Tafuta

2021.10.18 Papa Francisk amekutana na wajumbe wa mfuko wa kitengo cha Madawa cha Chuo Kikuu Roma 2021.10.18 Papa Francisk amekutana na wajumbe wa mfuko wa kitengo cha Madawa cha Chuo Kikuu Roma  

Papa:Mgonjwa apewe kipaumbele na hospitali katoliki zisifuate mafao

Papa amekutana na wajumbe wa mfuko wa Kitengo cha Tiba ya madwa cha Chuo Kikuu Roma.Amesisitiza kuweka tiba ya mtu katikati bila kusahau sayansi.Tiba bila sayansi ni bure na sayansi bila tiba ni tasa.Papa ametoa wito kwa vituo vya kiafya katoliki vishuhudie kwa matendo kwani hakuna maisha yasiyo stahili.Kwa upande wa chanjo unahitajika mipango ya kudumu na mbadala ya kugawanya.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumatatu tarehe 18 Oktoba 2021, amekutana na wawakilishi wa Mfuko wa Chuo Kikuu katika kitengo cha  Madawa cha Roma  na kuwashukuru ujio wao na zawadi yao. Amemshukuru Mwenyekiti wa Mfuko huo Profesa Paolo Arullani, kwa hotuba yake ambayo ameitoa kwa niaba yao wote. Ni vizuri kuwajua moja kwa moja katika siku ambayo inaadhimishwa Mtakatifu Luka ambaye Mtakatifu Paulo anamwita “yule tabibu mpendwa”, (Wakol 4,14). Baba Mtakatifu ameelezea alivyopokea kwa upendo pendekezo la kukutana nao ili kujua Kitengo hicho cha Madawa katika Chuo Kikuu Roma. Anajua ni kwa jinsi gani ilivyo ngumu leo hii kupeleka mbele kazi hiyo katika muktadha wa kiafya na kama inavyojionesha katika Hospitali yao ambayo inajikita si tu katika matibabu lakini pia hata katika utafiti ili kutafuta tiba kwa magonjwa hasa kwa yule anayefanya kazi hiyo kwa upendo wa mtu. Kumweka mgonjwa  kuwa mstari wa mbele kabla ya ugonjwa ndiyo msingi kwa kila nyanja ya madawa. Ni msingi kwa ajili ya tiba ambayo iweze kuwa ya kweli na fungamani na ya ubinadamu wa kweli. Papa amesisitiza tena kwamba “Mgonjwa apewe kipaumbele kabla ya ugonjwa”. Katika safari hiyo amekumbusha kwamba alikuwa anawatia moyo mwenyeheri Alvaro Del Portilo kwa kujikita kila siku katika huduma ya mtu binadamu na katika ufunganaishwaji wake wote. Papa amewashukuru kwa ajili hiyo kwamba Mungu anapendezwa na kazi yao.

Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa
Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa

Kitovu cha mtu ambacho ni msingi wa juhudi zao za utunzaji, lakini pia ni  kimtaala na katika utafiti vinawasaidia kuongeza nguvu ya maono ya umoja na kimkakati. Maono hayo hayatoi nafasi ya kwanza ya mawazo, ya kiufundi na mipango tu  lakini pia mtu wa kweli yaani mgonjwa wa kuweza kutunza kwa kukutana na historia, kumjua namna ya kuishi kwake, kwa kudumisha uhusiano wa kirafiki ambao unaponesha moyo. Upendo kwa binadamu hasa katika hali ya udhaifu, mahali ambapo panaonekana wazi sura hai ya Kristo msulibiwa ni hali halisi ya kikristo na hiyo Papa amesisitiza isipotee kamwe. Kitengo cha Mfuko  Chuo Kikuu cha  Madawa na Hospitali katoliki kwa ujumla, zinaitwa kushuhudia kwa matendo na ambayo hakuna kwa hakika maisha yasiyo stahili, au kubagulia kwa sababu ya kukwenda na mantiki ya kuhitajika  wale wenye kuleta faida.  Papa ameongeza kusema “leo hii tunaendelea kuona utamaduni wa kweli wa ubaguzi; hewa hiyo inavutwa lakini ambayo lazima kutenda dhidi ya utumaduni huu wa kibaguzi”. Kila jengo la kiafya, hasa yale katoliki Papa amesema yanapaswa kuwa mahali pa ushuhuda wa matendo ya kutunza mtu na mahali ambapo inawezekana kusema “hapa hawaoni madaktari na wagonjwa tu, lakini wanaona watu ambao wanakaribisha na kusaidiwa: hapa kuna onjo la mkono wa tiba ya hadhi ya binadamu”. Na hii kamwe pasiwezpo na  mchakato wa majadiliano bali  daima ni kuendelea na utetezi”.

Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa
Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa

Baba Mtakatifu amebainisha kwa ni kuweka kitovu cha tiba ya mwanadamu bila kusahau umuhimu wa sayansi na katika utafiti. Kwa sababu bila sayansi ni bure na kama sayansi ilivyo bila tiba ni tasa. Mambo mawili hayo yanakwenda  kwa pamoja na upamoja ndiyo unafanya sanaa ya tiba , sanaa ambayo inajumisha kichwa na moyo, ambao unaunganisha fahamu na huduma, taaaluma na rehemu, utaalam na maelewano. Papa Francisko amezidi kuwashukuru kwa sababu ya kusaidia maendeleo ya kibinadamu katika utafiti. Mara nyingi  amebainisha kuwa kwa bahati mbaya, zinajitokeza njia zile za kufatafuta mafao, kwa kusahau kuwa kabla ya fursa za kupata faida kuna mahitaji ya lazima ya wagonjwa. Na inaendelea kuona inahitajika maana maana hiyo kujiandaa kukabiliana na  magonjwa hayo na matatizo mengone mapya daima yanayoibuka.  Papa Francisko amekumbuka wazee wengi na wale ambao wanakutwa na magonjwa nadra au adimu. Zaidi ya kuhamasisha utafiti, wapo wanasaidia ambaye hana zana kiuchumi ili kusaidia manunuzi katika vyuo vikuu na kukabiliana na gharama kubwa ambazo katika bajeti za kawaida zisingetosha.

Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa
Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa

Papa mefikiria kwa namna ya pekee jitihada ambazo zimekabiliwa katika kituo cha UVIKO, Msaada wa kwanza, na  hali halisi ya kuwasindikiza watu ambao wananakaribia mauti. Kila kitu kilicho chema na kizuri kinaendesha dharura kubwa kwa ufunguzi daima mkubwa. “Ni muhimu kufanya kazi  kwa pamoja. Kwa kusisitizia hilo,neno la urahisi na wakati huo huo ni  gumu la kuishi  ni lile la upamoja. Hii ni kutokana na kwamba, Uviko umeonesha umuhimu wa kusukana, wa kushirikishana na kwa pamoja matatizo ya pamoja. Vituo vya afya kwa namna ya pekee katoliki, vin ana vitakuwa daima na mahitaji hayo ya kukaa katika mtandao wa umoja. Hakuna muda tena wa kufata  mtindo wa upekee au karama binafsi. Upendo unahitaji zawadi: ufahamu lazima ushirikishwe  utaalam lazima ushiriki, sayansi lazima iwekwe kwa matumizi ya pamoja.”

Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa
Wajume wa Mfuko wa kitengo cha madawa cha Chuo Kikuu Roma wakutana na Papa

Papa Francisko  amesema “Sayansi sio tu bidhaa za sayansi ambazo, zikitolewa peke yake, hubaki viraka vinavyoweza kuziba maumivu ya ugonjwa,  lakini sio kuponya kwa kina. Hii inatumika, kwa mfano, katika chanjo: ni muhimu kuzisaidia nchi ambazo zina upokeaji mdogo wa  chanjo, lakini lazima ifanywe na mipango ya kuona mbali yaani ya kudumu, na sio kusukumwa tu na haraka za mataifa tajiri kuwa salama. Tiba lazima zigawanywe kwa hadhi, sio kama sadaka za rehema. Ili kufanya vizuri, sayansi na matumizi yake muhimu lazima yaendelezwe: kuelewa muktadha, matibabu ya kutuliza, kufanya utamaduni wa utunzaji wa afya  ili uweze kukua. Japokuwa sio rahisi, lakini ni dhamira ya kweli, na ni matumani kwa ajili ya  huduma ya afya katoliki  ili iweze kuzidisha bidii kwa maana hiyo na kuwa kama kielelezo cha Kanisa hai na kama kiekelezea cha Kanisa ambalo linatoka nje. Amewatakia waendelee katika mwelekeo huo, wakikaribisha kazi yao kama huduma kwa msukumo na mshangao wa Roho, ambaye katika safari  hutenda  na kufanya ukutane  na hali nyingi zinazohitaji ukaribu na huruma. Papa anawasindikiza kwa sala na amesasisha shukrani zake na kuwapatia baraka. Hakusahau kuwaomba wamwombee. Amehitimisha.

HOTUBA YA PAPA 18 OKTOBA
18 October 2021, 16:16