Tafuta

Papa Francisko:Sinodi ni kwa ajili ya wote katika usikivu wa Roho Mtakatifu

Papa ametoa tafakari ya kuanza mchakato wa sinodi,ambapo ataizindua rasmi Dominika 10 Oktoba 2021,na Misa Takatifu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.Wakati wa mkutano wa maandalizi Papa amesisitiza "hakuna haja ya kufanya Kanisa lingine bali liwe Kanisa tofauti ambalo liko wazi kwa ajili ya mapya ambayo Mungu anataka kushauri kwa kujiweka katika usikivu,kutembea na roho ambaye anafanya dunia kuwa mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Sinodi ni mchakato ambao haukosi hatari, lakini pia ni hatua ya kutimiza kwa pamoja ili kupokea fursa nyingi. Ni tafakari ya Papa Francisko aliyotoa Jumamosi tarehe 9 Oktoba 2021, wakati siku ya kutafakari kwenye Ukumbi wa Sinodi ya maandalizi ya uzinduzi rasimi utakaofanyika Domika tarehe 10 Oktoba. Papa awali ya yote  ameshukuru wote waliotoka sehemu mbali mbali na Kanisa ili kushiriki mchakato wa kisinodi kuanzia katika moyo wa maswali na matumaini. Papa amesema Sinodi siyo bunge na walauchunguzi  lakini ni kipinidi cha kikanisa na kiongozi ni Roho Mtakatifu. Katika mwanzo wa hotuba yake Papa Francisko ameleekeza maneno matatu: muungano, ushiriki na utume ambayo kwa hakika ndiyo ufunguo wa Sinodi yenyewe. Amekumbusha kuwa umoja na utume ni vielelezo vya kitaalimungu. Hivyo vinaonesha huduma ya Kanisa na ambavyo ni vema kufanya kumbukumbu. Mtaguso wa Vatican II , umeweka wazi kuwa muungano unajieleza wenyewe katika asili ya Kanisa na wakati huo huo Kanisa limepokea utume wa kutangaza na kukarabati kwa watu wote ufalme wa Kristo na Mungu. Mtakatifu Paulo VI alitaka kujikita kwa kina na maneno hayo mawili ya Muungango na utume ambao ni mwalimu kiongozi yaliyotangazwa na Mtaguso. Kwa kufunga Sinodi ya 1985 hata Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka kueleza kuwa asili ya Kanisa ni ya Koinonia kwa njia hiyo, utume unataka kuwa ishara ya kina ya muungano wa familia ya mwanadamu na Mungu.

Tafakari ya Sinodi
Tafakari ya Sinodi

“Muungano na utume unabaki maneno ya kufikirika tu ikiwa mazoea ya Kanisa hayakuzwi na ambayo yanaonesha  kwa udhati wa kisinodi katika kila hatua ya safari na ya kazi, kuhamasisha ushiriki wa kweli wa kila mmoja. Ningependa kusema kwamba kuadhimisha Sinodi daima ni nzuri na muhimu, lakini inakuwa muafaka  ikiwa inakuwa dhihirisho hai la kuwa Kanisa, la kutenda linaloshirikishwa kweli. Na huo hauwezi kutokuwa mtindo unaohitajika wa imani. Ushiriki ni muhimu wa imani ya ubatizo. Kutoka katika ubatizo na hadhi ya wana wa Mungu licha ya tofauti za huduma na karama. Kwa maana hiyo sisi sote tunaalikwa kushiriki katika maisha ya Kanisa na utume wake. Ikiwa unakosa ushiriki wa kweli kwa watu wote wa Mungu, hotuba zote kuhusu Mungunano, ziko hatari ya kubaki nia tu”.

Kwa upande huu tumepiga hatua ya mbele, lakini bado kuna ugumu fulani na tunalazimika kurekodi ugumu na mateso ya wafanyakazi wengi wa wachungaji, wa mashirika ya ushiriki katika majimbo na maparokia, wanawake ambao bado wako pembezoni. Kila mtu anashiriki na ni ahadi ya lazima ya kikanisa ambayo haiwezi kuachwa! Papa Francisko amesisitiza kuwa sinodi itatoa fursa kubwa kwa ajili ya uongofu wa kichungaji ambao ni ufunguo wa kimisionari na hata wa kiekumeni, lakini ambao haukosi kuwa na hatari. Hatari ya kwanza ni ile ya muundo. Ikiwa tunazungumzia  juu ya sinodi, hatuwezi kujifurahisha na mtindo lakini tunahitaji hata zana na miundo ambayo inasaidia mazungumzo na ushirikishwaji wa watu wa Mungu hasa kati ya Mapadre na walei kwa sababu mara nyingi kuna hali ya usomi katika daraja la ukuhani ambalo linafanya kutengenisha na walei na mapadre baadaye wanageuka kuwa mabwana wa vibanda.

Sinodi inaweza kupunguzwa kama tukio lislo la kawaida, lakini likionekana kana kwamba mtu alikuwa akiangalia sura nzuri ya Kanisa bila kuweka mguu ndani yake. Badala yake Sinodi ni njia ya utambuzi mzuri wa kiroho, ambayo hatufanyi kutoa picha nzuri ya sisi wenyewe, bali kushirikiana vizuri katika kazi ya Mungu katika historia". Hatari ya pili ambayo Papa Francisko ameionesha ni ile ya kitaaluma. Papa amesema :“Kuifanya Sinodi iwe aina ya kikundi cha masomo na hotuba za kiutamaduni lakini za kufikirika juu ya shida za Kanisa na juu ya maovu ya ulimwengu; aina ya kuzungumza kisogo, ambapo tunaendelea kwa namna ya kijuu juu na kidunia na kuishia kuangukia ukawaida hasi wa kiitikadi na wa chama na kujitenga na ukweli wa Watu watakatifu wa Mungu kutoka katika maisha halisi ya jumuiya zote ulimwenguni.”

Hatari ya tatu ambayo imeelekezwa na Papa Francisko inatazama kishawishi cha kubaki pale pale. Ni kielelezo cha kusema ‘daima imefanyika  hivi' na ambayo ni sumu ya maisha katika Kanisa", Papa amesisitiza. "Wale wanaohamia katika upeo huo hata bila kujitambua, hufanya makosa kutochukua hatua yoyote katika wakati tunaoishi. Hatari ni kwamba mwishowe suluhisho za zamani zinapitishwa kwa shida mpya: kiraka cha kitambaa kibaya, ambacho mwishowe husababisha mchaniko mbaya zaidi (taz.Mt 9:16). Kwa sababu hiyo ni muhimu kwamba Sinodi iwe ya kweli, mchakato unaoendelea; kuhusisha, katika awamu tofauti kwa kuanzia chini, Makanisa mahalia, katika kazi ya kupenda na iliyojumuishwa, ambayo inaashiria mtindo wa umoja na ushiriki uliowekwa na utume”.

Papa Francisko ameshauri kuishi fursa hii ya mkutano, kusikiliza na kutafakari kama kipindi cha neema ambacho furaha ya Injili inaturuhusu kupokea angalau fursa tatu. Ya kwanza ni kujikita katika safari ambayo si kwa bahati mbaye lakini iwe ya kimuundo katika kuelekea Kanisa la sinodi: mahali palipo wazi ambapo kila mtu anahisi yuko nyumbani na anaweza kushiriki. Sinodi inatoa fursa ya kuwa Kanisa la kusikiliza. Kutoka kwenye “Kupumzika kwa miondoko yetu, kuacha mahangaiko yetu ya kichungaji na ili kusimama na kusikiliza. Kusikiliza Roho kwa kuabudu na kuomba. Ni jinsi gani tunakosa leo hii sala ya kuabudu! Wengi wamepoteza sio tabia tu, bali pia wazo la maana ya kuabudu. Kusikiliza kaka na dada juu ya matumaini na shida za imani katika maeneo  tofauti  ya ulimwengu, juu ya hitaji la haraka la kufanywa upya kwa ajili ya maisha ya kichungaji, juu ya ishara zinazotokana na hali halisi ya mahalia.”

Nembo ya Sinodi
Nembo ya Sinodi

Fursa ya tatu ni kuwa Kanisa la ukaribu. Papa anasisitiza kuwa mtindo wa Mung ,ni ukaribu,  wa huruma na upole. Ikiwa hii haitafanikiwa, hakutakuwa na Kanisa la ukaribu. “Sio kwa maneno tu, bali na uwepo, ili vifungo vikubwa vya urafiki viwe imara na jamii na ulimwengu: Kanisa ambalo halijitengi na maisha, lakini ambalo libabeba udhaifu na umaskini wa wakati wetu, kutunza majaraha na kuponya mioyo iliyovunjika kwa kuweka mafuta mazuri ya Mungu”. Hatupaswi kuunda Kanisa lingine , Papa Fransisko amethibitisha japokuwa ni kufanya Kanisa kuwa  tofauti na hii ndiyo changamoto. Kanisa wazi kuwa jipya ambalo Mungu anataka kulipendekeza”. Hii ndiyo sababu Papa anatumaini kwamba  katika Sinodi hii Roho Mtakatifu aweze kukaa ndani mwake. “Kwa sababu tunahitaji Roho, pumzi mpya ya Mungu, ambayo inatukomboa kutoka katika kufungwa kwetu, anafufua yaliyokufa, hufungua minyororo na hueneza furaha. Roho Mtakatifu ndiye anayetuongoza pale  ambapo Mungu anataka na sio pale ambapo mawazo na ladha zetu zingetupeleka”.

Kwa kuhitimisha Papa ameomba sala kwamba: “Njoo, Roho Mtakatifu. Wewe unayechochea lugha mpya na kuweka maneno ya uzima kwenye midomo yetu, tulinde dhidi ya kugeuka kuwa Kanisa la makumbusho, zuri lakini la ukimya, kwa siku za usoni na zilizopita na kidogo. Njoo kati yetu, kwa sababu katika uzoefu wa sinodi tusiishie katika majadiliano yaliyo tasa, upotovu, kutotii na unabii usiishie katika kila majadiliano yasiyofaa. Njoo, Roho Mtakatifu wa upendo, fungua mioyo yetu katika usikivu. Njoo, Roho wa utakatifu, ufanye upya watu watakatifu waamini wa Mungu. Njoo, muumbaji wa Roho, fanya uso wa dunia kuwa mpya.

TAFAKARI YA PAPA YA SINODI 9 OKTOBA 2021
09 October 2021, 13:31