Tafuta

Papa Francisko:Usitafute sifa,zama kwa huruma na hudumia maskini kama Yesu

Papa Francisko mara baada ya kuwaweka wakfu Monsinyo Guido Marini na Monsinyo Andrés Gabriel Ferrada Moreira,kuwa maaskofu,baadaye katika uwanja wa Mtakatifu Petro ametoa tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana.Akifafanua Injili ya siku,ameshauri kutotafuta sifa bali kuzama katika ubatizo wa Yesu na kwamba kuna watu wengi wana njaa ulimwenguni na wengine wanafanya kazi lakini hawawezi kuwa na chakula cha kutosha kwa mwezi mzima.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 17 Oktoba 2021, Papa Francisko mara baada ya kumaliza misa ya kuwaweka wakfu maaskofu wawili wa kanisa, katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ametoa tafakari yake pia kwa waamini na mahujaji waliokosanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican kabla ya sala ya Malaika wa Bwana. Akianza tafakari hiyo  amesema:  "Injili la liturjia ya leo (Mk 10, 35-45) inasimulia kuwa mitume wawili Yakobo na Yohane waliomba Yesu kukaa siku moja karibu na Yeye katika utukufu wake" na utafikiri kama mawaziri wakuu, kitu kama hicho Pa ameongeza kusema. Lakini mitume wengine wakasia na kukasirika. Kwa maana hiyo Yesu kwa uvumilivu alitoa mafunzo makuu kwamba utukufu wa kweli haupatikani kwa kujiinua juu ya wengine lakini kwa kuishi kikamilifu katika Ubatizo ambao Yesu ataupokea tangu happ taratibu akielekea Yerusalemu yaani msalaba. Papa Francisko ameuliza, je ina maana gani? Neno ubatizo maana yake ni kuzama kwa huruma  yake, Yesu alizama katika kifo kwa kutoa maisha yake ili kutukomboa. Utukufu wake,  yaani utukufu wa Mungu ni upendo ambao unatenda huduma,  si nguvu inayopendelea kutawala,  hapana. Ni upendo ambao unatenda huduma. Kwa maana hiyo Yesu alimaliza akiwaeleza wanafunzi wake na hata sisi pia kwamba “ anayetaka kuwa mkubwa kwenu atakuwa mtumishi wenu”( Mk 10,43). Ili kuwa mkubwa lazima kwenda katika njia ya huduma na kuhudumia wengine.

Papa Francisko amesema, tupo mbele ya mantiki mbili tofauti: wanafunzi wanataka kuonekana sifa zao na Yesu anataka kuzama. Maneno haya mawili, la kwanza linaeleza mantiki ya kidunia ambayo sisi sote daima tunashiwishika kuishi mambo yote kufikia mahusiano ili kukuza upendeleo wetu, wa kupanda ngazi za mafanikio na  ili kufikia nafasi ya juu. Utafutaji wa sifa binafsi unaweza kuwa ugonjwa wa roho, amebainisha Papa kwamba "kwa kufunika hadi nyuma ya nia nzuri: kwa mfano, wakati nyuma ya wema tunao tenda na kuhubiri, tunajifuta kiukweli sisi wenyewe na uthibitisho wetu". Kwa maaa ya kwenda mbele sisi wenyewe kwa kujikweza na hiyo hata katika Kanisa yanaonekana, Papa amesema. Je ni mara ngapi  sisi wakristo ambao tunapaswa kuwa wahudumu, tunatafuta kujikweza na kwenda mbele… Lakini daima tunahitaji kuhakikisha nia za kweli za moyo na kujiulza : “ kwanini napeleka mbele kazi hii na wajibu huo? Ni kwa ajili ya kutoa huduma au kwa ajili ya kuonekana, kutangazwa na  kusifiwa? Mantiki hiyo ya kiduna  kwa hakika Yesu anaipinga na kuweka yake kwamba badala ya  kujikweza juu ya wengine, ni lazima ushuke chini  ili kuhudumia. Badala ya kutaka sifa juu ya wengine, ni vema ukazama katika maisha ya wengine.

Papa amebainisha jinsi ambavyo alikuwa anatazama programu  moja ya  “A Sua immagine”, kuhusu huduma ya Caritas ambayo watu wasikose chakula. Ni wasiwasi mkubwa wa njaa ya wengine, ni kuwa na wasi wasi  wa mahitaji ya wengine. Wenye kuhitaji ni wengi sana leo hii na hasa baada ya janga wamekuwa zaidi. Inatakiwa kuwatazama na kuinama chini katika huduma na sio kujikweza na utukufu binafsi”, Papa ameshauri. La pili ndilo hilo la kuzama. Yesu anatuomba kuzama  lakini ni kwa namna gani ya kuzama?  Ni kuwa na huruma katika maisha ya wale ambao tunakutana nao kama yeye alivyofanya. Pale tunaona njaa. Lakini je sisi tuunawaoneha huruma watu wengi wenye njaa? Ikiwa sisi ttuko mbele chakula ambacho ni neema ya Mungu , tumepata kula, lakini kuna watu wengi ambao wanafanya kazi na hawapati chakula cha kutosha kwa ajili ya mwezi mzima. Papa ameomba wafikirie hilo. Kuzama kwa huruma  na  kuwa na huruma siyo jambo la kisomo,  kwa sababu kuna watu wengu wana njaa… Kuwa na huruma ya maisha ya wale ambao tunakutana nao kama Yesu alivyofanya na aliwakaribia kwa huruma.

Tumtazame Bwana aliyesulibiwa, alizama hadi mwisho katika historia ya majeraha yetu na tutagundua namna anavyotenda Mungu. Tunamwona kuwa Yeye hakubaki juu mbinguni. Kututazama kutoka juu, badala yake alijishusha na kuutosha miguu. Mungu ni upendo na upendo ni mnyenyekevu, haujikwezi, lakini unashuka chini kama mvua ambayo inanyesha chini ya ardhi na kuleta maisha. Je ni jinsi gani ya kuweka yote katika mwelekeo wa Yesu, kutoka katika kujionesha hadi kufikia kuzama, kutoka katika mantiki  kutaka sifa hadi katika huduma? Papa Francisko kwa kujibu amesema inahitaji juhudi , lakini peke yetu haitoshi  ni ngumu, japokuwa  ndani mwetu tuna nguvu ambayo inatusaidia. Nguvu hiyo ni ubatizo, ule wa kuzama na  Yesu, ambao tuliupokea kwa neema na ambao unatuongoza, unatusukuma kufuatana sio kutafuta mafao yetu binafsi ,  lakini kujiweka kwenye huduma. Ni neema, na moto wa Roho Mtakatifu ambao umewasha ndani mwetu, unaotakiwa kukuzwa

Papa ameomba leo hii Roho Mtakatfu ambaye anapyaisha ndani mwetu neema ya Ubatizo, ili kuzama katika Yesu na kwa namna ya kuwa watumishi , kwa ajili ya utumishi  kama Yeye alivyo fanya kwetu sisi. Tusali kwa mama Maria kwa kuwa yeye ni mkuu zaidi ambaye hakutafuta sifa maana alikuwa ni  mnyenyekevu mtumishi wa Bwana na yeye amezama katika huduma zetu ili atusaidia kukutana na Yesu.

TAFAKARI YA PAPA KWA SALA YA MALAIKA WA BWANA 17 OKT
17 October 2021, 12:58