Papa Francisko:Nchi ya Ukraine nchi inastahili kuwa na amani!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Jumatano tarehe 26 Januari 2022 ni siku ya maombi ya amani kwa ajili ya nchi Ukraine kama vile Papa alivyoomba wakati wa kumaliza Sala ya Malaika wa Bwana siku ya Dominika iliyopita, kwa maana hiypo mara baada ya kuhitimisha Katekesi yake, amerudia wito wake kwamba “Tunamwombe Mungu kwa msisitizo kwamba ardhi iweze kuona udugu ukishamiri na kushinda majeraha, hofu na migawanyiko" Akikumbuka mateso ya watu wa Ukraine yanayohusiana na Vita vya Pili vya Dunia, Baba Mtakatifu amekumbuka kwamba zaidi ya watu milioni tano waliangamizwa wakati wa vita na kwamba “Ni watu ni wato wanaoteseka ambao wanaostahili amani.
"Sala na maombi ambayo leo zinainuliwa mbinguni zguse akili na mioyo ya wale wanaohusika hapa duniani, ili kufanya mazungumzo na kuweza kutawala kwa ajili ya mema ya wote ambayo yawekwe mbele ya maslahi ya wote". Papa ameongeza kusema kwamba: “Tuombe amani na Sala ya Baba yetu ambayo ni sala ya watoto wanaomgeukia Baba yule yule: ni sala inayotufanya kuwa ndugu; ni sala ya ndugu wanaoomba upatanisho na maelewano".
Ili kujibu wito uliotolewa na Papa Francisko, mikutano ya maombi ya amani kwa ajili ya nchi Ukraine imepangwa katika nchi mbalimbali katika makanisa na parokia. Nchini Italia, hasa, mipango mingi imepangwa. Kwa mfano Roma, katika Kanisa la Mtakatifu Maria huko TrastevereJumuiya ya Mtakatifu Egidio itaendeleza sala maalum ambayo itaongozwa na Askofu Mkuu Paul Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa.
Vile vile Roma katika masifu ya jioni katika Kanisa la Mtakatifu Sofia la jumuiya ya Kiukraine, ambayo itahudhuriwa na Askofu Benoni Ambarus, mkurugenzi wa Ofisi ya Wahamiaji ya Jimbo, Monsinyo Pierpaolo Felicolo na Mkuu wa Kanisa Kuu na Padre Marco Jaroslav Semehen. Kwa kuhamasisha na Ofisi ya Wahamiaji ya Jimbo, mkesha huo utaona ushiriki wa mapadre na wawakilishi wa jumuiya za makabila mbalimbali. Huko Bologna, askofu mkuu, Kardinali Matteo Zuppi, taaongoza salakatika Kanisa Kuu la Watakatifu Bartolomeo na Gaetano Jumatano 26 Januari.