Tafuta

Papa Francisko ameonesha masikitiko makubwa kutokana na maafa yaliyosababishwa na mlipuko wa volkano na wimbi kubwa la tsunami ya Tonga tarehe 15 Januari 2022. Papa Francisko ameonesha masikitiko makubwa kutokana na maafa yaliyosababishwa na mlipuko wa volkano na wimbi kubwa la tsunami ya Tonga tarehe 15 Januari 2022. 

Mshikamano wa Papa Francisko Kwa Watu wa Kisiwa cha Tonga!

Papa Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye kwa sala na sadaka kwa ajili ya watu wa Mungu kwenye Kisiwa cha Hunga Tonga Hunga Ha'apai, ambao wameathirika kutokana na mlipuko wa Volkano na wimbi kubwa la “Tsunami ya Tonga” lililotokea tarehe 15 Januari 2022 na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake kuhusu Mtakatifu Yosefu Baba Mwenye Huruma, Jumatano tarehe 19 Januari 2022, amewaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye kwa sala na sadaka kwa ajili ya watu wa Mungu kwenye Kisiwa cha Hunga Tonga Hunga Ha'apai, ambao wameathirika kutokana na mlipuko wa Volkano na wimbi kubwa la “Tsunami ya Tonga” lililotokea tarehe 15 Januari 2022 na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo wake wa karibu kwa watu wote wa Mungu walioguswa na kutikiswa na maafa haya makubwa katika maisha yao.

Taarifa zinabainisha kwamba, zaidi ya watu watatu wamekwisha kufariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani mahali walipo. Watu 90 wameokolewa na kupewa hifadhi kwenye maeneo salama. Umoja wa Mataifa unasema, mlipuko huu wa Volkano ulikuwa mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha takribani miaka thelathini iliyopita. Wingu kubwa la moshi wa majivu lenye urefu wa kilomita 20, lilifuatiwa na tsunami, na mlipuko huo ulisikika hadi Australia na New Zealand, na kusababisha maonyo ya Tsunami katika ukanda wa bahari ya Pacifiki. Kwa sasa nchi kadhaa zimeanza kupeleka msaada wa kiutu kwa watu walioathirika kwenye Kisiwa cha Tonga.

Papa Tonga
19 January 2022, 15:48