Tafuta

2020.03.04 Papa Francisko na wanawake wakati wa Katekesi moja jijini Vatican. 2020.03.04 Papa Francisko na wanawake wakati wa Katekesi moja jijini Vatican. 

Papa:Wanawake ni muhimu katika ujenzi wa ulimwengu kama nyumba ya wote

Limefunguliwa huko Milano Italia Jukwaa la Wanawake 'Women's Forum G20 Italy' tangu 17-19 Oktoba 2021 kwa lengo la kujiwekea vipaumbele na miongozo kwa ajili ya kuanza upya maisha baada ya Uviko.Wakati ujao uko ndani ya mwanamke ili kujikwamua wote kwani umoja ni nguvu kwa lengo la ujumuishaji mpya katika uongozi.Papa amesema wanawake katika kipinid cha janga wamejua na kujitoa kwa dhati katika maisha kwa uvumilivu na ukimya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wanawake ndiyo kitovu cha kuanza tena kiuchumi na kijamii baada ya UVIKO-19.  Katika kutazama changamoto ya uongozi. Katika moyo wa Milano ambao sio tu kama mji wa uzalishaji katika Nchi ya Italia lakini pia ambao umegeuzwa kwa siku tatu kuwa maabara ambayo inawaona jukwaa la wanawake Women's Forum G20 Italy.  Lengo lake ni kutoa kipaumbele cha na miongozo kwa namna ya kuanza kwa upya katika uzalishaji kwa ajili ya wote.  Mada ni nyingi ambapo ni kutoka katika akili mbadala hadi kufikia maadili ya kifedha, kutoka katika mabadiliko hadi kufikia kile kinachoitwa mkakati wa mapambano ya kutoa elimu kwa ajili ya wote. Hata hivyo tathimini ya usawa haifariji. Kiukweli, kumekuwa na kuboreshwa kidogo kwa uwezeshwaji wa wanawake na uongozi, lakini tofauti za kijinsia bado zinaendelea kuonekana katika maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video, ambao umesoma na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Katika ujumbe huo uliomwelekeza Chiara Corazza, mwakilishi maalum wa G7 na G20 wa Jukwaa la Wanawake katika Uchumi na Jamii ambao huko Milano Italia amesema:Jukwaa la wanawake wa G20 unakaribishwa sana hasa katika ulimwengu ambao unahitaji uongozi wa wanawake na uongozi katika zana za  mawazo na kujitoa kwao. Mnamo 1995 Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika kuwa “wanawake wataendelea kushika nafasi katika kutoa suluhishokwenye matatizomengi ya wakati ujao(…) na watasukuma mfumo wa kuweza kusaidia katika mchakato wa kibinadamu mbao ni msingi katika ustaarabu wa upendo.

Baba Mtakatifu mwenyewe anasisitiza kuwa wanawake wanao mchango mkubwa usio na kifani katika kujenga ulimwengu ambao unaweza kuwa nyumba ya wote.  Ndani ya mwaka huu, wanawake wamejua na kujitoa kwa dhati katika tishio la maisha kwa uvumilivu na ukimya. Na katikati ya matatizo ya kiumchumi, kijamii na mabadiliko ya tabianchi, wanawake wamekuwa mchango mkuu wa kuhamasisha kuondokana na ubinafsi ambao inahitaji kushirikishana ili kuweza kutunza nyumba yetu ya pamoja na kupambana na mantiki za kutupa na kutafuta faida.

Baba Mtakatifu amesema kuwa hakuna shaka kwamba mshikamano na ushirikiano wa kweli kati ya wanawake na wanaume pia ni msingi katika jamii.  Hao kwa namna ya pekee wanaitwa kukumbatia wito wao wa kuwa wajenzi hao wa kijamii. Na wakati huo huo hii inahitaji mabadiliko ambayo yanaweza kutoka katika ufundi na ambao unaongozwa kujipyaisha maana ya ubinadamu na ahadi ya kweli ambayo ndiyo tabia ya mtu binadamu. Kwa niaba ya Papa Francisko, Kardinali  Parolin pia amechukua fursa  kusisitiza kwa kutia moyo kwa nguvu ya kwamba kila mwanamke  katika kila nchi, anaweza kupata elimu bora, ili kila mmoja wao asitawi, kupanua uwezo wao na talanta, na kujitoa kwa maendeleo na maendeleo ya jamii zinazoshikamana.

18 October 2021, 16:55