Tafuta

2021.10.22 SS Papa alikutana na wata wa Shirika la watawa wa kike wa Don Bosco 2021.10.22 SS Papa alikutana na wata wa Shirika la watawa wa kike wa Don Bosco  

Papa awaonya watawa waepuke udunia,ibilisi anaingia nyumba za watawa

Papa Francisko ametembelea nyumba kuu ya Shirika la wana wa Maria wa Msaada(Wasalesiani)waliokuwa kwenye mkutano mkuu.Akizungumza nao amewaomba wawe jumuiya inayozaa matunda na wanawake wa matumaini katika kipindi hiki kidhaifu na kisicho na uhakika.Amehimiza wakae karibu na maskini na vijana na kuwa daima waaminifu katika karama asili ya waanzilishi wao.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican.

Papa Francisko alikaribishwa na watawa wa Wasalesiani wakiwa katika mkutano mkuu wa shirika katika nyumba kuu Ijumaa tarehe 22 Oktoba 2021. Katika siku hizi  za kazi yao Papa emesema walingozwa na mada “ jumuiya inayozaa ya maisha katika moyo wa kisasa, pia kwa kuongozwa na maneno  ya Maria katika arusi ya Kanisa, “fanyeni atakayowaelekeza (Yh 2,5). Ni ishara nzuri sana ya Mama bila kuwa binafsi, bali kwa ajili ya kile anachokielekeza Yesu. Kuiga Maria ni kufanya hivyo hivyo Papa alisisitiza.  Kwa upande mmoja, alikumbuka muktadha wa kijamii na  kiutamaduni, unaoangaziwa na mivutano na changamoto ambazo wakati mwingine ni kubwa, kama zile zinazo endelea kusababishwa na janga; Na wakati huo huo, ni kusikiliza neno la Bwana, mapenzi yake, hasa katika wakati huu dhaifu na usio na uhakika, na aina za umaskini ambazo shida ya sasa imezalisha na kuongezeka.Kuna umaskini uliongezeka, hata umaskini uliojificha. Familia nyingi tajiri, au angalau katika tabaka la kati, hawana kile wanachohitaji ili kuishi. Janga hili limesababisha mauaji mengi sana,Papa amesema.

Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco

Kuamsha hali mpya ya uzalishaji wa ufundi wa Taasisi, ndiyo  lengo ambalo wamejiwekea. Ni mtazamo muhimu wa kuitikia mahitaji ya ulimwengu wa leo, unaohitaji kugundua katika maisha yaliyowekwa wakfu lile angazo la yale ambayo Baba, kupitia Mwana katika Roho, anatimiza kwa upendo wake, wema wake, uzuri wake (CIVCSVA katika viriba vipya vya divai, 6). Papa ameongeza kusema kwamba hii haimaanishi kukataa udhaifu na shida zilizopo katika jamii, lakini kuamini kwamba hali hii inaweza kuwasaidia kubadilisha leo hii kuwa kairós, wakati mzuri wa kwenda kwenye mizizi ya karama ili  kufanya kazi juu ya muhimu wake, kujigundua kwa upya binafsi, uzuri wa maisha ya wakfu. Changamoto hii amesema inawaalika  kujipyaisha kwao kwa Mungu wakati huu, kama wanawake na jumuiya zinazojiruhusu kusahihishwa na Bwana na kwa ukweli. Kutokana na hiyo wanaweza kuwa watawa wa unabii wa Injili, kushuhudia Kristo na mtindo wake wa maisha.

Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco

Papa Francsiko amesema kuwa katika Mtaguso wa II wa Vatican  ulionesha Kanisa kwa njia hii, ambayo ni njia ya Mungu: mwili katika historia, ulizamishwa katika hali ya kibinadamu. Lakini hii inadhihirisha kuwa na mizizi thabiti katika Kristo katika huruma ya ulimwengu  na katika aina na sura zao. Papa amehimiza wasisahau kwamba ubaya mbaya kabisa ambao unaweza kutokea katika Kanisa ni ulimwengu wa kiroho. Papa amesema kwamba inaonekana kuwa mbaya zaidi kuliko dhambi, kwa sababu ulimwengu wa kiroho ni roho ya hila inayochukua nafasi ya kutangaza, ambayo inachukua nafasi ya imani, ambayo inachukua nafasi ya Roho Mtakatifu. Padre De Lubac, katika kitabu cha tafakari juu ya Kanisa (Méditation sur l'Eglise), anazungumza haya katika kurasa nne za mwishomwisho. Papa amewaomba wakitafute kitabu hicho na kukisoma. Anasema "hii ni kali sana: ulimwengu wa kiroho ni uovu mbaya zaidi unaoweza kutokea katika Kanisa, mbaya zaidi kuliko kashfa ya wakati wa Mapapa. Ina nguvu. Ibilisi huingia kwenye nyumba za kitawa katika njia hii. Inanisaidia kuelewa jinsi shetani anavyoingia kati yetu", Papa ameeleza.

Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco

Na sio dhambi tu, sio mtawa mmoja anayeua mwingine, kashfa!  au anayemtukana mwingine, hapana, hii ni dhambi mbaya, wote wanashangaa na kutoa kashfa, wote wanaomba msamaha ... Papa amezidi kueleza. Yesu anatufundisha jinsi shetani anavyoingia na kusema hivi: “Pepo mchafu akishatolewa. mtu, huenda zake, anazurura jangwani, akichoka, halafu anasema: 'Nitarudi nyumbani kwangu kuona hali yake'. Nyumba ambayo ilikuwa safi, nzuri, na iliyoandaliwa vizuri. Baadaye anakwenda na kuwatafuta wengine  saba walio wabaya zaidi yake, wanaingia ndani ya nyumba ile. Lakini hawingii kwa kulazimisha, hapana, wanaingia kwa heshima: wanapiga kengele, wanasema hodi. Ni mashetani wenye adabu. Hatuoni kwamba wanaingia. Kwa maana hiyo wanaingia polepole ndani mwetu.  Jinsi ya uzuri tu,.... Na mwishowe, hali ya mtu huyo inakuwa ni mbaya zaidi kuliko mwanzo. Hivyo hutokea katika ulimwengu wa kiroho, Papa amefafanua.

 

[ Photo Embed: Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco]Papa Francisko akiendelea na ushauri huo kuhusu ushuhuda wa maisha ya kijumuiya na huduma amesema "Watu ambao wameacha kila kitu, wamekataa ndoa, wameacha watoto, familia zao ... na kuishia katika mambo ya kidunia,na kuwa na wasiwasi juu ya mambo hayo ... Na upeo wa macho. hufungwa, kwa sababu wanasema kwa kulalamika taama hata hakuniangalia, yule alinitukana, yule ... Migogoro ya ndani ambayo inafunga peo za maisha ya wakfu. Tafadhali epukeni na ondokeni katika roho ya kiulimwengu, Papa amehimiza watawa hao. Na pia suala la hadhi: Mimi ni mtawa,  mimi ni mwaminifu ... Chunguzeni hili. Hii ndio mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea. Ni kama […] ambayo huchukua nguvu zako polepole. Na badala ya kuwa wanawake waliowekwa wakfu kwa Mungu, wanakuwa ni wanawake wasio na adhabuu na ambao hawazai matunda ya kiroho. Papa alitumia neno la kiitaliano (Zitella) ikiwa na maana ya kuwa tasa kiroho[...]

Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
Papa akitoa hotuba yake kwa watawa wa Don Bosco
23 October 2021, 16:23