Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Mkutano na watawa,mapadre na maaskofu

Katika hotuba yake ya kwanza ya ziara yake ya Kitume huko Cyprus na Ugiriki,Papa Francisko amehutubia Maaskofu,Mapadre,Watawa Makatekista kwa kuwaalika wawe na roho ya udugu,msamaha,huruma na kufunguliana wazi.

Na Sr. Angella. Rwezaula – Vatican.

Kanisa lenye subira ndilo linalofaa zaidi katika ukweli wa Cyprus, Kanisa  ambalo halijiruhusu kufadhaishwa na kusumbuliwa na mabadiliko, lakini kwa utulivu linakaribisha upya na kupambanua hali katika mwanga wa Injili. Haya ni matarajio, maoni na faraja ya Papa Francisko kwa wakleri wakatoliki, watawa na makatekista waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Kimaronite la Nicosia la Mama yetu wa Neema mwanzoni mwa ziara yake ya Kitume huko Cyprus tarehe 2 Desemba 2021.

Papa akikutana na Maaskofu,Makleri, Watawa na makatekista
Papa akikutana na Maaskofu,Makleri, Watawa na makatekista

Papa Francisko akiwahutubia wawakilishi wakatoliki waliopo Cyprus wenye Ibada ya Kilatini, Waroma na Wakatoliki wa Armenia, Papa alikumbusha utajiri wa utofauti wao na kuwahimiza kuvumilia bila kuchoka au kukata tamaa. Miongoni mwa waliomkaribisha ni Askofu Mkuu wa Kimaronite wa Cyprus, Selim Sfeir, Patriaki wa Kimaronite wa Antiokia Bechara Boutros Rai na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalem Pierbattista Pizzaballa. Video fupi inaonesha tukio hili.

Papa akikutana na Maaskofu,Makleri, Watawa na makatekista
Papa akikutana na Maaskofu,Makleri, Watawa na makatekista

 

 

02 December 2021, 17:14