Tafuta

2021.11.15 Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wafransiskani Sekulari. 2021.11.15 Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wafransiskani Sekulari. 

Papa kwa wafransiskani wasekulari:toeni ushuhuda rahisi kwa watu na kutuliza maumivu

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Shirika la Wafransikani Wasekulari katika fursa ya Mkutano wao Mkuu.Akihutubia amesema wao ni sehemu ya Kanisa linalotoka nje.Watoe ushuhuda wa Injili ya maisha rahisi bila kujidai.Wapambane na kufanya kazi kwa ajili ya haki,utume na ikolojia fungamani.Wito wao unazaliwa kwa ajili ya utume wa ulimwengu ambao ni utakatifu.Wamfuase Kristo kwa mfano wa Mt.Francis.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kupambania haki, kushirikiana kwa mipango ya kimisionari, kufanya kazi kwa ikolojia fungamani, pia kujihusishaa kwa ngazi ya kijamii na kisiasa, bila kusahau wito wa msingi wa kuwa kati ya watu, na rahisi na bila majivuno kwa ì kutafsiri Injili, chanzo cha matumaini katika majanga ya sasa kwa kujikita katika matendo madhubuti. Ndiyo mwito wa maneno ya Papa Francisko Jumatatu tarehe 15 Novemba 2021 kwa mara nyingine tena kwa siku chache mara baada ya kutoka Assisi kwa ajili ya mkutano na maskini wa Ulaya, ya hotuba yake kwenye Jumba la Kitume, Vatican alipokutana na Wajumbe Wafransiskani Wasekulari, wakiwa katika fursa ya Mkutano Mkuu wao, ambalo ni tawi Kifransiskani linalowajumuisha  walei wa kike na kiume hata wale waliofunga ndoa, ambao wanataka kuishi maisha ya amani na  Injili kwa mfano  wake Mtakatifu Francis wa Assisi.

Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari
Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari

Na ndio hasa utume na wito huu, unaochota lishe yake kutoka katika wito wa ulimwengu wote ambao ni utakatifu unaoelekezwa kwa wabatizwa wote, na kwa maana hiyo Papa Francisko amekumbuka katika hotuba yake. Utakatifu unaotakiwa na katiba kuu lakini pia na sheria iliyoidhinishwa mwaka wa 1978 na Papa Paulo VI, ambayo inahusisha uongofu wa moyo, unaovutiwa, kupata ushindi na kubadilishwa na Kristo, ambaye ni mwema, kwa kila jema na aliye bora zaidi. Hili ndilo linalowafanya watubu wa kweli, Papa amesema. Hata hivyo amebainisha kuwa inabidi wawe waangalifu, ili wasichanganye kufanya toba na matendo ya toba. Hayo ya kufunga, kutoa sadaka, kufidia ni matokeo ya uamuzi wa kufungulia moyo kwa Mungu; Kufungulia moyo kwa Kristo, kwa kuishi kati ya watu wa kawaida, kwa mtindo wa Mtakatifu Francis, kama vile alivyokuwa ‘kioo cha Kristo’, vivyo hivyo na wao wanapaswa wawe vioo vya Kristo.

Papa Francisko akiendelea nahotuba yake amesema umaskini na urahisi, ni ishara bainifu mbele ya kila mtu kwa maana wao ni wanaume na wanawake waliojitolea kuishi ulimwenguni kulingana na karama ya Kifransiskani. Wito wa Wafransiskani Kisekulari kwa maana hiyo ni kuishi Injili ulimwenguni kwa mtindo wa Maskini Francis bila utajiri. Kuchukua Injili kama mtindo hai na kanuni ya maisha. Huo ndiyo mwaliko wa kuikumbatia Injili na kufinyangwa nayo katika uzima. Huo ndiyo mtindo wa kuishi umaskini, udogo, urahisi ambao kama ishara zao bainifu mbele ya kila mtu kwa sababu katika utambulisho wao wa Kifransiskani na wa kiulimwengu, wao ni sehemu ya Kanisa linalotoka nje Papa amesisitiza. Nafasi yao inayoipendeza zaidi ni kuwa miongoni mwa watu, na pale, kama walei, waseja au waliofunga ndoa, mapadre na maaskofu, kila mmoja kulingana na wito wake hususani, wanamshuhudia Yesu kwa maisha yaliyo rahisi, bila kujidai, daima wakiwa na furaha kumfuasa Maskini na msulubiwa Kristo, kama alivyofanya Mtakatifu Francis na wanaume na wanawake wengi wa Shirika lao.

Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari
Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari

Baba Mtakatifu Francisko akirudia kusisitiza faraja na mtindo ambao daima amekuwa akiwaelekeza waamini wote amesema wap waondoke kuelekea nje kwenda pembezoni mwa maisha ya sasa na huko ili kufanya neno la Injili kuwa na sauti. Wasiwasahau kamwe maskini, ambao ni mwili wa Kristo. Leo hii wote wanaitwa kutangaza Habari Njema kwao, kama alivyofanya Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria, ambaye ni Msimamizi wa Shirika la Wafransikani wasekulari kati ya wengine. Na kama ilivyokuwa zamani, mashirika ya watu waliotubu yalijulikana kwa kuanzisha hospitali, zahanati, meza za kutoa chakula kwa maskini na kazi nyingine za upendo ambazo ni thabiti kwa jamii, vivyo hivyo leo hii, Roho hiyo inawatuma kutekeleza upendo huo huo kwa ubunifu unaohitajika katika aina mpya za umaskini. Papa Francisko amewaomba watumie nafasi yao ya kisekulari kuwa kamili kwa ukaribu, huruma na upole. Nawanaweza kuwa wanaume na wanawake wa matumaini, waliojitolea kuiishi pia kuandaa, kutafsiri katika hali halisi za kila siku, ule uhusiano wa kibinadamu, katika jitihada ya kijamii na kisiasa; kukuza tumaini la kesho kwa kupunguza maumivu ya leo hii.

Hatimaye Papa Fransisko kwa wajumbe hao amekumbusha shauku kubwa ya Mtakatifu Francis kwamba, familia nzima iendelee kuwa na umoja na kwa hakika kuheshimu tofauti na uhuru wa vipengele mbalimbali pia kwa kila mjumbe mwanachama wa familia ya kifransiskani. Lakini siku zote kwa ushirikiano muhimu kwa wa kuheshimiana, kuota ndoto za pamoja ulimwengu ambazo kila mtu anazo na anahisi kama ndug na wanao jitahidi pamoja na ugumu kuujenga. Wanaume na wanawake wanapambania haki na amani na wanaofanya kazi kwa ajili ya ikolojia fungamani huku wakishirikiana katika mipango ya kimisionari na kuwafanya wawe wapatanishi na mashuhuda wa Heri za mlimani. Kwa kufanya hivyo ni kuanza njia ya uongofu na baadaye mapendekezo hayo yote ya kuzaa matunda yanayotoka moyoni, yakiunganishwa kwa Bwana na mpenda umaskini.

Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari
Papa amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wafransiskani Sekulari
15 November 2021, 16:06