Tafuta

Papa Francisko amekutana na washiriki wa Kongamano ka kitaifa la Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice. Papa Francisko amekutana na washiriki wa Kongamano ka kitaifa la Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice. 

Papa Francisko:mbele ya changamoto hatuwezi kutojali

Kwa hakika maneno matatu waliyochagaua,mshikamano,ushirikiano na uwajibikaji,unawakilisha misingi mitatu muhimu ya mafundisho jamii ya Kanisa ambayo yanatamani maisha ya mtu yaliyo wazi katika uhusiano na kama ncha ya uumbaji na kiini cha maisha ya kijamii,kiuchumi na kisiasa.Ndivyo Papa Francisko amewaeleza wawakilishi wa Kongamano la Kimataifa la Mfuko wa Centesimus Annus.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Kongamano la Kimataifa la Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice lilioanza tarehe 21 Oktoba jijini Vatican wa kuongozwa na kauli mbiu “Mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji: dawa kwa ajili ya kupambana na ukosefu wa haki, usawa na ubaguzi”. Tarehe 23 Oktoba 2021 kwa maana hiyo amesema kwamba Katika siku hizi wameshughulika na masuala makubwa na muhimu ya kauli mbiu  ambayo kwa hakika ni tafakari muhimu sana katika wakati ambao unakosa uhakika na hali ya wasiwasi inayoashiria kuwapo kwa watu wengi na jamii zinachochewa na mfumo wa uchumi ambao unaendelea kutupa maisha kwa jina la mungu pesa, ikisababisha mitazamo mibaya kwa rasilimali za Dunia na kuongezeka kwa aina nyingi za uovu. Mbele ya kukakabiliwa na hali hizi,  Papa amesema hatuwezi kubaki kutojali. Lakini jawabu la dhuluma na unyonyaji si kukashifu tu; awali ya yote ni kuhamasisha mema kwa vitendo: kukemea maovu lakini pia ni kuhamasisha mema. Papa amesema ni muhimu, tunahitaji: katika ardhi iliochafuliwa na utawala wa fedha tunahitaji mbegu nyingi ndogo ambazo zinaweza kufanya uchumi wa haki na wenye faida, kwa kiwango cha kibinadamu na anayestahili mwanadamu,na kuota ndoto. Tunahitaji uwezekano unaotimizwa, uhalisia ambao unatoa tumaini. Hii ina maana ya kuweka mafundisho ya kijamii ya Kanisa katika vitendo. Papa Francisko amesimulia jinsi ambavyo miaka minne iliyopita alitembelewa na mwanamke mmoja mchumi aliyekuwa na kazi katika serikali. Na alimwambia jinsi aliyokuwa ametafuta kufanya mazungumzo kati ya uchumi, ubinadamu, imani na dini na kwamba mazungumzo yalienda vizuri na kuendelea katika kikundi  cha tafakari. Lakini alipoandaa suala hilo hilo  katika kikundi kuhusu fedha, ubinadamu na dini hawakuweza hata kuanza. 

Kutokana na hilo amesema "ni jambo la kushangaza. Hiyo inafanya kufikiri. Mwanamke huyo alinifanya kuhisi kuwa fedha ilikuwa jambo lisiloachwa, maji na hewa ambayo mwishowe inakwsha na kubaki kama mnyororo wa Mtakatifu Antonia kama alivyo sema. Na kwa maana hiyo uzoefu labda unahitajika kwao". Kwa hakika maneno matatu waliyochagaua, mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji, unawakilisha misingi mitatu muhimu ya mafundisho jamii ya Kanisa ambayo yanatamani maisha ya mtu yaliyo wazi katika uhusiano  na kama ncha ya uumbaji na kiini cha maisha ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kwa mtazamo huu, umakini kwa mwanadamu na unajali ukamilifu wa mienendo ya kihistoria, mafundisho ya kijamii yanachangia maono ya ulimwengu ambayo yanapingana na mtu mbinafsi, kwani inategemea muungano kati ya watu na ina faida ya pamoja  kama lengo lake. Na wakati huo huo inapinga maono ya ujamaa usio wa kweli, ambao leo hii huibuka tena katika toleo jipya, lililofichwa katika mipango ya kiufundi ya kiteknolojia. Lakini hiyo sio jambo la kisiasa: mafundisho jamii ya Kanisa yametiwa nanga na Neno la Mungu, kuongoza michakato ya kukuza binadamu kuanzia imani kwa Mungu iliyofanywa na mwanadamu. Kwa sababu hii ni lazima kufuatwa, kupendwa na kuendelezwa: “tuwe na shauku ya mafundisho ya kijamii tena, tuyaeneze: ni hazina ya mapokeo ya kikanisa! Ni kwa kuyasoma kwamba wewe pia umehisi kuitwa kujitoa dhidi ya ukosefu wa usawa, ambao unaumiza hasa wadhaifu zaidi,na kufanya kazi kwa ajili ya udugu wa kweli na mzuri.

Papa Francisko akiendele na hotuba yake amesema kuwa mshikamano, ushirikiano, uwajibikaji: maneno matatu ambayo katika siku hizi yamekuwa  msingi wa tafakari yao na ambayo wanakumbuka kama fumbo lile lile la Mungu, ambaye ni Utatu. Mungu ni umoja wa Nafsi na anatuelekeza tujikamilishe kwa uwazi wa ukarimu kwa wengine (mshikamano), kwa kushirikiana na wengine (ushirikiano), kupitia kujitoa kwa wengine (wajibu). Na kufanya hivyo katika kila kielelezo cha maisha ya kijamii, kupitia mahusiano, kazi, kujitoa kwa raia, uhusiano na kazi ya uumbaji, siasa: katika kila nyanja ambayo leo hii tunalazimika zaidi ya wakati mwingine kutoa ushuhuda kwa wengine, kutoka nje,  sisi wenyewe, kujitoa bila malipo kwa ajili ya maendeleo ya jamii yenye uadilifu zaidi na yenye usawa, ambapo ubinafsi na masilahi ya upendeleo hayapo. Na wakati huo huo tumeitwa kutazama heshima kwa mwanadamu, uhuru wake, ulinzi wa historia yake isiyoweza kuvunjika. Hapa kuna dhamira ya kutekeleza mafundisho jamii ya Kanisa.

Katika kutekeleza maadili haya na mtindo huu wa maisha, tunajua, mara nyingi tunakwenda kinyume na wimbi, lakini  tukumbuke kila wakati kuwa hatuko peke yetu, Papa amebainisha. Mungu anakuja karibu nasi. Si kwa maneno, bali kwa uwepo wake: ndani ya Yesu Mungu alijifanyika mwili. Na pamoja na Yesu, ambaye alikuwa ndugu yetu, tunamtambua kwa kila mwanaume kuwa ndugu na katika kila mwanamke kuwa dada. Kwa kuuhuishwa na umoja huu wa ulimwengu, kama jamii inayoamini tunaweza kushirikiana bila hofu na kila mmoja kwa faida ya wote: bila kufungwa, bila maono ya kutengwa, bila upendeleo. Kama Wakristo tumeitwa kwa upendo bila mipaka na bila kizingiti, ishara na ushuhuda  kwamba tunaweza kupita zaidi ya kuta za ubinafsi na masilahi ya kibinafsi na ya kitaifa; zaidi ya nguvu ya pesa ambayo mara nyingi huamua sababu za watu; zaidi ya ua za itikadi, zinazogawanya na kukuza chuki; zaidi ya kizuizi chochote cha kihistoria na kiutamaduni na, juu ya yote, zaidi ya kutojali: utamaduni huo wa kutojali ambao, kwa bahati mbaya, ni wa kila siku.

Sote tunaweza kuwa ndugu na kwa hiyo tunaweza na lazima tufikiri na kufanya kazi kama ndugu wa wote. Inaweza kuonekana kama utopia isiyoweza kufikiwa. Lakini kinyume chake tunapendelea kuamini kwamba ni ndoto inayowezekana, kwa sababu ni ndoto ile ile ya Mungu wa Utatu. Kwa msaada wake ni ndoto ambayo inaweza kuanza kutimia hata katika ulimwengu huu, Papa amesisitiza. Kwa hiyo Papa amesema ni kazi kubwa kujenga dunia yenye umoja, haki na usawa. Kwa mwamini si kitu cha vitendo kilichojitenga na mafundisho, lakini ni kutoa mwili kwa imani, kwa sifa ya Mungu, mpenda binadamu na mpenda maisha. Kwa wote Papa amesema wema ambao wanamtendea kila mwanadamu duniani yanafurahisha moyo wa Mungu mbinguni. Waendelee na safari yao kwa ujasiri. Papa anawasindikiza kwa maombi na amewabariki kwa kujitoa kwao. Lakini wasisahau kumwaombea na Yeye.

23 October 2021, 17:14