Papa atuma salamu za rambi rambi na ukaribu kwa maombi
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Kufuatia na janga lililojitokeza la kuanguka kwa majengo kadhaa katika mji wa Ravanusa nchini Italia mnamo tarehe 12 Desemba 2021 kutokana na mlipuko wa gesi, Baba Mtakatifu Francisko Jumanne tarehe 14 Desemba 2021, ametuma salamu za rambi rambi na kushiriki mateso na watu wote waliopoteza wapendwa wao. Katika salamu zake zilizotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, kuelekeza kwa Askofu Mkuu Alessandro Damiano wa Jimbo kuu katoliki la Agrigento, anaonesha namna anavyobeba mateso ya watu wengi katika ajali hiyo na kuomba uwafikie ukaribu wake kwa kuwakikishia sala zake kwa ajili ya marehemu wote katika ajali hiyo.
Baba Mtakatifu aidha anaonesha shukrani kubwa kwa wale wanaoendelea kusaidia opereshini ya uokajia, na kama ilivyo hata ukusanyaji wa msaada maalum uliohamasishwa na Jimbo Kuu katoliki la Agrigento kwa ajili ya kusaidia jumuiya ya Ravanusa. Papa anawatakia baraka ya Mungu kwa maombezi ya Bikira Maria, mfariji na faraja kwa wele wanaoteseka na matokeo mabaya ya janga hilo na kuwabarki kwa baraka takatifu. Kuhusiana na tukio hil la Mlipuko wa gesi ambayo ilisababisha kuanguka kwa jengo la orofa nne na majengo mengine mengi. Ni zaidi ya watu 150 wasio kuwa na makazi wakati watu saba wamekufa. Hata salamu za rambi rambi ziliendelea kutolewa na wengi hata na Rais wa Jamhuri ya Italia mara baada ya mlipuko huo huko Ravanusa, Agrigento.