Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Mkutano na Sinodi ya Kiorthodox

Ijumaa tarehe 3 Desemba 2021 ikiwa ni katika siku ya pili ya ziara yake huko Cyprus,Papa Francisko amekutana na Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiorthodox ya Cyprus.Wakati wa hotuba yake,Papa amesisitiza uhusiano wa pamoja kati ya Makanisa katoliki na Kiorthodox na shauku yake ya kuimarisha mazungumzo ya kiekumene,ambapo ametumia mfano wa Mtakatifu Barnaba.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Ikiwa ni katika siku ya pili ya ziara yake huko Cyprus, Ijumaa tarehe 3 Desemba 2021 Papa Francisko amekutana na Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiorthodox ya Cyprus. Wakati wa hotuba yake, Papa amesisitiza uhusiano wa pamoja kati ya Makanisa ya katoliki na Kiorthodox na shauku yake ya kuimarisha mazungumzo ya kiekumene, ambapo amechukua mfano wa Mtakatifu Barnaba. Papa Francisko amesema kuwa tunda moja jema, kwa mfano, ni yote yaliyotokea Cyprus katika Kanisa la Panaghia Chryssopolitissa, kwa Mama yetu wa Jiji la Dhahabu mahali wanafanyia ibada kwa ajili ya madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayopendwa sana na watu na mara nyingi wanachagua kanisa hilo kwa ajili ya sherehe za kufunga ndoa. Papa amesema “ Hivyo ni ishara ya muungano katika imani na maisha chini ya mtazamo wa  Mama Mtakatifu wa Mungu anayewakusanya pamoja watoto wake. Ndani ya utata pia kuna safu ambapo, kulingana na mapokeo, Mtakatifu Paulo alipigwa viboko thelathini kwa sababu ya kutangaza imani huko Pafo. Utume, kama muungano, daima hupitia sadaka na majaribu. Papa amesema kuwa Kanisa letu ni mama, na mama huwakusanya watoto wake kwa upendo mwororo”.

Mkutano wa Papa na Sinodi ya Kiorthodox huko Cyprus
Mkutano wa Papa na Sinodi ya Kiorthodox huko Cyprus

Papa ameongeza kusema kuwa “Tuna imani kwa Mama Kanisa hili, ambalo linatukusanya sisi sote na, kwa uvumilivu, upendo mwororo na ujasiri, hutatufanya tusonge mbele katika njia ya Bwana. Na ili kuhisi umama wa Kanisa, sote inabidi twende huko, ambapo Kanisa ni mama. Sisi sote, pamoja na tofauti zetu, lakini watoto wote wa Mama Kanisa. Tumwombe Mungu atujalie hekima na ujasiri wa kufuata njia zake, na si zetu. Tuombe haya kwa maombezi ya watakatifu. Leontios Machairas, mwandishi wa historia wa karne ya kumi na tano, alifafanua Cyprus kuwa “Kisiwa Kitakatifu” kwa sababu ya idadi kubwa ya wafia dini na wanaokiri  ambao nchi hizo zimejua kwa karne nyingi. Mbali na wale wanaojulikana na kuheshimiwa, kama vile Barnaba, Paulo na Marko, Epiphanius, Barbara na Spyridon, kuna wengine wengi sana: safu nyingi za watakatifu ambao, wameunganishwa katika Kanisa moja la mbinguni. Mama Kanisa na wao wanatuhimiza tusafiri pamoja kuelekea bandari ambayo sote tunaitamani”. Video fupi na picha zinaonesha matukio ya leo.

Mkutano wa Papa na Sinodi ya Kiorthodox huko Cyprus
Mkutano wa Papa na Sinodi ya Kiorthodox huko Cyprus
03 December 2021, 10:50