Tafuta

2021.12.13 Papa Francisko akutana na Maaskofu wa Ufaransa. 2021.12.13 Papa Francisko akutana na Maaskofu wa Ufaransa. 

Nyanyaso kwa watoto:Papa amezungumza na Maaskofu wa Ufaransa

Rais wa Baraza la Maaskofu Ufaransa (Cef),Askofu Eric de Moulins-Beaufort,na makamu wake wawili walizungumza na waandishi wa habari Vatican masaa machache mara baada ya kukutana na Papa Francisko,mnamo Jumatatu tarehe 13 Desemba 2021.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Wajumbe kutoka Baraza la maakofu Ufaransa (CEF walikutana na Papa Francisko Jumatatu tarehe 13 Desemba 2021. Masaa machache baada ya kukutana na Papa, waliweza kuzungumza na waandishi wa habari, katika Seminari ya Kifaransa iliyoko Roma na kueleza kwamba walikwenda kumweleza yatokanayo na  mkutano wao wa mwaka uliofanyika hivi karibuni huko Lourdes. Ni kweli kwamba maaskofu waliunganika huko Lourdes kuanzia tarehe 2 hadi 8 Novemba 2021 na kujikita na tafakari kwa namna ya pekee juu ya ripoti ya Ciase yaani Tume  ya maaskofu  kuhusu nyanyaso katika Kanisa ambayo ilichapishwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2021 na (kuibua jaziba kubwa sana chini Ufaransa, kwa namna ya pekee  juu ya takwimuambayo kulingana na uchunguzi wa waathirika inabainisha ni 330,000 wa unyanyasaji wa kijinsia ndani ya Kanisa Katoliki tangu 1950).

Askofu  Éric de Moulins-Beaufort, Rais wa Baraza la Maaskofu ameelezea kwamba maaskofu wa Ufaransa katika mkutano huo huko Lourdes waliishi kipindi cha uongofu na wakati Askofu Olivier Leborgne yeye hata alizungumza juu ya matukio ya kiroho ambayo yaliwaongoza kuweza kusikiliza na kuwajali waathirika katikati ya njia yao. Yote hii ni pamoja na dhana ya uwajibikaji wa kitaasisi, zaidi ya mapungufu ya mtu binafsi. Na wakati wa Mkutano mnamo tarehe 13 Desemba 2021, Papa Francisko amesisistiza juu ya hadhi ya tabia yao na ya ulimwengu kwa njia ya kuelewa na kufikiria ripoti Ciase, ya Tume kwa ajili ya uchunguzi  na kuwatia moyo ili waendelee kupia njia ya kisinodi kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa.

Kwa maana hiyo ripoti hiyo inasalia kuwa msingi  wa kufanyia kazi, licha ya mabishano ya hivi karibuni. Papa, ambaye atampokea Jean-Marc Sauvé, rais wa Tume hiyo (Ciase), katika tarehe ambayo bado haijapangwa, ameonesha kupendezwa na baadhi ya vipengele ambavyo maaskofu waliweza kueleza moja kwa moja kwake, hasa  takwimu za kihistoria  ambamo Kanisa la Ufaransa lilishughulikia mapadre wenye matatizo. Masuala maalum zaidi na ya hivi sasa kuhusu namna ya kuwasaidia waliopata unyanyasaji wa watoto pia yalijadiliwa wakati wa mikutano ya  Baraza la Maaskofu wa Ufaransa (CEF) na Makardinali Marc Ouellet na João Braz de Aviz, wote wawili wwenyeviti wa  Baraza la  Kipapa la Maaskofu na wa Baraza la Kipapa la  Taasisi za Mashirika ya Kitawa  na Jumuiya za maisha ya Utume, ambao walikuwa amejulishwa kuhusu ripoti ya Ciase. Kuhusu nchi nyingine za Ulaya, kumekuwa na mabadilishano yasiyo rasmi. Januari ijayo, mkutano wa Baraza la Maaskofu Ufransa ( CEF) na marais wa Mabaraza ya Maaskofu wa Ujerumani na Uswisi utaruhusu kubadilishana uzoefu na uchunguzi mwingine unaofanywa kwa njia tofauti.

Katika mazungumzo yake na Urais wa CEF, Papa mwenyewe alirejea kwenye mkutano wa kilele wa ulinzi wa watoto wadogo katika Kanisa uliofanyika Vatican mnamo mwezi Februari 2019, kwa kushirikisha marais wa maaskofu kutoka duniani kote, na alilisisitiza kufanya kila linalohitajika kukabili na mzizi wa uovu katika ngazi ya kimataifa. Kwa upande wa Maaskofu, changamoto ni kuishi safari ya kiroho na ujiweka mbele za Bwana huku wakichukua majukumu yao mbele ya wahanga na mbele ya Kristo. Kuhusu kujiuzulu kwa hivi karibuni kwa Monsinyo Michel Aupetit, ambaye sasa ni askofu mkuu mstaafu wa Paris, maaskofu hao waliambia vyombo vya habari kwamba Papa aliwaelezea huzuni yake kwa kuchukua uamuzi huu, ikizingatiwa kwamba hali ambayo imeundwa lakini pia  inaruhusu zaidi kujirudia katika jimbo. Papa Francisko alionesha heshima yake kwa mwitikio wa kichungaji wa Askofu Mkuu Aupetit na kuelezea jinsi ambavyo mara nyingi hutokea kelele lakini bila kukubali kwamba maaskofu wanaweza kuwa wadhambi. Kwa mujibu wa Askofu  de Moulins-Beaufort amehitimisha kwamba mtazamo huu, unatofautiana na ule wa watu wa Mungu wanaosali na wanaoteseka.

14 December 2021, 16:03