neno la Mungu katika maisha ya vikundi vyao. Na pia kutoa nafasi kwa ajili ya maombi, mambo ya ndani, na katika  kuabudu.

Hatua ya tatu ni kujikita katika matendo na ishara na kuwafikia vijana walipo

Papa Francisko akifafanua hatua ya tatu ya chama chao  linapaswa kuwa na hatua ya Mungu daima. Baada ya ufufuko, Mtakatifu Marko anasema kwamba: “Bwana alitenda pamoja na Mitume]na kulithibitisha Neno kwa ishara zilizoambatana na nalo” (16:20). Kwa maana hiyo, “matendo ni ya Bwana, kwani ni Yeye aliye na haki ya kipekee ya kutembea kwa siri katika historia tunayoishi” (Rej Hotuba kwa Chama cha Matendo Katoliki cha Italia, 30 Aprili 2021). Kwa maana hiyo jukumu letu ni kuunga mkono na kuhamasisha tendo la Mungu mioyoni, kuzoea hali halisi inayoendelea kubadilika. Watu ambao kutokana na tabia yao imewawezesha kufika ni vijana na ambapo Papa Francisko amewafikiria hasa vijana ambao  sio sawa na vijana wa miaka michache iliyopita. “Leo, hii hasa katika Ulaya, wale ambao mara kwa mara wanafika katika harakati za Kikristo zaidi wanafikia na mashaka, ambapo wao wanafika kwa madai ya chini na zaidi kuwa na mahusiano ya kijujuu.

Vijana wa kizazi cha leo ni nyeti na wadhaifu katika imani kuliko vizazi vilivyotangulia

Vijana ni nyeti zaidi na kuathirika, kwa njia hiyo  ni hatari zaidi, kwa maana ni wadhaifu zaidi kuliko vizazi vilivyotangulia, katika  mizizi ya imani, lakini hata hivyo katika kutafuta maana, ukweli, ambao hawakosi ukarimu” Papa Francisko ameongeza huo ni utume kama  Chama cha Matendo katoliki kwenda kuwafikia mahai walipo na  kuwafikia jinsi walivyo, ili kuwafanya wakue katika upendo wa Kristo na jirani na kuwaongoza katika kujitolea thabiti zaidi, ili wawe ni wahusika wakuu wa maisha yao na  maisha ya Kanisa, kusudi  ulimwengu uweze kubadilika. Papa Francisko kwa kuhitimisha ameshukuru marafiki wapendwa, kwa dhati kwa ajili ya huduma yao ya ukarimu, ambayo Kanisa linahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote, katika wakati huu ambapo anatumaini sana kwamba kila mtu atapata au kugundua tena furaha ya kujua urafiki wa Kristo na ya kutangaza Injili. Amewaomba wamsindikize katika sala zalo na kuwakabishi viongozi hao pamoja na washiriki wote wa timu zao kwa maombezi ya Bikira Maria, na amewabariki kwa baraka takatifu ya kitum.

13 January 2022, 17:59