Tafuta

2021.12.15 Papa akutana na Waandaaji na Wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana 2021.12.15 Papa akutana na Waandaaji na Wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana 

Papa Francisko:sanaa inaunda udugu na maelewano hakuna adui

“Janga kwa bahati mbaya limezidisha utofauti wa kielimu kwa mamilioni ya watoto na vijana waliobaguliwa kwa kila shughuli za mafunzo.Kuna hata majanga mengine ambayo yanazuia kueneza utamaduni wa mazungumzo na ujumuishwaji”.Papa amesema hayo kwa wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana ambapo fedha zitakazo patikana watasaidia nchi ya Haiti na Lebanon.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kama ilivyo kila mwaka katika siku kuu za kuzaliwa kwa Bwana, litafanyika Tamasha kwa ajili ya mshikamano Alhamisi tarehe 16 Desemba,  na kwa maana hiyo Papa Francisko, Jumatano tarehe 15 Desemba 2021 kabla ya Katekesi yake katika Ukumbi mdogo wa Paulo VI, amewasalimia na kuzungumza na Wasanii ambao watafanya Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana 2021 na kuwashukuru kwa msaada ambao kutokana na tamasha hilo fedha zitakazo patikana zitaweza  kusaidia mipango ya kielimu nchini Haiti na Lebanon. Papa Francisko “Ningemwomba Kardinali Versaldi maneno haya yasisambazwe kwenye tamasha: tamasha ni sanaa, hii haina uhusiano wowote; hiyo sanaa inajieleza yenyewe. Ninafuraha kuweza kuwasalimu kabla ya Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana, Asante, asante sana.” Kuzaliwa kwa Bwana kunatualika kukazia mtazamo juu ya tukio ambalo lilipelekea ulimwengu wa uhuruma ya Mungu na kwa maana hiyo liliibua na kuendelea kuibua furaha na matumaini. Huruma, furaha na matumaini. Hisia na tabia ambazo hata wasanii wanajua kuuisha na kutenda kwa talanta zao.

Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana
Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana

Papa akianza kufafanua  amesema huruma inazaliwa na upendo, ni kama lugha ya upendo. Ikiwa wewe unapenda mtoto, unambembeleza, ukiwa unampenda mchumba wako, unambembeleza. Ndivyo inavyozaliwa. Ishara ya Upendo ni iliyo rahisi zaidi. Katika Pango tunaona upendo wa mama anayemkumbatia mtoto mchanga aliyezaliwa, upendo wa baba ambaye anamlinda, na kuitunza familia yake; tunaona wachungaji ambao wanashangaa mbele ya kitoto kichanga; malaika ambao wanafanya siku kuu ya kuja kwa Bwana… Kila kitu kina maana ya mshangao na upendo ambao unaleta huruma. Papa amependelea kurudia kwamba “Lugha ya Mungu ni ukaribu, huruma na upole, ni mambo matatu pamoja, Papa amekazia. Mtakatifu Francis wa Assisi kwa kutengeneza pango lake hai huko Greccio, alitaka kuwakilisha kile kilichokuwa kimetokea katika Groto ya Bethlehemu, ili aweze kutafakari na kuabudu. Maskini alikuwa amejaa huruma sana ambayo ilimpelekea kuwa na hisia kali akifikiria umaskini wa mahali alipozaliwa mwana wa Mungu. Ni upendo huo huo ambao unaonesha tamasha kama hilo la furaha, amesisitiza Papa kwa wasanii hao wa Tamasha. Kuchanua kwa maisha daima ni sababu ya furaha ambayo inasaida kushinda mateso. Tabasamu la mtoto linayeyusha mioyo iliyo migumu zaidi. “Tumeaona, baadhi ya watu flani wagumu ambao hawasalimii yoyote, lakini anapozaliwa mjukuu wanafunguka”.

Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana
Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana

Katika Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana wao kama wasanii wanatoa ubora wa kisanii ili kuweza kusaidia mipango ya kielimu, kwa ajili hasa ya watoto na vijana wa nchi mbili ambazo zinaishi katika hali ngumu sana, Papa amezitaja nchi hizo kuwa ni Haiti na Lebanon. Huko Lebanon wanapeleka mbele wasalesiani, kwa ujasiri ambao daima wanabuni chochote ili maisha ayaende mbele. Hiyo ndiyo uhamasishaji wa maisha. Wakati huko Haiti wanajikita mbele Scholas Occurentes, harakati moja ya kipapa mabyao inaongozwa vizuri na Monsinyo Zani”.  Kwa njia ya muziki wao na nyimbo zao, zinasaidia kufungua mioyo ili wasiweze kusahau anayeteseka na kufanya ishara za dhati za kushirikishana na ambazo zinawapa furaha familia nyingi zenye kuhitaji kwa kuwawezesha wawe na wakati ujao wa watoto wao kwa jia ya elimu.

Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana
Papa akutana na waandaaji na wasanii wa Tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana

Papa Francisko akiendelea na mada hiyo ya huruma, furaha na matumaini, amesema katika Grotto ya Bethlehemu matumaini yalishuka kwa ubinadamu. Janga kwa bahati mbaya limezidisha utofauti wa kielimu kwa mamilioni ya watoto na vijana waliobaguliwa kwa kila shughuli za mafunzo. Na kuna hata majanga mengine ambayo yanazuia kueneza utamaduni wa mazungumzo na ujumuishwaji. Leo hii amebainisha kwamba kwa bahati mbaya unatawala utamaduni wa kibaguzi. Nuru ya Kuzaliwa kwa Bwana, inatufanya kugundua maana ya udugu na kutusukuma katika mshikamano na yule mwenye kuhitaji. Na wao katika sanaa kwa haraka wanaunda udugu; mbele ya sanaa hakuna marafiki na maaduo kwa maana wote ni sawa, marafiki wote na wote ni ndugu. Ni lugha yenye matunda ya ya kazi yao.  Kuwekeza katika elimu maana yake ni kufanya kugundua na kupongeza thamani muhimu zaidi na kusaidia watoto na vijana kuwa wajasiri wa kutazama kwa matumaini wakati wao ujao. Katika Elimu inaishi mbegu ya matumaini; tumaini la amani na tumaini la hakika, tumaini la uzuri, tumaini  la wema ; tumaini la maelewano kijamii. Kwa kuhitimisha, Papa ameshukuru sana tena sana kwa ukarimu ambao wanasaidia mipango hiyo kati ya kizazi cha vijana. Amewatakia wawe daima wajenzi wa uhuruma wa furaha na matumaini

15 December 2021, 15:23