Tafuta

2021.12.18 Papa akutana na wawakilishi wa Chama matendo ya Vijana Katoliki Italia 2021.12.18 Papa akutana na wawakilishi wa Chama matendo ya Vijana Katoliki Italia  

Papa kwa Chama Katoliki cha Vijana Italia:ujasiri na ukaribu kwa wenye shida

Papa amekutana na Chama cha matendo ya Vijana Katoliki Italiana kuhimiza juu ya kauli mbiu ya mwaka huu kwame wavae mavazi yaliyoundwa kulingana nao na kuthaminisha upekee wao. Amekumbusha maneno ya Mwenyejeri Carlo Acutis na kijana Gino Pistoni,ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 20 mnamo 1944, ambaye mchakato wa kutangazwa wenyeheri unaendelea. Mwaliko ni ujasiri katika nyanja zote za maisha.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 18 Desemba 2021, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa vijana wa Chama cha Matendo  cha vijana Katoliki Italia, kama 70 hivi na katika hotuba yake amewashukuru ujio wao ambao ni kama utamaduni wa kila mwaka katika siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Katika ukumbi huo kulikuwa na mtoto anayezunguka na ambaye aliomba wamwache afanye hivyo kwa sababu alisema ni mjasiri na atakuwa na bahati katika maisha. Alionekana kuwa na ujasiri wa kutafuta kile ambacho hakijuhi. Kwa maana hiyo Papa Francsiko akiwageukia vijana wa kike na kiume amesema wanapaswa kwenda mbele kwa ujasiri. Amemshukuru Rais wa Kitaifa wa Chama hicho Profesa Giuseppe Notarstefano, Msimamizi Mkuu Monsinyo Gualtiero Sigismondi, pamoja na wahusika wakuu wa kitaifa na baadhi ya wasimamizi wa vijana. Amesalimia kwa upendo na kwa njia yao kuwashukuru watu wengi ambao wanajitolea kwa ukarimu katika mafunzo yao ya kidini, kwa kujitoa muda wao na rasilimali ya Chama hicho.

Sisi siyo nakala

Baba Mtaaktifu Francisko amekumbusha juu ya kauli mbiu inayowaongoza mwaka huu katika makuzi yao ya imani kuhusu ‘Kipimo chao’, ambayo ilitokana na shughuli zao wanazofanya ndogo ndogo za ushonaji. Papa amependa mada hiyo ambayo inafanya kufikiria nguvu za ona walivyo andaa kazi zao kwa kipimo  na ambazo zinafaa kwa kila aina ya watu . Ni vizuri kwa sababu kila mmoja ni wa pekee Papa amesisitiza. “Hakuna wawili wanaofanana, hapana,  ni mmoja, wa kipekee! Sisi sio nakala, sote ni asili! Na jambo baya ni pale tunapotaka kuiga wengine na kufanya mambo ambayo, watu wengine wanafanya na kutoka katika asili ambapi tunageuka kuwa nakala. Hii ni mbaya. Kila mtu anapaswa kutetea asili yake.”  Papa amekumbusha kwamba Mwenyeheri Carlo Acutis, kijana mwenzao alikuwa anajua hilo na kurudia mara nyingi “Na kiukweli ni muhimu kwamba kila mtu avae mavazi ya asili yake, ya utu wao wenyewe, kila siku kwa furaha”.

Papa akutana na chama cha matendo ya vijana Katoliki Italia
Papa akutana na chama cha matendo ya vijana Katoliki Italia

Papa amesema:“fikiria, katika historia hakuna mtu na hakutakuwa na mtu yeyote sawa na wewe,…Sisi sote ni tofauti. Kila moja ana uzuri wa kipekee na usioweza kurudiwa. Na wakati mtu  huyo anafanya mambo mabaya, kila mtu ni mbaya wa kipekee, usioweza kurudiwa. Kila mtu ni asili katika mema na mabaya!” Kwa namna hiyo Papa amefafanua kwamba  Yesu anawaona na ambaye anawapenda jinsi walivyo vaa hata kama inawezekana kuwapo hasiye wafikiria na kuwajali. Yesu ambaye alikuja ulimwenguni akiwa mtoto, anaamini katika ulimwengu wa kipimo cha mtoto. “Alitufanya kujua hili kwa kuzaliwa Bethlehemu. Lakini hata leo hii, vijana wa leo hii kwa kila Nchi na kila watu na anafanya kila siku. Ni mtindo wa Mungu ambaye anajieleza kwa maneno matatu: ukaribu, huruma na upole. Huo ndio mtindo wa Mungu hakuna mwingine”, Papa ameeleza.

Vijana wajifunze ukaribu wa wengine, familia na marafiki

Mbele ya Yesu ambaye anajifanya kuwa karibu, Papa amwasahauri wajifunza na wao kuwa karibu; kwa ukaribu na wengine, familia, marafiki, wenzao na wenye kuhitaji  Inawezekana daima kufanya lolote kwa ajili ya wengine bila kusubiri wengine wafanya lolote kwa ajili yao. Inawezekana daima kuwa wamisionari wa Injili na kuwa kila mahali kuanza na mazingira ambayo kila mmoja anaishi; katika familia, shuleni, parokiani na katika maneo ya michezo na starehe.  Lakini ili kufanya hivyo, kuchukua mtindo wa Yesu, kuwa mashuhuda wake, ni lazima wawe pamoja naye, wampe nafasi katika siku zao. Papa akiendelea  amewauliza kila mmoja wao, wavulana na wasichana: “je, mnampatia  Yesu nafasi katika siku zenu, katika kazi zenu, katika masomo yenu, katika mapumziko yenu, katika mchezo wenu? Je, Yesu anaingia humo? Kwa maana hiyo ameongeza kusema kwamba wasiogope kutenga muda kwa ajili yake katika maombi, yaani, kuzungumza pamoja na Yesu  kuhusu marafiki zao kumwomba msaada katika magumu, kumwambia wanapofurahi na wakiwa na ukiwa na huzuni. Na Yesu atawafanya wakuwe katika uungwana huo walionao kama mtu aliyechukuliwa kipimo chake mwenyewe.

Gino Pistoni mchakato wa kutangazwa mwenyeheri

Hata hivyo kwa kuwapa mfano wa dhati amesema Papa kuwa: “Leo nilipokea wasifu wa mvulana ambaye alitoa maisha yake akiwa na miaka 20 tu,  alitoa maisha yake kwa nchi yake: Gino Pistoni. Mchakato wake wa kutangazwa mwenyeheri unaendelea. Na alitoa maisha yake kwa damu yake, iliyoandikwa kwa damu yake ... Na mara moja nilifikiria juu yenu: nitampeleka kwenye tafakari ya Katekesi ili kuzungumzia kuhusu kijana huyu. Maisha yenu … Kila mmoja wenu atoe maisha, lakini vizuri, kwa kila kitu: kujifafanua kama alivyojieleza kwa damu, kujieleza kwa kila kitu mlichonacho”.

Papa akutana na chama cha matendo ya vijana Katoliki Italia
Papa akutana na chama cha matendo ya vijana Katoliki Italia

Yesu anatoa katika moyo uliojaa furaha kwa sababu ni yeye peke yake mwenye uwezo wa kufanya mambo yote mapya katika maisha. Yeye hasahau kamwe wao; na daima yuko tayari kuwatia moyo na hachoki kamwe kuwaamini wao. Papa Francisko ameongeza kusema kuwa Yesu anawaona nguvu zao, na ujasiri kila mara wanapokwenda kukutana naye katika Misa, anawatazama na kutabasama,  kwa namna ya peke wanapojarifu kufanya ishara za kushirikishana na mshikamano kuelekeza kwa wengina, hasa wanapokuwa na uwezo wa kukaa karibu na yule aliye na upweke , bila marafiki, aliye katika matatizo; kwa yule anayeteseka ambao kwa bahati mbaya wapo wenzao wengi wanaoteseka. Baba Mtakatifu amewaomba wafikirie hao jamaa wasio wajua, lakini wapo wengi. Wawabebe katika mioyo yao na kumwambia Yesu kwa ujasiri katika safari yao ya maisha. Yesu anawategemea wao. Kwa kuhitimisha amewashukuru tena na kuwatakia sikukuu ya furaha kwa familia zao na Chama kizima chao. Amewabariki kwa moyo na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

18 December 2021, 17:00