Tafuta

Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa sala. Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa sala. 

Tarehe 22 Oktoba ni kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane Paulo II

Mtakatifu Yohane Paulo II alizaliwa mnamo tarehe 18 Mei 1920 na kifo chake mnamo tarehe 2 Aprili 2005. Alitangazwa kuwa mwenyeheri mnamo Mei Mosi,2011.Papa Fransisko alimtangaza kuwa Mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ambayo inakumbushwa Upapa wake, Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 22 Oktoba ambayo kwa hakika  inaweza pia kukumbusha mambo mengi ambayo yanasukuna pamoja katika vipindi vya mchakato wa safari yake na upapa wake. Papa Yohane Paulo II alizaliwa mnamo tarehe 18 Mei 1920 huko Poland na kifo chake  tarehe 2 Aprili 2005 jijini Vatican. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef Wojtyła.  Urithi wake hadi leo  hii katika nyakati za janga unatufanya kutambua zaidi na kurudia kumkabidhi Mama Yetu Maria ambaye alikuwa kwake kioo na kweza kukumbuka ushauri wake wa kufungua mawazo ya moyo wetu kwake Kristo. Hayo aliweza kishuhudia kwata katika majribu mwengi aliyopata yawe ya kushmbuliwa au katika ugonjwa wake uliomfikisha mwisho na uvumilivu..

Ilikuwa ni tarehe 22 Oktoba 1978 siku ambayo ilikuwa inaadhimishwa misa ya kuanza Upapa wake Askofu mpya wa Roma na ulimwengu, Yohane Paulo II yanakumbukwa maneno yake: “ Kaka na dada Msiogope kumkaribisha Kristo na kukubali uwezo wake! Msaidie Papa na wale wote wanaotaka kumtumikia Kristo na kwa uwezo wa Kristo, kuwatumikia watu na wanadamu wote! Msiogope! Badala yake Fungukeni, kwa hakika fungueni milango wazi kwake Kristo! ”. Yeye alikuwa Papa wa 264 kuanzia 16 Oktoba 1978 hadi kifo chake kwa kudumu katika huduma hiyo  kwa muda mrefu kuliko mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pio IX

Yeye alimfuata Papa Yohane Paulo I na ambaye hivi karibuni Baba Mtakatifu Francisko ameridhia  Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu ili atangawe na mwenye heri. Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ni Papa wa kwanza asiye kuwa mwitaliano tangu miaka 455, wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena Papa wa kwanza kutoka Poland katika historia yote ya Kanisa. Baada yake yeye alifuatia ni Papa mstaafu Benedikto XVI. Na kwa sasa tunaye Papa Francisko. Mataktifu Yohane Paulo wa Pili ni papa aliyeonesha njia ya kuishi mateso ya Kristo. Mnamo tarehe 22 Oktoba 1980 siku ya Jumatano ya Katekesi yake akiwasalimia wagonjwa akiwa bega kwa bega na mateso ya Kristo aliwakumbusha wote kuwa ni kwa njia ya mateso Yesu alitukomboa kutoka dhambini na kutuimarisha katika muungano na Kristo. Matashi yake kwa wagonjwa hao ilikuwa ni kuwahakikisha maombi yake ili waweze kweli kupata kitulizo cha fumbo la wokovu ambao haukatishi tamaa badala yake mateso ya kibinadamu ni ya lazima

Tarehe 22 Okotba 1981 mwezi mmoja kabla ya shambulia dhidi yake katika Uwanja wa Mtakatif Petro , Papa Wojtyła akiadhimisha misa kwa wanafunzi wa Taasisi ya Kipapa katika Seminari Kuu ya Roma aliwambia "Muwe mboni ya macho yangu na matumaini ya Kanisa la Roma". Na katika fursa hiyo hiyo  akaonesha ishara wazi kwamba katika seminari kuna jumuiya ya kikristo yenye uwezo wa kukomaa katika umbu la wale ambao siku moja watawekwa  wakfu wa kikuhani na wataendeleza katikati yao kazi ya Kristo.

Manmo tarehe 22 Oktoba 1985, Papa Wojtyła kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo ya Kipapa ya Seminari kuu Roma kwani alipendelea sana kukutana nao na wakati huo huo ndiyo ulikuwa mwanzoni mwa mchakati wa Siku ya vijana Duniani,  aliwambia amekwenda hapo katika siku yenye maana sana, pamoja nao waliozungukia altare ya Bwana ili kutoa kwao sadaka takatifu ya Misa. "Mungu ametuumba kwa ajili ya kusaidia tushiriki sadaka yake kuu na timilifu. Lakini Yesu anatufanya tuelewe jambo hili kwa njia fulani, akisema kwamba hali hiyo itabadilishwa,na Mungu mwenyewe atajiweka katika utumishi wetu. Amin, nawaambia, atavaa mavazi yake na kuwaketisha mezani na atakuja na kuwahudumia. Wazo la Mbingu lazima litufanye tushangilie kwa furaha na lazima lichochee kila mmoja kujitoa kwa kudumu katika utakaso binafsi."

22 October 2021, 15:15