Tafuta

2021.10.18:Kampeni ya watoto milioni moja kusali Rosari inayohamasisha na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji. 2021.10.18:Kampeni ya watoto milioni moja kusali Rosari inayohamasisha na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji. 

Watoto milioni moja wasali Rosari

Tarehe 18 Oktoba 2021 watoto milioni moja wamesali rosari kwa pamoja kwa ajili ya Amani,kama mchakato wa Kampeni hiyo iliyoanzishwa mnamo 2005 na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji.Rosari imewaunganisha watoto kwa ngazi za shule,parokia na familia.Papa Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika Oktoba 17,aliwakumbuka na kuwatia moyo.

Na Sr. Anela Rwezaula – Vatican.

Kampeni iliyoanzishwa na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji linataka kuhamasisha sura ya Mtakatifu Yosefu katika mwaka ambao umetolewa wakfu kwa ajili yake na kwa maana hiyo ni milioni moja ya watoto aamesali rosari, kwa kuhusisha maparokia yote, shule za watoto awali, shule za msingi na katika familia zote, kwa sala kubwa kwa ajili kuombea ya amani na umoja ulimwenguni kote. Tukio hili limeandaliwa kufanyika tarehe 18 Oktoba, 2021 siku ambayo inataka kwa hakika kutia moyo hata watoto ili watafute msaada na nguvu ya Mungu katika wakati mugumu, kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa Kardinali Mauro Piacenza, Mwenyekiti wa Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (Acs). Katika toleo hilo wamependekeza vifungu kutoka katika Barua ya “Patris Corde”, yaani Moyo wa Baba ambayo Papa Francisko aliandika kwa ajili ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 150 tangu kutangazwa kwa Mtakatifu Yosefu kuwa Msimamizi na mlinzi wa Kanisa la ulimwengu.

Papa awatia moyo watoto milioni moja kusali rosari

Baba Mtakatifu mara baada ya sala ya malaiaka wa Bwana Dominika tarehe 17 Oktoba 2021 alikumbusha juu ya  Kampeni ya watoto milioni moja kusali Rosari iliyoandaliwa na Shirika la Kipapa cha Kanisa hitaji kwa kuhamasisha taasisi za kielimu, familia  na parokia zote kusali kwa ajili ya  umoja na amani. Amewatia moyo katika kampeni hiyo ambayo kwa mwaka huu inaongozwa kwa namna ya pekee kwa  Maombezi ya Mtakatifu Yosefu katika fursa ya maadhimisho ya miaka 150 tangu kutangaza kuwa msimamizi wa Kanisa la Ulimwengu. Amewashukuru watoto wote kwa ushiriki wao.

Kuiga mfano wa Mtakatifu Yosefu

Lengo la shirika la Kanisa Hitaji ni kuwaalika watoto wote kusali na Mama Maria, chini ya ulinzi wa Mtakatifu Yosefu katika mwaka ambao umewekwa kwa ajili yake. Mtakatifu Yosefu, msimamizi wa Kanisa kwa maelezo ya Kardinali Piacenza, "ni kwa ajili yetu mfano mkuu wa jinsi ambavyo Mungu anaweza kuelekeza yote yaliyo mema kwa njia ya sala zetu, uaminifu wetu, na utii wetu kwa Neno la Mungu". Katika maelezo ya Kardinali Piacenza amebainisha kwamba leo hii sio tu mgogoro wa kiafya uliosababishwa na virusi vya Uviko-19 kuhatarisha nchi, lakini pia kuna hata njaa, umaskini, ufisadi, vita, kashfa ya maisha ya binadamu, na uharibifu wa kazi ya uumbaji ambao umeona unaharibu idadi kubwa ya maisha ya watu na ndiyo sababu kuna haja kweli ya maombi muhimu, hasa, ya  watoto, ili Mungu aupatie  ulimwengu wokovu wote". Mwaka jana, watoto milioni moja waliosali Rozari walivunja rekodi ya mahudhurio, ambapo walikusanya watoto kutoka nchi 136 ulimwenguni  kwa ajili ya kusali sala, pamoja na nchi ya  Siria, Iraq, Mexico, Armenia, Papua New Guinea, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vile vile kwa kujiandikisha kwenye ukurasa tovuti ya Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji, zaidi ya watoto 509,000.

 Kampeni ilianza 2005

Tovuti ya Mfuko wa kipapa imetoa zana muhimu za bure katika lugha 26 ili kusali katika parokia, shule, vikundi vya watoto au na familia, na maagizo ya jinsi ya kusali Rozari, tafakari juu ya mafumbo na kujitoa kwa watoto kwa Mama wa Mungu Maria. Mambo mapya kwa mwaka huu hasa ni juu ya Mtakatifu Yosefu ambaye amewekwa katika mabango karibu na Bikira Maria na sala yake ambayo Baba Mtakatifu Francisko anasali kila siku. Kampeni ya Milioni moja ya watoto ya kusali rosari ilianzishwa mnamo 2005 wakati kikundi cha watoto walikuwa wakisali Rosari katika Kanisa dogo la Carcas nchini Veezule na wengi wao waliokuwapo walikumbuka maneno ya Padre Pio: “ikiwa milioni moja ya watoto watasali rosari, ulimwengu utabadilika. Na tangu wakati huo, kampeni hiyo kwa haraka ilisambaa ulimwenguni kote.

Msaada kwa Afrika na nchi za mashariki ya Kati

Idadi kubwa ya mipango ya kusaidia na kukuza imani kwa watoto wakristo imegawanyika katika maeneo mengi ya kijiofia. Nchi za mashariki ya Kati kwa mfano Baraza la kipapa la Kanisa Hitaji, linafadhili kifedha taasisi tatu zinazo endeshwa na Shirika la Wakarmeli kwa wanafunzi 2500. Kwa namna ya pekee nchini Siria, mfuko unachangia kozi za makatekista zinazo tolewa na Wajesuit kwa watoto na vijana 1,150 wa Homs, na katika makambi mbali mbali ya kiangazi. Barani Afriika huko Essiengbot (Camerun), wamenzisha shule ya awali ya watoto 305 na wanafunzi wengine wa wshule 101 inayoendeshwa na Watawa wa Shirika la Mungu Mpaji. Hata huko Dhadim (Etiopia), Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji ACS linasaidia shughuli za maparokia kwa ajili ya mafunzo ya mamia ya watoto: Huko  Katikamu (Uganda), wanasaidia kifedha Kituo kimoja cha Emmaus kwa ajili ya kuhamasisha imani kwa wakimbizi kutika Sudan Kusini walioko kwenye kambi la Bidibidi.

Na Amerika Kusini latina

Shirika hili pia inasaidia huko Vietnam, kwa msaada wa makatekista , kwa karibu ya wmafunzi 26,000 wanaotoka katika maparokia 185 au nchini  Armenia katika makambi ya kiangazi kwa ajili ya vijana, ambao wanasaidiwa na Wata wa Kiarmeno wa Maria Mkingiwa wa huko Tzaghkadzor. Na hatimaye huko Barani Amerika ya Kusini nchini  Paraguay wanasaidia kituoa cha malazi kiitwacho  “Mamá Margaritaù kinachoendeshwa na watawa wa Maria mama wa Msaada  huko  Ñu Apu’, wakati nchini  Uruguay ACS inasaidia Mfuko wa Sophia wa Montevideo, jengo ambali linaendesha shule 32, Nchi Venezuela , shirika hili linazsidia Wadomenikani katika Serikali ya Ampure, wakiendesha shule ya awali , msingi na sekondari kwa wanafunzi zaidi ya 1,100.

18 October 2021, 16:51