Tafuta

Mahitaji ya kijamii ya Taranto Mahitaji ya kijamii ya Taranto 

Papa Francisko:Sayari tunayotarajia yahitaji uongofu wa mioyo

Sayari tunayotarajia inaomba wakati huo shauku na utashi wa kuikomboa.Sayari tunayotarajia inapaza sauti tayari tangu sasa kuwa na mtindo wa maisha uliopyaishwa mahali ambamo mazungira, kazi na wakati ujao havipingani kati yao,bali vina maelewano kamili.Ni kutoka ujumbe kwa njia ya video wa Papa FRancisko aliowatumia washiriki wa Jula la 49 la kijamii katoliki Italia 21-24 Oktoba 2021.

Papa Francisko zaidi ya ujumbe waliowatumia washiriki wa Wiki ya 49 ya Jamii ya Wakatoliki Italia vile vile Alhamisi 21 Oktoba 2021 aliwatumia hata ujumbe kwa njia ya video. Katika ujumbe huo  Papa amesema: “kaka na dada wapendwa ninawasalimia wote ambao mnaoshiriki Juma la 49 la Jamii ya Wakatoliki Italia ambayo imefunguliwa leo hii Taranto. Katika siku hizi mtatafakari kuhusu mada muhimu sana ambayo inatazama wakati wetu ujao na kizazi kijacho: ‘Sayari tunayotarajia. Kwa kuongezea anasema “Sayari hii tunayotarajia, inahitaji hasa uongofu ambao unafungulia tumaini. Sayari tunayotarajia inaomba wakati huo huo shauku na utashi wa kuikomboa. Sayari ambayo tunatarajia inapaza sauti tayari tangu sasa mtindo wa maisha uliopyaishwa, ambamo mazingira, kazi na wakati ujao havipingani kati yao, bali vina mawewano kamili.”

Kwa kutoa onyo Papa amesema “Haitakiwi kusahau kamwe kwamba kila kitu kimesukana” na kwa maana hiyo wazo lake limewandea kwa namna ya pekee na kuwatia moyo vijana kwamna “ ninatambua kuwa ni wawakilishi katika tukio hilo: tufundishe kutunza uumbaji! “Ninyi ni wakati uliopo, ninyi ni sayari ya leo, msijihisi katu kuwa pembeni mwa mipango, au tafakari. Ndoto zenu zinapaswa kuwa ndoto za watu na juu ya mazingira ambayo mna mengi ya kufundisha.” Hakuishia kwa vijana tu bali aliongeza kutazama sehemu nyingine kwamba: “Mniruhusu kuwambembeleza mama wote na mababa wote wa Taranto ambao wamelia na wanalia kwa sababu ya  vifo na mateso ya watoto wao. Ninawakumbatia na kuwakikishia maombi yangu. Na msali kwa ajili yangu, nami nitafanya hivyo kwa ajili yenu. Na Bwana awabariki!”. Amehitimisha ujumbe huo Papa Francisko.

Katika Wiki ya 49 ya Jamii ya Wakatoliki nchini Italia ambayo katikati yake wanaongozwa na Waraka wa ‘Laudato si’, pia hata wa   wa ‘Fratellii tutti’unawapa fursa ya kuingia kwa kina katika masuala yanayohusu jamii nzima ya Italia, lakini si hata katika mji huo wa Taranto. Juma limafunguliwa tarehe 21 hadi 24 Oktoba 2021 ambapo zaidi ya maaskofu 140, wawakilishi 670 wa majimbo 218, wataalam, wajumbe wa ulimwengu wa kisiasa, raia, na utamaduni wazungumzia mada kuhusu “sayari tunayotarajia. Mazingira, kazi, wakati ujao, vyote vinaunganika”. kwa lengo la kutafakari kwa kina juu ya mtindo mpya wa maendeleo na juu ya kuanzisha mpito wenye maono ya matarajio ya ikolojia fungamani.

Akitoa hotuba ya ufunguzi Kardinali Bassetti baada ya ule wa Papa Francisko amesema tukio hilo ni kiekelezo cha Kanisa linalojifungua na kuzungumza na ulimwengu. Wamejikita katika mji wa Taranto ambao kihistoria umekuwa na mkakati wa kimediteranea ambao unawakilisha  si tu katika moyo wa ustaarabu wa Italia lakini pia hata katika bahari inayoaribisha na kukubambatia familia ya Ibrahimu. Bahari ambamo inajikita katika dunia tatu za dini na utamaduni: wayahudi, wakristo na waislam ambao wanaweza kuishi kwa amani kama yalivyo kuwa matashi mema ya Giorgio La Pira”.

Wakati wa hotuba yake, Kardinali Bassetti aidha ameweza kutoa maswali kama vile, nini maana ya kuchukua wajibu katika karne ya XXI, utashi wa kuhamasisha haki ya kijamii? Awali ya yote amejibu kwamba ni kulinda na kuthamanisha kila hali, thamani isiyokanyagwa ya hadhi ya binadamu. Utu wa mwanadamu hawezi kunyonywa, hauwezi kuwa bidhaa na wala kuuawa. Hakuna sababu za kiuchumi zinazoweza kuhalalisha kila aina ya mtindo wa itumwa kimwili na kimaadili wa mwanaume na mwamke au mtoto. Kardinali ameonesha maskitiko mengi kuhusiana na ajali nyingi zinatokea katika muktadha wa kazi. Kwa maana hiyo inahitajika kuhamasisha haki ya raia na kijamii na kichukua wajibu kila siku katika maana hiyo. 

Katika pendekezo la Laudato si na ambalo linatushauri kueliendeleza na kuhamasisha ikolojia fungamani Kardnali Bassetti amekumbuka kuwa janga hata hivyo limetuachia urithi kwa bahati mbaya mgumu na usiohesabika katika mataifa maskini. Urithi mbaya pia ambao unaonekana vizuri katika mataifa yaliyo endelea kama Italia. Amekumbuka marehemu wengi waliokufa, matatizo mengi ya familia, hali ngumu za kiuchumi kwa makampuni na viwanda, hatimaye, tathmini ya kutisha na unyong’onyevu kijamii. Picha ya sasa ya maandamano na ghasia zinazoonekana katika viwanja mbali mbali kwenye miji ya italia, vinaonesha ni kwa jsi gani janga limeacha madhara. Kuna hali nyingi za kutokufarahi kijamii na ambazo zinaendelea kukua katika umbo la kijamii na kuonesha kwa maana nyingine mgogoro wa kibindamu, na mwanzo ulikuwa ni wahamiaji na sasa ni janga… amesisitiza Kardinali Bassetti.

 

22 October 2021, 15:52