Papa:Mkutano wa G20 Roma utambue msimamo wa dunia
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Mkutano Mkuu wa G20 yaani unaokaribi wa matataifa makuu tajiri ulimwenguni utakaofanyika Roma, lazima kuwe makini kuchukua maamuzi kwa kuzingatia uhusiano kati ya Nchi ambazo hazijaendelea nazilizo endelea na kutambua msimamo wa ulimwengu kwa mtazamo upatikanaji wa matibabu ya kiafya , ili kushinda vema janga. Huo ni uthibitisho wa Papa Francisko katika mahojiano na a Télam, shirika la Habari la Nchi ya Argentina. Kwa viongozi wa Nchi na Serikali za nchi zilizo tajiri zaidi kwenye sayari (G20) Papa anatarajia kwamba mkutano unaweza kusaidia kushusha mivutano kwa ngazi ya ulimwengu mbele ya vurugu zinazoendelea na zinazoibua vurugu zaidi ya vurugu.
Ni kipinidi cha kuondoka nadharia na kutenda
Papa amesema kuwa "Hiki ni kipindi cha kuondoka nadharia na kujikita katika matendo". Akisisitiza zaidi amesema "Mchezo unaochezwa sasa hivi inawezekana kuondokana na janga kwa pamoja. Lazima kuyapa matatizo majina yake yote mawili ambayo yanaukabili ubinadamu katika kipindi baada ya janga. Ni msingi vile vile ambao ni sawa sawa na changamoto zitakazo kabiliwa na COP26 kuhusu tabianchi huko Glasgow ambao utafanyika mnamo tarehe 12 Novemba".
Ziara za kitume za Papa zijazo
Papa Francisko pia ameelezea kuhusu ziara zake za kitume ambazo anatarajia wakati ujao, kuanzia na ile ya mwezi Desemba huko Ugiriki na Ciprus ambayo tayari imetajwa. Kwa kwa sasa lakini amebainisha ni ziara mbili ambazo hazijapangwa lakini zilizo kwenye akili yake, huko Congo na Hungheria”, wakati huo huo pia anataka kuzingatia ziara huko Papua Guinea Mpya na Timor Est zilizohairishwa kipindi cha janga. “Nilifikiri daima ulimwengu wa pembezoni unaonekana wazi katika miaka saba ya mwisho kamaPapa nimejionea kwa macho yangu mwenyewe”.
Shukrani kwa Leo Messi
Kwa kufunga baadaye Papa amemshukuru nyota ya mpira wa miguu ya Argentina Lionel Messi, mchezaji sasa wa Paris Saint-Germain, ambaye amehamia Ufaransa, kwa jezi aliyookea katika fursa ta ziara yake Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex, anamshukuru kwa urahisi wake na kwa kumjali. “ Asante kwa ukaribu, kwa ushuhuda kwa kutokugonfisha kichwa na Mungu akubariki na kuwa na imani daima juu yangu” .